Kashfa ya Watergate iliyomgo'a Richard Nixon kwenye kiti chake cha Urais

Kashfa ya Watergate iliyomgo'a Richard Nixon kwenye kiti chake cha Urais

mcTobby

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2018
Posts
4,072
Reaction score
12,119
Naam am back,

Wadau wa JF je mnaikumbuka kashfa au skendo maarufu ya kisiasa kuwahi kutokea na kuitikisa Marekani miaka ile ya 1970s?

Hii ilikuwa ni kashfa kubwa ya kisiasa iliyomkumba rais wa 37 wa marekani wakati huo bwana Richard nixon iliyopelekea mgogoro mkubwa wa kikatiba miaka ya mwanzoni mwa 1970.

Iko hivi skendo hii ilianza kama utani utani hivi ambapo ilipokuja kulipuka baadaye ikamuondosha anko Richie kwenye kiti chake cha urais.

Ni kashfa gani hiyo ? Twende kazi . Siku moja tarehe 17 mwezi juni 1972 kwenye mtaa fulani katikati mwa jiji la Washington d.c. kuna uhalifu ulifanyika ambapo "vibaka" watano walikamatwa na maafisa wa kiusalama kwa tuhuma za kuvunja jengo moja na kuingia ndani kwa kusudio la uporaji. Jengo hilo halikuwa lingine bali ni jengo la watergate building.

Jengo hili la ghorofa ndilo lililokuwa makao makuu la chama cha democratic ambapo pia lilikuwa upande mmoja wa hili jengo lilikuwa ni hotel yenye hadhi.

Bahati nzuri walidakwa . Lakini hawa vibaka walipofanyiwa upekuzi vizuri hawakuwa wa kawaida . Kwa maana ya kwamba hawakuwa wameiba kitu chochote ndani ya jengo hilo. Baada ya polisi kushindwa kuielewa hii kesi ya hawa jamaa watano wakaamua kuwatupia Fbi

Sasa rasmi makachero wakawa wameinunua hii kesi ili kuifanyia upelelezi wa kina. Na kweli ikagundulika hawa jamaa hawakuwa vibaka , bali ni timu au task force ilyotumwa maalum kwa ajili ya kudukua mawasiliano na mazungumzo yote ya viongozi wa democratic kwa siri. Kwa maana ya "device bugging". Yaani hawa jamaa walibainika walikuwa wanafunga came na vinasa sauti kwenye simu zile za mezani na ukutani kwenye ofisi za viongozi wa juu wa chama cha democratic.

Kati ya hao vibaka watano, mmoja alibainika kuwa afisa mstaafu wa CIA. Na upelelezi wa fbi ulipoendelea ilibainika hawa vibaka walikuwa na uhusiano na kamati ya kampeni ya Richard nixon mrepublican. (Chawa wa Nixon au team NIxon).

Kutokana na upelelezi huu wa awali fbi wakaamua kuchimba zaidi kutaka kujua ni mchezo gani mchafu wa kisiasa unaoendelea nyuma ya pazia dhidi ya wagombea wa upande wa democratic kwenye uchaguzi uliokuwa unatarajiwa kufanyika siku chache zijazo. FBI walipofukua zaidi ikabainika ya kuwa , nixon na kamati yake ya kampeni walikuwa kwenye harakati za kuwadukua (spying) wapinzani wao yaani democratic lengo tu ni kuvuruga harakati zao za uchaguzi.

Ikabainika ya kwamba timu ya kampeni ya Richard nixon iliyojulikana kama CREEP(committee for the re _election of the president. ) ilikuwa ikitengeneza pesa chafu za madili za ku support kamapeni kupitia mgongo wa nixon zaidi ya dola milioni 60. Pesa hizi nyingi zilipatikana kifisadi.

Kwa maana ya kwamba timu kampeni ya nixon ilikuwa inazilazimisha makampuni na mashirika yanayofanya tenda na serikali ya marekani kuchangia mfuko wa kampeni ili zipate upendeleo pale zabuni na tenda za serikali zitakapotoka.

