Hii ni njia nyingine ya kutafuna pesa za walala hoi, bila shaka mleta mada ni mnufaika wa hili swala ndo maana umekimbilia kuleta huu uzi humu ili mpate watu wengi wa kuwapiga. Kila siku tunaambiwa kuwa mwenyekiti ni tajiri wa kutupa lkn utajiri wake hatuuoni.
Makao makuu hovyo, ofisi ndogo hovyo na bado ruzuku au michango ikipatikana inaliwa na mwenyekiti akishirikiana na genge lake ambalo wengine wapo humu. Kuna jamaa alitoa pesa za kujenga Makao Makuu ya chama pamoja na kuchimba visima mbali mbali, hela hiyo ikayayukia ktk mikono ya wajanja wachache ambao leo hii ndio wanaoshikilia remote ya chama.