Kasi ya ukuaji uchumi wa Tanzania kufunika nchi zote Mashariki mwa Afrika

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2019
Posts
319
Reaction score
755
Uchumi wa Tanzania unategemea kukua kwa asilimia 5.2 mwaka huu wakati ambapo nchi nyingine sita za Mashariki mwa Bara la Afrika zikitarajia kuporomoka kiuchumi kwa sababu ya athari za janga la corona.

Kiwango hicho cha ukuaji wa uchumi wa Tanzania ni zaidi ya nchi zote za Mashariki mwa Bara la Afrika, kwa mujibu wa Ripoti ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).
Hata hivyo, kabla ya kutokea kwa mlipuko wa virusi vya corona, AfDB ilitarajia kiwango cha uchumi wa Tanzania kukua kwa asilimia 6.4.
Nchi sita za Mashariki mwa Bara la Afrika ambazo kiwango chao cha uchumi kimeporomoka zaidi ni Seychelles (-10.5), Sudan (-7.2), Burundi (-5.2), Somalia (-3.3), Comoro (-1.2) na Sudani Kusini (-0.4).

Nchi nyingine sita ambazo uchumi wake utakuwa lakini ziko chini ya kiwango cha wastani wa ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa mwaka huu ni Rwanda (4.2), Ethiopia (3.1), Uganda (2.5), Kenya (1.4), Djibouti (1) na Eritrea (0.3).

AfDB imeeleza kuwa pato la ndani la Tanzania (GDP) litawezeshwa zaidi na ongezeko la bei ya dhahabu iuzwayo nje ya nchi.
Ripoti ya mwezi Mei inaonesha kuwa dhahabu imeongoza kwa kuingiza fedha nyingi zaidi za kigeni Tanzania, ikizidi sekta ya utalii ambayo ilikuwa ikiongoza kabla ya mlipuko wa corona.

1594384611424.png
 
Hivi mnaposema uchumi unakua mna angalia nini??? Hawa graduates waliograduate tangu 2015 na hawana ajira ndo uchumi kujua???

Hii sekta ya biashara ya mazao ya kilimo iliyokufa kutokana na Sera mbovu za Serikali ya awamu ya tano ndo uchumi kukua ??

Haya makampuni na mashirika yanayofunga biashara na ofisi kwa kasi sana kupelekea watu kupoteza ajira ndo uchumi kukua???

Hivi kariakoo ya mwaka huu unaweza kuifananisha na kariakoo ya Mwaka 2013-2014???

Hawa wawekezaji wanaokimbia kila siku ndo uchumi kukua????
 
Hivi mnaposema uchumi unakua mna angalia nini??? Hawa graduates waliograduate tangu 2015 na hawana ajira ndo uchumi kujua???

Hii sekta ya biashara ya mazao ya kilimo iliyokufa kutokana na Sera mbovu za Serikali ya awamu ya tano ndo uchumi kulia???

Wengi huwa ni kula kulala pale mashemeji zao wanapobadili magari kwao ni kipimo cha kukua uchumi
 
Hivi mnaposema uchumi unakua mna angalia nini??? Hawa graduates waliograduate tangu 2015 na hawana ajira ndo uchumi kujua???

Hii sekta ya biashara ya mazao ya kilimo iliyokufa kutokana na Sera mbovu za Serikali ya awamu ya tano ndo uchumi kulia???

Haya makampuni na mashirika yanayofunga biashara na ofisi kwa kasi sana kupelekea watu kupoteza ajira ndo uchumi kukua???

Hivi kariakoo ya mwaka huu unaweza kuifananisha na kariakoo ya Mwaka 2013-2014???

Hawa wawekezaji wanaokimbia kila siku ndo uchumi kukua????
Hii ni kwa mujibu wa Ripoti ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)...
 
Embu nielezee basi ni sekta ipi yenye ukuaji mzuri kuonesha kuwa Eti tunaongoza kwa ukuaji wa uchumi???

Maana wote tunaishi Tanzania na tunaona, hali za maisha tunaziona
 
jianganyeni tu. Vijana huku wanakufa njaa nyie mnahusudu hizo international prides tu. Watanzani wameichukia sana ccm na jpm wake. Wakulima wa mbaazi na korosho wanalia nyie mnasema uchumi umekua
 
Kawaulize benki ya Maendeleo ya Africa
Na kama limekuuma kale Tango na Asali
Kama wanasoma humu basi wasems??? Huku kulishana matango pori kumezidi sasa. Sio kwamba nchi ikiwa inakopa sana kwao ndo wanaleta takwimu hizi ili tu kula na kipofu vizuri
 
Hongera kwa Tanzania.mwanzo mgumu lakini mwisho wa siku tutafika.
 
