Kasimu Majaliwa: Polisi Mtafuteni Mmiliki wa Jengo

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Mheshimiwa Waziri Mkuu wetu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mwalimu Kasimu Majaliwa ametoa maagizo kwa jeshi la Polisi kumtafuta mmiliki wa jengo ambalo limeanguka na kusababisha vifo vya karibu watu 15 mpaka hivi sana na majeruji kadhaa .

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo wakati wa shughuli ya kuaga miili ya wale waliopoteza Maisha katika tukio hilo la kuporomoka kwa jengo eneo la kariakoo.

Ila mimi Mwashambwa naona kumpata mmiliki ni rahisi tu pasipo hata kumtafuta zaidi ya kumpigia simu.Maana naamini mmiliki ni mlipa kodi na anayetambulika na TRA .ambako huko TRA kuna taarifa zake zote. Lakini nilikuwa nafikiria kuwa pengine mpaka muda huu au siku ya Leo ilitakiwa mmiliki awe ameshapatikana na kufahamika na kushikiliwa na hatua za awali zikawa zinaendelea hususani zile za mahojiano.

Japo mwingine unaweza kusema kuwa Mwashambwa huna akili utaanzaje kumhoji mtu badala ya kujielekeza katika uokoaji. Jibu ni kuwa serikali ni kubwa sana na yenye watu mbalimbali katika vitengo mbalimbali na wenye majukumu tofautitofauti ambapo siyo wote waliokatika eneo la uokoaji japo macho ,masikio yao yapo hapo hapo pia katika kufuatilia kila kinachoendelea.kwa hiyo zoezi la uokoaji linaweza kuendelea huku mahojiano pia yakiendelea kwa ajili ya kukusanya taarifa muhimu za awali.

Ndio Maana Rais wa Nchi hayupo Nchini lakini serikali nzima ipo eneo la tukio ikitekeleza kwa ufasaha na ufanisi maelekezo yake yote kikamilifu.na ndio maana Hata katika hotuba yake fupi Mheshimiwa Rais alitoa taarifa ya hadi idadi ya vifo na majeruhi na maelekezo aliyoyatoa kwa watendaji wa serikali yake na vyombo vya dola kama vile kwa jeshi la polisi na ofisi ya waziri Mkuu na taasisi zingine.

Mwisho niseme tu ya kuwa huu ni wakati wa kuungana kama watanzania kusaidiana katika kuwafikia wale walionasa chini ya jengo na ambao bado kuwafikia.kuwaombea ili Mungu aendelee kuwaweka hai.siyo wakati wa kulaumiana au kunyoosheana vidole vya lawama au kushutumiana. Ni muda wa kupigania kuokoa Maisha ya wale ambao wapo bado hai chini ya jengo walikonasa.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Lucas Mwashambwa unajua vi kirukuu vilikuwa vinabeba majeruhi kabla ya Ma V8 na ma Toyota Land cruiser washwasha na upuuzi mwingine haujafika?
 
1. Wanaokoa siku ya tatu what shame.

2. Hawana ramani ya jengo.

3. Kwanini hadi leo mmliki hajajitokeza na hawajampata?

4. Vipi wanaotoa vibali vya ujenzi je wamekamatwa?

5. Muhandisi wa huo ukarabati yuko wapi?

6. Selikali ilikuwa wapi?

Majengo zaidi ya 20 kariakoo hayafai, report ya lowasa.

CCM inalitafuna taifa
 
Mmiliki wa jengo watamuonea tu.Hana kosa kabisa.mwenye kosa ni serikali ambayo inaruhusu ujenzi usiozingatia ubora wa majengo.mmiliki wa jengo anavibali vyote vya ujezi Sasa mnataka akamatwe Kwa kosa Gani?Njia nzuri ya kuwajibika ni kujiuzulu Kwa waziri mkuu na bosi wake Kwa kuwa wameshindwa kusimamia ubora wa majengo zaidi ya kupaa tu angani kwenda kuombaomba pesa ambazo zinakuja kuishia mifukoni mwa mafisadi
 
Back
Top Bottom