Kasimu Majaliwa: Polisi Mtafuteni Mmiliki wa Jengo

Kwani wewe mtu akikwambia chizi huwa unashangaa? Kwani wewe unajiona upo sawa. Wewe ni sawa na SAGAI GALGANO au Benjamini Netanyau ambao hawajitambui
Dogo uwe na adabu Mimi ndio huwa natoa posho ya kuwalipa Machawa wa humu JF ukiwemo na wewe
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mheshimiwa Waziri Mkuu wetu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mwalimu Kasimu Majaliwa ametoa maagizo kwa jeshi la Polisi kumtafuta mmiliki wa jengo ambalo limeanguka na kusababisha vifo vya karibu watu 15 mpaka hivi sana na majeruji kadhaa .

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo wakati wa shughuli ya kuaga miili ya wale waliopoteza Maisha katika tukio hilo la kuporomoka kwa jengo eneo la kariakoo.

Ila mimi Mwashambwa naona kumpata mmiliki ni rahisi tu pasipo hata kumtafuta zaidi ya kumpigia simu.Maana naamini mmiliki ni mlipa kodi na anayetambulika na TRA .ambako huko TRA kuna taarifa zake zote. Lakini nilikuwa nafikiria kuwa pengine mpaka muda huu au siku ya Leo ilitakiwa mmiliki awe ameshapatikana na kufahamika na kushikiliwa na hatua za awali zikawa zinaendelea hususani zile za mahojiano.

Japo mwingine unaweza kusema kuwa Mwashambwa huna akili utaanzaje kumhoji mtu badala ya kujielekeza katika uokoaji. Jibu ni kuwa serikali ni kubwa sana na yenye watu mbalimbali katika vitengo mbalimbali na wenye majukumu tofautitofauti ambapo siyo wote waliokatika eneo la uokoaji japo macho ,masikio yao yapo hapo hapo pia katika kufuatilia kila kinachoendelea.kwa hiyo zoezi la uokoaji linaweza kuendelea huku mahojiano pia yakiendelea kwa ajili ya kukusanya taarifa muhimu za awali.

Ndio Maana Rais wa Nchi hayupo Nchini lakini serikali nzima ipo eneo la tukio ikitekeleza kwa ufasaha na ufanisi maelekezo yake yote kikamilifu.na ndio maana Hata katika hotuba yake fupi Mheshimiwa Rais alitoa taarifa ya hadi idadi ya vifo na majeruhi na maelekezo aliyoyatoa kwa watendaji wa serikali yake na vyombo vya dola kama vile kwa jeshi la polisi na ofisi ya waziri Mkuu na taasisi zingine.

Mwisho niseme tu ya kuwa huu ni wakati wa kuungana kama watanzania kusaidiana katika kuwafikia wale walionasa chini ya jengo na ambao bado kuwafikia.kuwaombea ili Mungu aendelee kuwaweka hai.siyo wakati wa kulaumiana au kunyoosheana vidole vya lawama au kushutumiana. Ni muda wa kupigania kuokoa Maisha ya wale ambao wapo bado hai chini ya jengo walikonasa.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Jamani ukiangalia kwenye system ya wilaya si unapata nina la mmiliki maana kibali cha ujenzi hakiwezi kutolewa bila faili la kiwanja na hati ya umiliki kufika wilayani. Mbona unaleta siasa kwenye kila kitu. Nyie mtajeni mmiliki mwiteni mahakamani au polisi. Ila kusema mmiliki mnatafuta huu ni uwongo.
 
Huwa wanasepa hata miezi 3 kukipoa ndio anakuja kimya kimya......kumbuka huwa ma kada hawa
 
Yaaani ghorofa inaanza kujenga na serikali haijui mmiliki ni nani na yuko wapi? Kibali hakina majina yake? DUH
Hii ni danganya toto na uzembe mkubwa.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mheshimiwa Waziri Mkuu wetu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mwalimu Kasimu Majaliwa ametoa maagizo kwa jeshi la Polisi kumtafuta mmiliki wa jengo ambalo limeanguka na kusababisha vifo vya karibu watu 15 mpaka hivi sana na majeruji kadhaa .

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo wakati wa shughuli ya kuaga miili ya wale waliopoteza Maisha katika tukio hilo la kuporomoka kwa jengo eneo la kariakoo.

Ila mimi Mwashambwa naona kumpata mmiliki ni rahisi tu pasipo hata kumtafuta zaidi ya kumpigia simu.Maana naamini mmiliki ni mlipa kodi na anayetambulika na TRA .ambako huko TRA kuna taarifa zake zote. Lakini nilikuwa nafikiria kuwa pengine mpaka muda huu au siku ya Leo ilitakiwa mmiliki awe ameshapatikana na kufahamika na kushikiliwa na hatua za awali zikawa zinaendelea hususani zile za mahojiano.

Japo mwingine unaweza kusema kuwa Mwashambwa huna akili utaanzaje kumhoji mtu badala ya kujielekeza katika uokoaji. Jibu ni kuwa serikali ni kubwa sana na yenye watu mbalimbali katika vitengo mbalimbali na wenye majukumu tofautitofauti ambapo siyo wote waliokatika eneo la uokoaji japo macho ,masikio yao yapo hapo hapo pia katika kufuatilia kila kinachoendelea.kwa hiyo zoezi la uokoaji linaweza kuendelea huku mahojiano pia yakiendelea kwa ajili ya kukusanya taarifa muhimu za awali.

Ndio Maana Rais wa Nchi hayupo Nchini lakini serikali nzima ipo eneo la tukio ikitekeleza kwa ufasaha na ufanisi maelekezo yake yote kikamilifu.na ndio maana Hata katika hotuba yake fupi Mheshimiwa Rais alitoa taarifa ya hadi idadi ya vifo na majeruhi na maelekezo aliyoyatoa kwa watendaji wa serikali yake na vyombo vya dola kama vile kwa jeshi la polisi na ofisi ya waziri Mkuu na taasisi zingine.

Mwisho niseme tu ya kuwa huu ni wakati wa kuungana kama watanzania kusaidiana katika kuwafikia wale walionasa chini ya jengo na ambao bado kuwafikia.kuwaombea ili Mungu aendelee kuwaweka hai.siyo wakati wa kulaumiana au kunyoosheana vidole vya lawama au kushutumiana. Ni muda wa kupigania kuokoa Maisha ya wale ambao wapo bado hai chini ya jengo walikonasa.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Tulitegemea sasa hivi ungekuwa Kariakoo umeshaopoa hata majeruhi wawili, badala yake uko kweye keyboard unampongeza mama na kahawa pembeni!
 
Back
Top Bottom