Kasma ya Road Fund: Kwanini Magufuli siyo mkweli?

Kasma ya Road Fund: Kwanini Magufuli siyo mkweli?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
Juzi hivi Magufuli- Waziri wa Miundo mbinu- alituhadaa pale alipokuwa akifungua mkutano wa TANROADS kule Mwanza kuwa kuanzia sasa fedha za bajeti ya ROAD FUND kuwanufaisha wazawa na kwa kufanya hivyo hakuwa mkweli hata kidogo.

Wakati umefika wanasiasa waache
porojo kwa sababu na sisi tuna macho na masikio na mbongo za kutafakari kauli zao, pia.

Matatizo ya kauli ya Magufuli ni kama ifuatavyo:-

1) Msimamo wa serikali kwa makampuni ya ujenzi ya wazawa ni ujima kwa maana waungane kama vile vijiji vya ujamaa au vyama vya ushirika vilivyoshindikana na kufa kifo cha paka shume kwa matatizo ya umiliki n.k; ili pia, kampuni za ujenzi zife na serikali waweze kuwaneemesha wageni kiulaini kwa madai potofu wazawa kwisha khabari yao kumbe sera za serikali ndiyo shubiri yao!

2) Hakuna sheria hivi sasa ambazo zinailazimisha serikali kupitia TANROADS kutoa kazi za fedha za ROAD FUND kwa makampuni ya wazalendo hivyo kufanya kauli za Magufuli kuwa gumzo la kijiweni. Serikali ambayo kweli inajali soko la ajira la ndani ingelikuwa imekwisha kutunga sheria stahiki siku mingi kabisa.......................
na kutuondolea huu utapeli wa domokaya.

3) Wakati Magufuli akiropoka utapeli tajwa wakati huohuo TANROADS ilikuwa inatoa kazi lukuki kwa kampuni za kigeni kwa malipo ya ROAD FUND na hivyo kufanya kauli zake kuwa ni za kitapeli na sijui anamtapeli nani?

4) Khoja ya kuwa kampuni za kizalendo hazina mitaji ni khoja ambazo zinashindwa kukiri kuwa jukumu la serikali ni kuwajengea mazingira mazuri raia wake kuweza kutatua matatizo ya nchi yao badala ya kuwakandia. Jukumu la serikali ni kujenga mazingira ya utoaji wa mikopo isiyo na riba ya kununulia mitaji ili kazi karibu zote zifanywe na wazalendo na kuliinua soko la ajira la hapa nchini.

5) Sheria hazipo zakuhakikisha miradi yote ya ujenzi inasimamiwa na wazalendo ambao tumewasomesha kwa gharama ya kutisha na kwa kutofanya hivyo serikali inajima nafasi ya kunufaika na wataalamu hao na huku gharama za miradi mingi zinakosa ushindani na kuwa mzigo kwa taifa. Kutokana na ukosefu wa ushindani ambao serikali inahusika moja kwa moja kwenye hilo miradi mingi imekumbwa na mushkeli wa
"overinvoicing" na kufanya jitihada za serikali kujenga miundo mbinu nyingi kukwama kabisa kutokana na bei za kutisha za makandarasi wageni hapa nchini.

6) Serikali inawahusudu wageni kwa kuwa huwapelekea
"ten percent" kwenye akaunti zao uswisi na ndiyo maana pamoja na kulia na bei za makandarasi wengi ni za kutisha hawako tayari kuachia mkate wao na kubadilisha mfumo mzima wa utendaji ndani ya Wizara ya miundo mbinu ikiwa pamoja na TANROADS.

7) Magufuli alizungumzia utendaji wa TANROADS lakini alionekana ni mwoga kuleta mabadiliko yenye tija kwa sababu uozo ndani ya TANROADS ni kipato kikubwa kwake na wenzie ndani ya serikali. Haiwezekani miradi mingi tena yenye kuligharimu taifa pesa nyingi zifujwe na hakuna ambaye huwajibishwa. Haiwezekani ajira ndani ya TANROADS ziwe za milele bila kupimwa kila baada ya miaka mitano kwa mikataba mifupi fupi kama siyo kulindana.

