Kasi ya ukuaji uchumi wa Tanzania kufunika nchi zote Mashariki mwa Afrika

Kasi ya ukuaji uchumi wa Tanzania kufunika nchi zote Mashariki mwa Afrika

Makao makuu yamehamia Dodoma. Bandari Salama itadorora kidogo hiyo ni kawaida huo ni mtikisiko wa makao makuu.
Dodoma ni miradi ya serikali tu. Zinazoanguka Dar sio miradi ya serikali Bali ni miradi ya wananchi. Sasa huo uchumi unakuwa wapi?
 
Hivi mnaposema uchumi unakua mna angalia nini??? Hawa graduates waliograduate tangu 2015 na hawana ajira ndo uchumi kujua???

Hii sekta ya biashara ya mazao ya kilimo iliyokufa kutokana na Sera mbovu za Serikali ya awamu ya tano ndo uchumi kukua ??

Haya makampuni na mashirika yanayofunga biashara na ofisi kwa kasi sana kupelekea watu kupoteza ajira ndo uchumi kukua???

Hivi kariakoo ya mwaka huu unaweza kuifananisha na kariakoo ya Mwaka 2013-2014???

Hawa wawekezaji wanaokimbia kila siku ndo uchumi kukua????
Mkuu naomba urudi darasani usomee uchumi. Ukuaji wa uchumi tunaangalia Gross domestic product (GDP), Gross domestic product per capita na Gross Domestic Product PPP (Purchasing power parity)

Hapo kwenye GDP tunachukua bidha zote zinazozalishwa katika mwaka husika tunazibadirisha kuwa cash, money. hiyo thamani tunayo ipata hapo ndio inatumika ku predict ukuaji wa uchumi. Tunafanyaje tunalinganisha na miaka ya nyuma then tuna pata rate ya ukuaji wa uchumi. Nadhani unajua hesabu za kujumlisha na kutoa then kugawanya mara 100.

Rate ikiwa ni kubwa maana yake ni ni ni? maana yake ni kwamba
1. Uzalishaji umeongezeka mwaka huo
Kwanini umeongezeka labda viwanda vimeongezeka, au kuna sekta fulani inakua kwa kasi
2. Usafirishaji na uuzaji wa bidha nje ya nchi umeongezeka (Export)
3. Labda thamani ya pesa imepanda ukilinganisha na dolla
4. Au thamani ya madini imepanda. That's means yakiuzwa nje ya nchi basi yanatuletea fedha nyingi za kigeni ambazo tukitafutia GDP lazima iwe kubwa.

GDP per capita hapo tutagawanya na idadi ya watu.

Basi kama ni hivyo, kama kipindi cha korona tungelala ndani uzalishaji wa hizo bidhaa nani angefanya, kwa hiyo kungekua hakuna export pia. Hizo data za kutafutia GDP. tungezipata wapi. Kwa hiyo kama zinarekodiwa its means zingekua chache zikiwa na thamani ndogo sana, automatically ukitafuta rate baada ya kutoa na miaka ya nyuma jibu lingekuka hasi, less production
 
Uchumi wa Tanzania unategemea kukua kwa asilimia 5.2 mwaka huu wakati ambapo nchi nyingine sita za Mashariki mwa Bara la Afrika zikitarajia kuporomoka kiuchumi kwa sababu ya athari za janga la corona.

Kiwango hicho cha ukuaji wa uchumi wa Tanzania ni zaidi ya nchi zote za Mashariki mwa Bara la Afrika, kwa mujibu wa Ripoti ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).
Hata hivyo, kabla ya kutokea kwa mlipuko wa virusi vya corona, AfDB ilitarajia kiwango cha uchumi wa Tanzania kukua kwa asilimia 6.4.
Nchi sita za Mashariki mwa Bara la Afrika ambazo kiwango chao cha uchumi kimeporomoka zaidi ni Seychelles (-10.5), Sudan (-7.2), Burundi (-5.2), Somalia (-3.3), Comoro (-1.2) na Sudani Kusini (-0.4).

