Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Juzi hivi Magufuli- Waziri wa Miundo mbinu- alituhadaa pale alipokuwa akifungua mkutano wa TANROADS kule Mwanza kuwa kuanzia sasa fedha za bajeti ya ROAD FUND kuwanufaisha wazawa na kwa kufanya hivyo hakuwa mkweli hata kidogo.
Wakati umefika wanasiasa waache porojo kwa sababu na sisi tuna macho na masikio na mbongo za kutafakari kauli zao, pia.
Matatizo ya kauli ya Magufuli ni kama ifuatavyo:-
1) Msimamo wa serikali kwa makampuni ya ujenzi ya wazawa ni ujima kwa maana waungane kama vile vijiji vya ujamaa au vyama vya ushirika vilivyoshindikana na kufa kifo cha paka shume kwa matatizo ya umiliki n.k; ili pia, kampuni za ujenzi zife na serikali waweze kuwaneemesha wageni kiulaini kwa madai potofu wazawa kwisha khabari yao kumbe sera za serikali ndiyo shubiri yao!
2) Hakuna sheria hivi sasa ambazo zinailazimisha serikali kupitia TANROADS kutoa kazi za fedha za ROAD FUND kwa makampuni ya wazalendo hivyo kufanya kauli za Magufuli kuwa gumzo la kijiweni. Serikali ambayo kweli inajali soko la ajira la ndani ingelikuwa imekwisha kutunga sheria stahiki siku mingi kabisa.......................na kutuondolea huu utapeli wa domokaya.
3) Wakati Magufuli akiropoka utapeli tajwa wakati huohuo TANROADS ilikuwa inatoa kazi lukuki kwa kampuni za kigeni kwa malipo ya ROAD FUND na hivyo kufanya kauli zake kuwa ni za kitapeli na sijui anamtapeli nani?
4) Khoja ya kuwa kampuni za kizalendo hazina mitaji ni khoja ambazo zinashindwa kukiri kuwa jukumu la serikali ni kuwajengea mazingira mazuri raia wake kuweza kutatua matatizo ya nchi yao badala ya kuwakandia. Jukumu la serikali ni kujenga mazingira ya utoaji wa mikopo isiyo na riba ya kununulia mitaji ili kazi karibu zote zifanywe na wazalendo na kuliinua soko la ajira la hapa nchini.
5) Sheria hazipo zakuhakikisha miradi yote ya ujenzi inasimamiwa na wazalendo ambao tumewasomesha kwa gharama ya kutisha na kwa kutofanya hivyo serikali inajima nafasi ya kunufaika na wataalamu hao na huku gharama za miradi mingi zinakosa ushindani na kuwa mzigo kwa taifa. Kutokana na ukosefu wa ushindani ambao serikali inahusika moja kwa moja kwenye hilo miradi mingi imekumbwa na mushkeli wa "overinvoicing" na kufanya jitihada za serikali kujenga miundo mbinu nyingi kukwama kabisa kutokana na bei za kutisha za makandarasi wageni hapa nchini.
6) Serikali inawahusudu wageni kwa kuwa huwapelekea "ten percent" kwenye akaunti zao uswisi na ndiyo maana pamoja na kulia na bei za makandarasi wengi ni za kutisha hawako tayari kuachia mkate wao na kubadilisha mfumo mzima wa utendaji ndani ya Wizara ya miundo mbinu ikiwa pamoja na TANROADS.
7) Magufuli alizungumzia utendaji wa TANROADS lakini alionekana ni mwoga kuleta mabadiliko yenye tija kwa sababu uozo ndani ya TANROADS ni kipato kikubwa kwake na wenzie ndani ya serikali. Haiwezekani miradi mingi tena yenye kuligharimu taifa pesa nyingi zifujwe na hakuna ambaye huwajibishwa. Haiwezekani ajira ndani ya TANROADS ziwe za milele bila kupimwa kila baada ya miaka mitano kwa mikataba mifupi fupi kama siyo kulindana.