Ruta,
Labda mie nigusie kidogo tu hilo la kuungana!!
For what i know, kampuni zetu nyingi mtaji ni magumashi! Sana sana, wengi wao wanatarajia kupewa advance ndipo waanze ujenzi!! So, assume construction ni ya abt TZS 50 Billion, na moja ya vigezo, contractor anatakiwa kuwa annual turnover ya say TZS 5 billion! Je, ni kampuni ngapi zinaweza ku-compete on their own?!

Binafsi, sioni tatizo katika kuungana hasa kwavile nafahamu kampuni nyingi kimtaji ni magumashi! Kinyume cha hili, basi kampuni nyingi zitaishia kazi za kuchimba mitaro na kujaza udongo kwenye barabara za vijiji! Tatizo ninaloona mimi ni nia na dhati ya serikali ya kutoa hizo tenda kwa local companies pale wanapokuwa tayari wamekidhi vigezo!
 
6) Serikali inawahusudu wageni kwa kuwa huwapelekea
"ten percent" kwenye akaunti zao uswisi na ndiyo maana pamoja na kulia na bei za makandarasi wengi ni za kutisha hawako tayari kuachia mkate wao na kubadilisha mfumo mzima wa utendaji ndani ya Wizara ya miundo mbinu ikiwa pamoja na TANROADS.
Hilo la 10% mkuu wangu wala hakuna aliyesalimika....wote, foreign na local, ni corrupt wakubwa!! Kuna wakati nilikuwa NMB....kuna siku nilishangaa pale cheki ya malipo ya Mkandarasi (ni local huyu) ilipofika benki kwa malipo!! Yaani yule bwana, alichukua just part of the total amount....!! Nilipowauliza bankers wenzangu wenye muda mrefu pale kulikoni, nikaambiwa nitulie wenye amount iliyobaki utawaona!! All of them walikuwa District Officials walio-initiate tender
 
Duh hali ni mbaya sana kumbe!! Coz hata hizi pesa za mabarabara za World Bank zinapitia manispaa yaani ni uchakachuaji kwa kwenda mbele...bora zingeenda moja kwa moja kwa moja kwa mkandarasi...We have long way to go
 
Shida apa kazi ambayo mzawa atapewa kwa 1b kazi iyo iyo ushangaa mtu wa nje kapewa kwa 2B
Izi 10% toka hasa kwa wachina zitakuja kutumaliza matokeo yake wanajenga barabara substandard na hakuna wa kumkoromea bse ushalamba cha juu
 
Njowepo yaani hili tumbo sijui kwanini baadhi yetu tunahangaika nalo hivyo..............tunasahau kuwa halina hata cha shukrani kabisa....
 
Yaani huko Manispaa, balaa tupu

NasDaz serikali kuu ndiyo chanzo cha haya yote. TUnapaswa kujifunza kutoka Kenya uwajibikaji umeongezeka maradufu kwa sababu magavana wanachaguliwa moja kwa moja na wapigakura hakuna cha DED kuletwa na serikali kuu. Ajira zote ni jukumu la madiwani na hakuna kuhamishwa kwenda kaunti nyingine.........bila ya kujenga upysa uwajibikaji kwenye Manispaa na Halmashauri tutajikuta kila siku tunalaumiana tu!
 
Hilo la 10% mkuu wangu wala hakuna aliyesalimika....wote, foreign na local, ni corrupt wakubwa!! Kuna wakati nilikuwa NMB....kuna siku nilishangaa pale cheki ya malipo ya Mkandarasi (ni local huyu) ilipofika benki kwa malipo!! Yaani yule bwana, alichukua just part of the total amount....!! Nilipowauliza bankers wenzangu wenye muda mrefu pale kulikoni, nikaambiwa nitulie wenye amount iliyobaki utawaona!! All of them walikuwa District Officials walio-initiate tender

NasDaz Angalau ajira imebakia nyumbani. Sasa hao takukuru wao kazi ni kuchapana risasi tu na kulipana mishara na posho bila ya kuvuja jasho?
 