Nchi nyingine sita ambazo uchumi wake utakuwa lakini ziko chini ya kiwango cha wastani wa ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa mwaka huu ni Rwanda (4.2), Ethiopia (3.1), Uganda (2.5), Kenya (1.4), Djibouti (1) na Eritrea (0.3).

AfDB imeeleza kuwa pato la ndani la Tanzania (GDP) litawezeshwa zaidi na ongezeko la bei ya dhahabu iuzwayo nje ya nchi.
Ripoti ya mwezi Mei inaonesha kuwa dhahabu imeongoza kwa kuingiza fedha nyingi zaidi za kigeni Tanzania, ikizidi sekta ya utalii ambayo ilikuwa ikiongoza kabla ya mlipuko wa corona.


View attachment 1502864
hapa wakenya itawauma sana, waanze na wao angalau kulima dhaabu maana shamba la Tanzanite kwa sasa limerudi mikononi mwa TANZANIA
 
Mkuu naomba urudi darasani usomee uchumi. Ukuaji wa uchumi tunaangalia Gross domestic product (GDP), Gross domestic product per capita na Gross Domestic Product PPP (Purchasing power parity)

Hapo kwenye GDP tunachukua bidha zote zinazozalishwa katika mwaka husika tunazibadirisha kuwa cash, money. hiyo thamani tunayo ipata hapo ndio inatumika ku predict ukuaji wa uchumi. Tunafanyaje tunalinganisha na miaka ya nyuma then tuna pata rate ya ukuaji wa uchumi. Nadhani unajua hesabu za kujumlisha na kutoa then kugawanya mara 100.

Rate ikiwa ni kubwa maana yake ni ni ni? maana yake ni kwamba
1. Uzalishaji umeongezeka mwaka huo
Kwanini umeongezeka labda viwanda vimeongezeka, au kuna sekta fulani inakua kwa kasi
2. Usafirishaji na uuzaji wa bidha nje ya nchi umeongezeka (Export)
3. Labda thamani ya pesa imepanda ukilinganisha na dolla
4. Au thamani ya madini imepanda. That's means yakiuzwa nje ya nchi basi yanatuletea fedha nyingi za kigeni ambazo tukitafutia GDP lazima iwe kubwa.

GDP per capita hapo tutagawanya na idadi ya watu.

Basi kama ni hivyo, kama kipindi cha korona tungelala ndani uzalishaji wa hizo bidhaa nani angefanya, kwa hiyo kungekua hakuna export pia. Hizo data za kutafutia GDP. tungezipata wapi. Kwa hiyo kama zinarekodiwa its means zingekua chache zikiwa na thamani ndogo sana, automatically ukitafuta rate baada ya kutoa na miaka ya nyuma jibu lingekuka hasi, less production
Asante kwa ufafanuzi mzuri,ndio uzuri wa jamii forums kuna watu wa kila aina humu jukwaani.
Kilimo hiki hiki ambacho wizara yake bajeti ni ndogo sana na wanapewa only 30% ya bajeti hio?
Ni kweli wamesema jana nilimsikia bashiru akilizungumzia ngoja tuone lakini.Tukijipanga kwenye kilimo vizuri hii nchi itapaa sana kiuchumi.
Maana miundumbio ya kuungunganisha mikoa na mikoa karibu barabara nyingi zinzmaliziwa Kuanzia KIgoma,Tabora,Mpanda mpaka Sumbawanga
Ukija kwenye reli njia ya zamani toka Dar mpaka Isaka ipo mwishoni kwenye ukarabati,njia ya Mpanda to Kaliua wanatoa reli ya zamani sana wanaweka pound 60 hivyo kasi itaongezeka
Ukija ya njia ya kaskazini mpaka Arusha imefunguliwa hizo zote zitachochea usafirishaji wa mazao,hsa ile njia ya Mpanda wanaitegemea sana.
Ishu nyingine ni kwenye pembeje za kilimo ndio shida hapo zipo feki nyingi inabidi wapambane sana kulimaliza hilo tatizo.Na ishu ya masoko wasiingilie mkulima aruhusiwe kuuza popote anapotaka ndani au nje ya nchi.ILa naona msimu huu NFRA wameanza kununua mahindi na kwa bei ya soko itawainunua sana wakulima.
 
Back
Top Bottom