Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Eti 'nimesingiziwa na tume imesema uongo'

Mwalimu nae 1995 alisema uongo?

Dhambi imezoeleka hata inaonekana ni sahihi!

No remorse!
 
Lowassa will go down in history as one of the most corrupt figures in our country. Nadhani this episode will forever change the political landscape in our country. Who knws?

Yes, Mwakyembe alitangaza kwamba yeyote mwenye ushahidi au chochote aende mbele ya kamati. Its nonsense kulalamika kwamba hawakutendewa haki wakati walipewa opportunity ya kutoa duku duku lao mbele ya kamati.

Thanks Harrison and members, this was one of the best report I have ever read in my life!
 
Msabaha na Karamgai nao wameamua Kujiuzulu. Ila Lowasa anasisitiza kuwa Tume ya Mwakyembe imesema uongo. Sasa hivi wabunge wa CCM "Mh. Joseph Selukemba (Mb-Kigoma)et al" wanasema EL ni shujaa. Hii ni AIBU kubwa kwa wabunge wa aina hiyo.
 
EL kaishiwa HOJA mpaka anajifananisha na "YESU" Kristo eti ametolewa kafara. Yeye arudi tu Monduli asubiri hukumu ya wadanganyika, arudishe fedha ili gharama za Umeme zishuke.
 
Wakuu,
Tetesi za awali zinasema EL na karamagi wanahusika pia kwenye Buzwagi saga. Hii siyo "Bangusilo"

Halafu kumbe sababu ya Spika kusisitiza kwenye Hadidu za Rejea kuwa Mwakyembe asiguse IPTL ni kwa sababu Mkuu mwenyewe "JK" IPTL ndiyo ka-mradi kake.
 
Chenge anatapatapa, siku ya kufa nyani miti yote huteleza, anajua fika siku ya siku imashajongea...
 
Kamati imesema haikuweza kumuita kwa sababu , maneno yalisemwa out of record, lakini papo hapo akumbuke yeye ndio kiongozi wa Serekali hivyo inapotokea makosa makubwa kama hayo na yeye asichukue hatua yoyote au asijue kinachoendelea katika jambo zito kama hilo ni kuonyesha kwamba ana mapungufu.
 
Napenda kuchukua fursa hii kutoa hongera zangu nyingi sana kwa wana JF wote popote walipo duniani katika michango yenu mbali mbali hapa ukumbini kuhusiana na vita dhidi ya ufisadi mkubwa unaofanywa dhidi ya nchi yetu na wale tuliowapa madaraka ya kutuongoza.

Msikate tamaa katika vita hii tunapata ushindi kidogo kidogo, kelele zetu za kupinga ufisadi imeshamuangusha kigogo mmoja bado wengi wameshika madaraka lakini tutaendelea kupambana nao katika kila kona na hatimaye kuikomboa nchi yetu toka mikononi mwa mafisadi.

Nyerere alituambia kuhusu uadilifu wa Lowassa, kama aliyoyasema yangesikilizwa basi Lowassa asingestahili kupewa hata ujumbe wa nyumba kumi kumi achilia mbali uwaziri mkuu.

Kwa mara nyingine tena, ahsanteni sana kwa juhudi zenu za kupambana na ufisadi na hongera sana.

Alutta Continua!

Mungu ibariki Tanzania
 
Mugo"The Great";137099 said:
Msabaha na Karamgai nao wameamua Kujiuzulu. Ila Lowasa anasisitiza kuwa Tume ya Mwakyembe imesema uongo. Sasa hivi wabunge wa sisiemu "Mh. Joseph Selukemba (Mb-Kigoma)et al" wanasema EL ni shujaa. Hii ni AIBU kubwa kwa wabunge wa aina hiyo.

Mugo ndo maana nasema inabidi tuanze na hawa wawakilishi uchwara wanaotetea njaa zao kwa maslahi ya mda mfupi. We need fundamental changes tuanze kutuma wabunge responsible Dodoma. I know this chap yaani ukimuona barabarani utafikiri kichwa kina busara, but Iam afraid kichwani ni tope! Hawawezi hata kufanya analysis wakaangalia the price baing paid by their poverty stricken voters! Its so sad kuwa na watu kama hawa bungeni. Anyway tutafika, safari ndiyo imeanza kabisa.

Honestly speaking, simchukii Lowassa in his personal level, but his incompetence has been at the detriment of millions of our people. Ni mtu mroho, mpenda madaraka na utajiri! Yaani sijui huyu bwana tumhukumu vipi! Ni vema akarudi Monduli akaangalie mifugo yake. Yaani nina hasira naye sana! Iam sorry, but ninapoona mtu anamtetea Lowassa, I tend to think otherwise of that person! The good news is the report of Mwakyembe is in SWAHILI..nitaipeleka kijijini ASAP watu waipitie....
 
Na hiyo Natural Justice anayo sema Lowasa, Mbona hhaioni inapokuja issue ina maslahi kwa Wananchi , Kama haki ya Kupata Umeme wa Nafuu, Kupewa report za Uchunguzi zinazowahusu Viongozi au zinazo husu Serekali aliyo kuwa anaiongoza.

Kuwakaripia walio chini yake kama watoto wadogo, nafikiri Ma Dc wengi watakuwa wanasherekea, pamoja na Mawaziri wenzake.
 
Wa tatu ni waziri wa EAC, Dr Ibrahim Msabaha, ameomba kuwajibika kwa pamoja kwa kujiuzuru nafasi yake serikalini kutokana na taarifa ya kamati ya Dr Mwakyembe.
 