Hivyo makampuni na mashirika kwa sababu ya kuogopa kupoteza tenda ,ikabidi zitoe pesa japo kishingo upande. Na la zaidi ni kwamba kumbe kiasi fulani cha hizi pesa chafu za madili zilikuwa zinaenda moja kwa moja kwenye akaunti binafsi ya kampeni manager wa Richard nixon bwana John Mitchell ambaye kwa wakati huo alikuwa ni mwanasheria mkuu wa serikali mstaafu. Lengo kuu iliku ni kuwachafua wagombea wa democratic kisiasa.

Sasa basi kutokana na uchunguzi huu wa fbi ,wakajitokeza waandishi wawili wa habari kwenye gazeti la Washington Post bwana Carl Bernstein na Bob Woodward wakaingia mzigoni kufanya investigation kutaka kuchimba zaidi hili swala. Na kweli ripoti ikatoka na kuchapishwa kwenye magazeti.

Ripoti hizi zilibainisha kinagaubaga kulikuwa na michezo michafu ya kisiasa ikiendelea dhidi ya wagombea wa democratic . Lakini yote kwa yote Richard nixon akazikana shutuma zote zilizotolewa kwenye magazeti dhidi yake pamoja na wandani wake wa kisiasa wa republican.

Hili likapita ,uchaguzi mkuu ukafanyika na chama cha republican kikapata ushindi wa kishindo , wenyewe wanasema landslide victory. Ikawa tabasamu kwa Nixon, tabasamu kwa wana republican. Uncle Nixon akaamini hili swala limepita na kusahaulika na life goes on. Oh maskini Uncle Richie alikuwa anajifariji tu kwenye nafsi yake . 🤭🤭🤭🤭🤣🤣.
....
Sasa ilipofika mwezi January mwaka 1973 wale vibaka walifikishwa kwenye mahakama ya kisutu ya huko marekani😄😄😄 na kusomewa mashtaka yanayowakabili. Na kweli walipatikana na hatia na ikatoka ruling au hukumu waende segerea kutumikia vifungo vyao.

Ilipofika mwezi January mwaka 1973 , hawa vibaka wakiwa wanaendelea kutumikia vifungo vyao, mmoja wa mawakili wa upande wa utetezi alitoa hoja mahakamani akidai kwamba ikulu ya white house ya Marekani inajaribu kufunika kwa kila namna katika kutokuhusika kwake katika tukio la udukuzi kwenye jengo la watergate makao makuu ya democratic. Na vile vile wakili huyu alidai mashahidi waliotoa ushahidi wao mbele ya mahakama, walitoa ushahidi wa uongo.

Na katika tuhuma hizi mpya za huyu wakili wa upande wa utetezi hakumtaja nixon katika kuhusika kwake kwa huu mchezo mchafu wa kisiasa ila maafisa wa ngazi za juu ikiwemo wa white house walitajwa kuhusika. Kama kawaida ya uncle Nixon akaendelea kukana kwamba hakuna kitu kama hicho kuhusu udukuzi kwenye jengo la wapinzani wao wa kisiasa democratic 🤣🤣🤣.

Nixon akaona mbona kama anaandamwa hivi 🤭🤭. Unajua alifanyaje? Ili kuzuga na kuhadaa umma wa wamarekani ambao walikuwa wakilifuatilia hili suala kwa makini, alichukua uamuzi wa kumteua mwanasheria Archibald cox kama msimamizi mkuu wa kusimamia kamati iliyokuwa inachunguza hili swala la watergate building scandal, kiuhalisia huyu Archibald alikuwa ni kama chawa tu wa nixon na asingefanya lolote zaidi ya kuzuga😄😄.