Ruta,
Labda mie nigusie kidogo tu hilo la kuungana!!
For what i know, kampuni zetu nyingi mtaji ni magumashi! Sana sana, wengi wao wanatarajia kupewa advance ndipo waanze ujenzi!! So, assume construction ni ya abt TZS 50 Billion, na moja ya vigezo, contractor anatakiwa kuwa annual turnover ya say TZS 5 billion! Je, ni kampuni ngapi zinaweza ku-compete on their own?!

Binafsi, sioni tatizo katika kuungana hasa kwavile nafahamu kampuni nyingi kimtaji ni magumashi! Kinyume cha hili, basi kampuni nyingi zitaishia kazi za kuchimba mitaro na kujaza udongo kwenye barabara za vijiji! Tatizo ninaloona mimi ni nia na dhati ya serikali ya kutoa hizo tenda kwa local companies pale wanapokuwa tayari wamekidhi vigezo!
4) Khoja ya kuwa kampuni za kizalendo hazina mitaji ni khoja ambazo zinashindwa kukiri kuwa jukumu la serikali ni kuwajengea mazingira mazuri raia wake kuweza kutatua matatizo ya nchi yao badala ya kuwakandia. Jukumu la serikali ni kujenga mazingira ya utoaji wa mikopo isiyo na riba ya kununulia mitaji ili kazi karibu zote zifanywe na wazalendo na kuliinua soko la ajira la hapa nchini.

NasDaz hiyo khoja ya sita inabidi iende sambamba na hoja ya 4..........Ni jukumu la serikali kutoa mikopo kwa makandarasi wake na vitendea kazi ili kuongeza ushindani katika zabuni zake ambapo kwa kufanya hivyo gharama za ujenzi zitashuka sana na kuhakikisha kazi zinakuwa na ubora wa kuridhisha.
 
Duh hali ni mbaya sana kumbe!! Coz hata hizi pesa za mabarabara za World Bank zinapitia manispaa yaani ni uchakachuaji kwa kwenda mbele...bora zingeenda moja kwa moja kwa moja kwa mkandarasi...We have long way to go

Sizinga serikali kuu inashindwa kukemea kwa sababu wakati wa uchaguzi manispaa na halmashauri ndiyo wachakachuaji wazuri wa kura na kuwahakikishia vibosile kule serikali kuu ugali...........hakuna aaccountability katika khali hii....
 
urais utamvua nguo huyu mzee sasa.anaanza kutia aibu

mharakati huyu selule kuna nguvu ya kwenda huko kweli au naye anataka kuanza kutuangukia majukwaani kama kibosile wake?
 
Magufuli anajiandaa kuingia Ikulu so 10% ni muhimu kutunisha mifuko
Ameshuhudia live swahiba wake -Raila akigaragazwa kama kuku, lazima ajipange
 
Magufuli anajiandaa kuingia Ikulu so 10% ni muhimu kutunisha mifuko
Ameshuhudia live swahiba wake -Raila akigaragazwa kama kuku, lazima ajipange

Mwakalinga Y. R na yeye asubiri kusulubiwa na wapigakura wasiotaka mchezo.........kama wale wa kenya.
 
Ruta,
Umesema yote na mengi nakubaliana nayo.

Kitu ulichosahau ni kuwa hayo makampuni ya kizalendo kiwango chao cha ufanyaji kazi ni hafifu sana.
In fact mengi ni kama conduit tu ya pesa za umma. Yaani mtu X ana kampuni A ya ukandarasi kwa ajili ya akina ABCD wanaopiga krosi.

Kwakweli tatizo ni sisi wenyewe, na nasema heri overpriced ya Kajima kazi ifanyike kuliko mkandarasi mzawa anayeweka lami kwa kutumia fagio na kamashine kamoja kabovu kalikopaki pembeni mwa bara bara. Utapeli mtupu.

