ToniXrated
JF-Expert Member
- Sep 21, 2022
- 1,134
- 2,993
Amani iwe nanyi
Sitoi pole kwa Yanga kwa kufungwa na Al hilal licha ya kumiliki sana mpira!! Natoa pole kwa wachezaji wa ligi nzima ya bongo kwa kushindwa kuwa na kasi kiwanjani pindi wanapokuwa na mpira ama wasipokuwa na mpira.
Nitaendelea sana kuongelea kasi/pace/speed ya wachezaji wetu katika hizi klabu kubwa hapa nchini kuwa hairidhishi na wala haiendani na mpira wa kisasa unaochezwa duniani.
Naona makocha wetu wanatumia muda mwingi kufundisha kitandaza mpira kwa maana ya kupiga pasi fupi fupi huku timu ikianza mashambulizi kutoka nyuma. Ni jambo jema ila amini kwamba mpira wa pasi bila ya kuwa na kasi inakuwa sawa na kupoteza muda.
Yanga jana nilikuwa nawashangaa jinsi wanavyosukuma mpira taratibu kana kwamba wao ndio walikuwa wanaongoza katika matokeo. Al hilal sio kwamba walikuwa wakicheza vizuri kuliko yanga, walikuwa wakicheza tu kimkakati na kasi ya wachezaji wao iliwanufaisha sana na kuwawezesha kuondoka na ushindi. Nilikuwa nashangaa sana jinsi mchezaji wa al hilal alivyokuwa akiwazidi mbio wachezaji wa Yanga na kufanikiwa kwenda kuonana na Diara uso kwa uso. Al Hilal silaha yao kubwa ilikuwa ni mbio huku wakijua kuwa wachezaji wengi wa yanga hawakimbii uwanjani ila wana jog tu .Wachezaji angalau wanampira wa kasi ni Tuisila Kisinda,Ambundo ,Shabani Juma na farid Musa. Waliobaki ni mwendo wa kobe.
Kama timu zetu zimeamua kucheza mpira wa pasi basi tuhakikishe kuwa wachezaji wanakimbia uwanjani pindi wawapo na mpira na pale wasipokuwa na mpira. Timu za waarabu hazina mafundi wengi wa soka ila wanajivunia uwezo wao wa kucheza mpira wa kasi .
Nina imani siku tutakapoweza kucheza mpira kwa kasi ndio siku ambayo tutaweza kubeba kombe la klabu bingwa Africa.