Kuporomoka kwa uchumi majirani, kutaathiri biashara sana. Mfano, Rwanda ndo biggest importer wa bidhaa zetu
 
Mie nikiangalia Posta tu kwa miaka hii mitano naiona kama imekufa, kulikuwa na biashara za restaurant kubwa pale posta kama Spur na maduka mengi ya biashara. Saivi yote hayapo na yamekufa. Watu wamepoteza ajira. Ukienda quality Centre pale pugu road ndo usiseme maduka karibu yote yamekufa na watu hawafanyi biashara. Mkuki house hakuna cha maduka wala supermarkets zote zimekufa yamebaki maduka machache sana.

Nenda Masaki ya Oysterbay, Real estate market was booming, wazungu, waarabu na wahindi walikuwa wanagombania apartments kurent saivi majengo mengi yako wazi na hayana hata wapangaji

Pita New Bagamoyo Road jaribu kutembelea majengo mapya yanayouzwa, mengi yana a lot of spaces kwa sababu hakuna biashara na hakuna wapangishaji. Kampuni nyingi zimefunga na hazifanyi kazi.

Sasa huo uchumi unaokuwa upo wapi???
 
Tumerudi kwenye uchumi halisi sasa,lazima kufanya kazi na kodi ilipwe.Nadhani wachumi watatusaidia why tuko hv sasa tofauti na 2015 kurudi nyuma
 
Kwa iyo uchumi halisi ndo watu kupoteza ajira na biashara kufungwa?
 
Ndio maana nikasema wachumi watatusaidia kwenye hilo,hata mimi nimuanga wa kutokuwa na ajira baada ya mkataba kutoongezwa.Na sababu nikushuka kwa biashara na hilo ni kawaida.
 
Uchumi wa Tanzania unategemea kukua kwa asilimia 5.2 mwaka huu wakati ambapo nchi nyingine sita za Mashariki mwa Bara la Afrika zikitarajia kuporomoka kiuchumi kwa sababu ya athari za janga la corona.

Kiwango hicho cha ukuaji wa uchumi wa Tanzania ni zaidi ya nchi zote za Mashariki mwa Bara la Afrika, kwa mujibu wa Ripoti ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).
Hata hivyo, kabla ya kutokea kwa mlipuko wa virusi vya corona, AfDB ilitarajia kiwango cha uchumi wa Tanzania kukua kwa asilimia 6.4.
Nchi sita za Mashariki mwa Bara la Afrika ambazo kiwango chao cha uchumi kimeporomoka zaidi ni Seychelles (-10.5), Sudan (-7.2), Burundi (-5.2), Somalia (-3.3), Comoro (-1.2) na Sudani Kusini (-0.4).

Nchi nyingine sita ambazo uchumi wake utakuwa lakini ziko chini ya kiwango cha wastani wa ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa mwaka huu ni Rwanda (4.2), Ethiopia (3.1), Uganda (2.5), Kenya (1.4), Djibouti (1) na Eritrea (0.3).

AfDB imeeleza kuwa pato la ndani la Tanzania (GDP) litawezeshwa zaidi na ongezeko la bei ya dhahabu iuzwayo nje ya nchi.
Ripoti ya mwezi Mei inaonesha kuwa dhahabu imeongoza kwa kuingiza fedha nyingi zaidi za kigeni Tanzania, ikizidi sekta ya utalii ambayo ilikuwa ikiongoza kabla ya mlipuko wa corona.

View attachment 1502864
Usipaze sauti wakisikia watachukia. Khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Pesa nyingi imepelekwa kwenye mega project na mega project ni kodi ya wananchi.
Shida ya megaproject inakomba hela nyingi kwenda nje ya nchi.
Lakini kama kweli tuna change inabaki mbona mishahara haipandi mwaka wa tano?
 
Mie nikiangalia Posta tu kwa miaka hii mitano naiona kama imekufa, kulikuwa na biashara za restaurant kubwa pale posta kama Spur na maduka mengi ya biashara. Saivi yote hayapo na yamekufa. Watu wamepoteza ajira. Ukienda quality Centre pale pugu road ndo usiseme maduka karibu yote yamekufa na watu hawafanyi biashara. Mkuki house hakuna cha maduka wala supermarkets zote zimekufa yamebaki maduka machache sana.

Nenda Masaki ya Oysterbay, Real estate market was booming, wazungu, waarabu na wahindi walikuwa wanagombania apartments kurent saivi majengo mengi yako wazi na hayana hata wapangaji

Pita New Bagamoyo Road jaribu kutembelea majengo mapya yanayouzwa, mengi yana a lot of spaces kwa sababu hakuna biashara na hakuna wapangishaji. Kampuni nyingi zimefunga na hazifanyi kazi.

Sasa huo uchumi unaokuwa upo wapi???

Makao makuu yamehamia Dodoma. Bandari Salama itadorora kidogo hiyo ni kawaida huo ni mtikisiko wa makao makuu.
 
Ilani ya CCM 2020-2030 imeweka kilimo kipaumbela sana,tutegemee mageuzi makubwa kwenye kilimo

Kilimo hiki hiki ambacho wizara yake bajeti ni ndogo sana na wanapewa only 30% ya bajeti hio?
 
Back
Top Bottom