# Sasa bunge la seneti la marekani likaona mbona kama nixon anataka kuwapanda kichwani hivi. Wakaamua kuunda kamati yao wenyewe ya kuchunguza swala hili la watergate kivyao.

Kamati hii ya seneti ilikuwa ikiongozwa na seneta wa north Carolina sam irvin. Hii kamati ilianza kukusanya ushahidi na ushahidi ukapelekwa mbele ya wajumbe wa kamati ya seneti ili kusikilizwa kati ya mwezi mei na novemba mwaka 1973.

Vikao vya kamati hii vilikuwa vikipeperushwa mubashara kwenye runinga huku wamarekani wakifuatilia kwa karibu kabisa. Na kweli ushahidi wa kamati hii ya seneti ikabainisha pasipo shaka kwamba maafisa wa ngazi za juu wa white house walihusika katika kuwatuma vibaka kwenda kudukua majengo ya watergate. 😱😱😱

Ahaa mdogo mdogo siri zikaanza kutoka . Kumbe white house inahusika?ALAA!. Nixon akaanza kupata pigo moja baada ya lingine. Washauri wake wakuu ndani ya white house wakaanza kujiuzulu mmoja baada ya mwingine. Na mmoja wa hawa washauri wa rais akaamua kumwaga mboga na ugali vyote kwa pamoja 😁😁😁.

Alipohojiwa huyu mmoja wa washauri wa rais mbele ya kamati ya seneti ,alitoboa siri akisema kwamba yeye pamoja na nixon waliwahi jadili hilo swala la kuwadukua democratic kwenye ofisi zao ndani ya jengo la watergate... eheerr nixon akaendelea akakaza fuvu kukana hizi shutuma ( deny deny deny).😄😄😄 kenge hasikii mpaka atokwe damu za masikioni.

Sasa katika mwendelezo wa vikao hivi vya seneti na harakati zote za kufuatilia hili swala ikabainika kwamba , kumbe uncle nixon tangu 1971 alikuwa akirekodi mazungumzo yote yaliyokuwa yakifanyika ndani ya ikulu ya white house kati yake na maafisa wa ngazi za juu wa ikulu kwa siri.🤔

Sasa kamati ya seneti na ile ya Archibald cox ikatoa shinikizo kwa nixon atoe mikanda ya tape recorder yote ya mazungumzo aliyokuwa akiirekodi kutaka kujua nini yaliyomo kwenye mazungumzo hayo. Kama kawaida uncle Richie akaendelea kukaza fuvu akadinda kuitoa 😜😜😜 .

Nixon akaona mbona kama mambo yanataka kuwa mengi hivi🤣🤣🤣. Kasheshe linazidi hivi... sasa akaamua kutaka kuzorotesha juhudi za hizi kamati mbili zinazomchimbachimba mambo yake. Guess what unajua alichukua uamuzi upi?

Alimtaka mwanasheria mkuu (attorney General)wa wakati huo kumfuta kazi Archibald aliyekuwa anasimamia kamati ya uchunguzi dhidi yake kuhusiana na watergate skendo. Na kweli attorney General akafuata maamuzi ya boss papaa nixon ya kumfuta kazi cox, ila na yeye aliamua kujiuzulu nafasi yake kama attorney General.

Nixon hapa bado hakupata escape route ya kujitoa kwenye hiki kitanzi cha kashfa ya watergate. Akateuliwa mwanasheria mwingine kuchukua nafasi aliyejulikana kama Leon jaworski . Nae akakataa kuwa chawa akaendelea kushinikiza nixon atii uamuzi wa vikao vya seneti kutoa hiyo mikanda ya tape recorder na aiwasilishe mbele ya kamati.

Dah!😂😂 kinyongeee Nixon akaona mambo yasiwe mengi akatoa baadhi ya hizo mikanda ya tape recorder. Asa bwana 🤣🤣 moja ya mkanda alioutoa bwana Nixon mbele ya kamati hizi mbili za kiuchunguzi ulipowekwa kwenye record player kukawa na gape la kama dakika 18 na nusu hivi hamna mazungumzo yanayosikika. Kuona hivi kamati ya seneti ikaona mbona kama nixon analeta mazoea sana . 😄 mazoea yanataka kuvuka mipaka aloo.