  1. Kumbe Lowasa alimaliza tembo mzima halafu akatuambia watanzania tugawane kasungura; dah, mshenzi kweli jamaa huyu.
  2. Kama Rais huyu alipinga kujiuzulu kwa Ballali na baadaye akatangaza kumfukuza kazi, ninategemea atafanya vivyo hivyo safari hii kwa Lowassa, Kalamagi na Msabaha.
  3. Ndege ya Lowassa imepata pancha huko angani.
  4. Watu wate waliohusika na upotevu wa mamilioni ya pesa za umma wasiishie kufukuzwa kazi tu na kuachiwa waendelee kudumbua walichoiba, lazima wachukuliwe hatua za kisheria ili siyo tu warudishe walichoiba bali pia waweze kutumikia vifungo vya muda mrefu jela na kufanyishwa kazi za suluba.
  5. Matokeo ya tume ya Mwakyembe yanaonyesha kuwa TAKUKURU haifanyi kazi zake ipasavyo. Ni matumaini yangu kuwa Rais ameliona hilo na atamchukulia hatua kali pia Mkurugenzi wa TAKUKURU kwa kulidanganya taifa kuwa taratibu za utoaji wa tenda hiyo hazikukiuka sheria yoyote na wala hakukuwa na shinikizo la rushwa.
 
Wote walionufaika na ufisadi wao wa Richmonduli wafilisiwe na wafunguliwe mashtaka haraka sana. Kujiuzulu pekee yake haitoshi na hao wadosi warudishe $172 milioni zetu haraka sana na kama wako nje ya nchi tuombe interpol watusaidie na bank account zao frozen.
 
Kumkoma Nyani mbele kwa mbele..



Wahusika wote waanikwe...JK hii ni opportunity ya pekee kufanya lile linaloweza kurudisha iman za Wa-TZ waliochoka ktk kila secta.

Baada ha hili skendo tunahitaji... Uchunguzi wa kila Idara Nyeti..usiomuonee Haya mtu yoyote ktk...wala usiomuonee Huruma yoyote ktk kutekeleza wajibu...usipofanya bora ...UTACHEKWA..UTASIMANGWA NA WAPINZANI TUTAFANYA MAANDAMANO AMBAYO HAYAJAWAHI KUTOKEA TANZANIA TANGU UHURU...na HAPO NDIPO UTAKAPOJUA NGUVU ZA UMMA.
 
Nafikiri nchi nzima ina matatizo, yaani kila kitu kinakwenda hovyo hovyo.

Nafikiri wizara zinaongozwa kjinga kijinga na hiyo ni mbali ya matatizo ya rushwa.

Hawa viongozi hawatakiwi kujiuzulu wanatakiwa kuwa sacked.

Na hili ndilo tatizo.
Leo hapa tunajipongeza kwa Lowasa na wenzake kujiuzuru na tunasahau system nzima iliyooza tokea mesenja mpaka Rais mwenyewe kiutendaji.

Tuufurahie kuubadilisha mfumo mzima wa utendaji na uwajibikaji kila sehemu; kuanzia kwenye serikali za vijijini na kwetu sote binafsi.

Matatizo ni makubwa zaidi, na binafsi sina sababu ya kufurahia chochote hapa.
 
Hata Kikwete naye ajiuzulu. Kulikuwa na ushahidi wa kutosha muda mrefu tu wa ufisadi mkubwa uliofanywa na mawaziri mbali mbali lakini hakuwa tayari kumfukuza kazi yeyote. Kikwete pia kazi imemshinda na naamini hata yeye si safi ndio maana alikuwa anaogopa kumfukuza kazi waziri yeyote, bora ajiuzulu tu...🙁
 
JK huu ndio mwanya wa kurudisha imani safisha kabisa kila idara.

Hii isiwe ndio kulisahaulisha la BOT. bado kule tumeelekeza macho na masikio, Kuna issue ya import support, kuna issue ya Kiwira, kuna Nyumba za serikali, kuna issue ya Container Terminal jamani tutafika?

Naona mama Lowasa anatia huruma sana hapa kwenye picha. Mama pole sana kila kitu nitalipwa hapa hapa duniani.
 
Hili la PM limefikia ukomo, sioni kama JK atakuwa na sababu ya kumkumbatia, akifanya hivyo wananchi hatutamwelewa kabisa.
PM hana shina na ajira, hata akifirisiwa bado anao ujuzi wa kisanii, atakuwa mjarasilimali kwa kuanzisha shughuli za comedy. maana usanii wake ni wa hali ya juu, ni kwa JKN aligonga mwamba.
 
Hata Kikwete naye ajiuzulu. Kulikuwa na ushahidi wa kutosha muda mrefu tu wa ufisadi mkubwa uliofanywa na mawaziri mbali mbali lakini hakuwa tayari kumfukuza kazi yeyote. Kikwete pia kazi imemshinda na naamini hata yeye si safi ndio maana alikuwa anaogopa kumfukuza kazi waziri yeyote, bora ajiuzulu tu...🙁

For sure na Kikwete naye ni useless kwani haiwezekani watu wote ambao kawateua yeye wanafanya madude namna hii kuanzia kwa waziri mkuu hadi PCCB na Mwanyika. Lakini hii ni watz wenyewe ambao walimpa u-presidaa mchekeshaji kwa hiyo watz tusilalamike sana kwani LIPUMBA aliwaambia kuwa huyo anafaa kuwa waziri wa michezo na burudani.
 
Karamagi hatujamalizana naye maana antuibia sana kule container bandarini...lazima tumwanike hapa na uchafu wake wote,pressure pressure mwanangu tukilala watatugeuzia kibao maana uzoefu unaonyesha hivyo
 
Back
Top Bottom