Hawa wageni siyo wachina, ninaamaanisha Makampuni yaenye heshima zao. Nasema wapewe tu maana sisi hatuwezi ni projo utapeli na kulalama. Kazi hatuwezi wapewe wageni.
 
NasDaz serikali kuu ndiyo chanzo cha haya yote. TUnapaswa kujifunza kutoka Kenya uwajibikaji umeongezeka maradufu kwa sababu magavana wanachaguliwa moja kwa moja na wapigakura hakuna cha DED kuletwa na serikali kuu. Ajira zote ni jukumu la madiwani na hakuna kuhamishwa kwenda kaunti nyingine.........bila ya kujenga upysa uwajibikaji kwenye Manispaa na Halmashauri tutajikuta kila siku tunalaumiana tu!
Ruta,
FISADI NI FISADI tu, awe amepigiwa kura na wananchi au ameteuliwa! Tena kwa hapa kwetu, ulete watendaji ambao wamechaguliwa na wananchi, usikute ndo wakaharibu zaidi; why? coz' wanaweza kuleta politics instead of professionalism! Hivi umeshawahi kujiuliza ni kwanini ma-DED kwa upande mmoja na madiwani na wabunge kwa upande mwingine huwa hawaelewani?! Mara nyingi madiwani na wabunge huwa wanataka kuleta siasa kwenye serious issues ili mradi tu waonekani wazuri kwa wapiga kura! Na hata ma-DC na wabunge, huwa hawaelewani for the same reason!

Hilo la kupeleka ajira zote kwa madiwani ndo wala usithubutu kushauri! Hapo fahamu kwamba watakaoajiriwa na watoto wa mjomba na mashangazi! Uliza wakati ajira zinatolewa na Halmashauri moja kwa moja...utapata jibu! Isitoshe, hawa madiwani ni very corrupt at their level! Narudia, madiwani ni one of the most corrupting community hapa nchini sema tu hawajulikani!

Binafsi, sioni tatizo la DED kutoka serikali kuu! Tatizo ninaloona kwao ni ukosefu wa uwajibikaji na ubunifu! Unajua DED is like CEO of larger business firm! So, unapokuwa na CEO ambae ni less creative then mambo mengi hayataenda! Kama unapata perfect chemistry btn DED and Head of Departments, then mambo mengi yangewezekana!! Lakini kwavile hawapo committed enough, ndo maana unakuta ni jambo la kawaida kabisa kuona fedha za halmshauri kutoka Akaunt X zinarudishwa serikali kuu kwavile hazikutumika!! Yaani hazikutumika wakati wananchi wana matatizo kibao!

Hilo la kujenga upya uwajibikaji ni kama sijakuelewa...sijui unataka kumaanisha nini?! Kama unamaanisha uwajibikaji kama uwajibikaji basi nakuunga mkono kwa 100%. Hilo ndilo tatizo la pili la msingi la kwanza likiwa ni corruption! Inahuzunisha lakini ndio ukweli wenyewe! Tanzanian community ni very corrupt at all level! Kenyans wenzetu, nao ni very corrupt kama sisi! Hata hivyo, wenzetu ndo wametuzidi hapo kwenye uwajibikaji! Unakuwa na corrupt executive/leader lakini ni very responsible as well! Kutokana na hili, Kenyans corrupt make things happen while Tanzanians corrupt do not!
 
NasDaz Angalau ajira imebakia nyumbani. Sasa hao takukuru wao kazi ni kuchapana risasi tu na kulipana mishara na posho bila ya kuvuja jasho?
WITH due respect SIR, next time usinitajie TAKUKURU....wananichefua hawa wadudu hadi najisikia hasira kila ninapokutana na jina lao! Next time just use Corruption Endorsement Gang or simply CEG....nitakuwa nimekuelewa unamaanisha nini!
 
Back
Top Bottom