Ilipofika mwezi April 1974 nixon akatoa tena transcript ya mikanda yote ya cassette kwenye kamati za seneti na ile ya kimahakama ambazo zilikuwa na kurasa 1200 lakini nyingi zilikuwa zimeeditiwa pakubwa sana.

Sasa bwana Leon jaworski msimamizi wa kamati hii ya kuchunguza swala hili akaamua kukata rufaa kwenye mahakama kùu ya marekani. Na kweli mahakama ikatoa order kwamba ikulu ya white house itoe tape recorder zote zoteee za mazungumzo yaliyokuwa yakifanyika ndani ya ikulu tangu 1971.

Baada ya tape zote kusikilizwa na kufanyiwa uchunguzi wa kina, ikabainika kwamba nixon alikuwa akijaribu kuingilia uchunguzi uliokuwa ukiendelea dhidi yake ili kuficha ukweli dhidi ya kuhusika kwake kwenye tukio la udukuzi kwenye jengo la watergate ,kitendo ambacho ni kinyume na katiba ya marekani. Hapa ikawa ndio pigo la mwisho kwa uncle nickson.

Sasa ilipofika julai 27, 1973 kamati maalum kwenye bunge la Congress ilikutana na kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais Richard nixon. 😬😬😬🥸🥸🥺 kwa kukiuka sheria na katiba ya marekani. Na mbaya zaidi kura za maoni ( opinion polls) za takribani 66% ya wamarekani wote waliunga mkono maamuzi ya Congress kutaka kumu_ impeach Richard nixon na aondolewe kwenye nafasi yake kama rais wa marekani.

Sasa hapa uncle nickson akaona moja haikai ,mbili haikai na ameshanyea kambi, aliamua kuchukua maamuzi magumu. Akaona kulìko afanyiwe impeachment, akaamua kuandika barua ya kujiuzulu mwenyewe kama rais wa 37 wa taifa la marekani tarehe nane August mwaka 1974.
......
Kwakuwa nixon alichukua uamuzi wa kujiuzulu mwenyewe, ingetarajiwa angefunguliwa mashtaka na mwendesha mashtaka wa serikali Leon jaworski. Lakini haikuwa hivyo kaimu wake aliyefuata bwana Gerald ford alimkingia kifua na kumsamehee uncle nickson. Lakini wengi wa machawa wake waliomsapoti kipindi chote waliishia segerea kunyea debe kuhusiana na hii kashfa ya watergate.

Baada ya hii kashikashi yote hii ya kisiasa kipindi hicho, bunge la Congress liliamua kukaa chini na kupitisha sheria kadhaa ili kuzuia michezo michafu kama hii ya kisiasa kujirudia tena.

Kwa mfano bunge la Congress lilipitisha sheria iliyojulikana kama (privacy act of 1974). Sheria ya faragha ilyokuwa inawapa raia wa marekani mamlaka ya kuiamuru serikali itoe mafaili yoyote ya kiserikali na kuyachunguza na kuyafanyia upekuzi ikiwa wanayatilia mashaka.

Pili Congress walipitisha sheria iliyojulikana kama The budget act of 1974.sheria hii ilitungwa mahsusi ikiwa na vipengele vinavyomtaka rais kuwajibika na fedha zote zinazotumika kwenye ofisi yake. Na vilevile matumizi ya fedha chini ya ofisi ya rais yakaguliwe na kuwasilishwa bungeni.

Sheria hii ilitungwa mahsusi maana ilisemekana Richard nixon baadhi ya fedha za ofisi ya rais zaidi ya mamilioni ya dola alikuwa anazitumia kwa matumizi binafsi na pia ukwepaji kodi wa kiasi cha dola laki 4.

Na mwisho Congress walipitisha sheria ya Election campaign act of 1974. Ambapo sheria hii ilikuwa inaweka ukomo wa fedha ambazo zingestahili kutumika wakati wa kampeni za urais kwenye vyama vya siasa. Na sheria hii ilikuwa na kipengele kilichokuwa kinakataza vyama vya siasa na wagombea kupokea michango ya fedha za kampeni kutoka nje ya marekani.


Yote kwa yote siasa chafu za nickson zikafunika mazuri yake yote aliyofanya kipindi cha utawala wake.. pole sana in advance Richard nixon. Am done and out .Over kama umenisoma🤛
 
20250218_123852.jpg
 
Katika ubora wako. Mleta mada, milikumiss sana kwenye issues kama hizi

Mimi nafarijika propaganda za kisiasa si huku kwetu tu hadi huko waliko endelea .

Uzuri wenzetu kila tukio ni funzo kwa kwao tofauti na sisi ambao inakuwa kawaida hata kama si kawaida .
 
Katika ubora wSko. Mleta mada, milikumiss sana kwenye issues kama hizi

Mimi nafarika propaganda za kisiasa si huku kwetu tu hadi huko waliko endelea .

Uzuri wenzetu kila tukio ni funzo kwa kwao tofauti na sisi ambao inakuwa kawaida hata kama si kawaida .
Karibu mdau.. nilisahau kuku tag ,,ila natambua uwepo wake...
 
Katika ubora wako. Mleta mada, milikumiss sana kwenye issues kama hizi

Mimi nafarijika propaganda za kisiasa si huku kwetu tu hadi huko waliko endelea .

Uzuri wenzetu kila tukio ni funzo kwa kwao tofauti na sisi ambao inakuwa kawaida hata kama si kawaida .
Wapuuzi hawa nao wana mambo mengi ya hovyo sana.

Ford alitoa presidential pardon kumkinga Nixon asichukuliwe hatua za kisheria. Miaka 50 baadaye Biden naye katoa msamaha kama huo kwa mwanae Hunter, kabla hajaondoka White house kumkingia kifua mwanae asiwajibishwe kisheria kwa makosa kibao.

Halafu wanatuhubiria utawala wa kisheria.
 
Wapuuzi hawa nao wana mambo mengi ya hovyo sana.

Ford alitoa presidential pardon kumkinga Nixon asichukuliwe hatua za kisheria. Miaka 50 baadaye Biden naye katoa msamaha kama huo kwa mwanae Hunter, kabla hajaondoka White house kumkingia kifua mwanae asiwajibishwe kisheria kwa makosa kibao.

Halafu wanatuhubiria utawala wa kisheria.
That's the game of power is played. Ford alimkinga pengine labda kutokana na mazuri yake ya nyuma aliyoyafanya katika utawala wake ... no one knows
 
That's the game of power is played. Ford alimkinga pengine labda kutokana na mazuri yake ya nyuma aliyoyafanya katika utawala wake ... no one knows
Biden kamwekea kinga mtoto wake kwa mazuri gani aliyolifanyia taifa? Huoni kama hapo kuna mkinzano na utawala wa sheria, na mgongano wa kimaslahi!
 
Biden kamwekea kinga mtoto wake kwa mazuri gani aliyolifanyia taifa? Huoni kama hapo kuna mkinzano na utawala wa sheria, na mgongano wa kimaslahi!
🤣🤣🤣 power is everything in your hand .. you can do anything. Just anything.
 
Yote kwa yote siasa chafu za nickson zikafunika mazuri yake yote aliyofanya kipindi cha utawala wake.. pole sana in advance Richard nixon. Am done and out .Over kama umenisoma🤛
Kwa hapo nilipo-bold, unaamaanisha nini mkuu?

By the way, umenikumbusha uzi ufuatao wa Tumia akili

 
Back
Top Bottom