GE2025 Kassim Majaliwa atangaza ghafla kutogombea tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa

GE2025 Kassim Majaliwa atangaza ghafla kutogombea tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Huyu kagundua mapema kuwa mwaka huu hakutakuwa na uchaguzi kama reforms hazitafanyika. Lkn pia anafahamu kuwa endapo reforms zitafanyika chadema inachukuwa nchi.

Mungu ibariki chadema!
Akili matope, nchi gani wanachukua ambao hawashiriki uchaguzi? Hao red brigade ndo wa kuchukua nchi?
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ametangaza rasmi kustaafu kugombea tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa, mkoani Lindi, baada ya kuliongoza kwa takribani miaka 15 mfululizo tangu mwaka 2010.

Soma, Pia: Waziri Mkuu, Majaliwa atangaza kugombea tena Ubunge wa Ruangwa akiaga Bunge

Vyanzo vyetu vya habari kutoka kwa wandani wa Waziri Mkuu Majaliwa vimeieleza Jambo TV kuwa, akiwa jimboni kwake Ruangwa kwa siku kadhaa za mashauriano na wananchi na wazee wa eneo hilo, Majaliwa amefikia uamuzi huo baada ya tafakari ya kina na ushauri wa wadau mbalimbali na amewashukuru Wanaruangwa kwa kipindi chote cha miaka 15 ya kumpa ubunge na kuwawakilisha vyema.

Hatua hiyo imekuja siku chache tu baada ya Majaliwa kutangaza Bungeni, Juni 26, 2025, kuwa anapanga kugombea tena ubunge wa jimbo hilo, akisisitiza kuwa anaendelea kuhitaji ridhaa ya wananchi. Hata hivyo, kauli hiyo sasa imebadilika rasmi.

"Ninatambua wakati mwingi nimekuwa nje ya jimbo nikilitumikia taifa lakini wana Ruangwa wameendelea kuniunga mkono. Nitumie nafasi hii kusema asanteni sana na ninamuomba Mwenyezimungu azidi kuimarisha mshikamano uliopo kati yetu sote. Ninaomba kuwajulisha kuwa ninakuja kuchukua fomu ya kuomba ridhaa yenu tena.", alinukuliwa bungeni.

Uamuzi wa Majaliwa umepokelewa kwa hisia tofauti, huku baadhi ya wachambuzi wa siasa wakiutaja kuwa ni uamuzi wa busara na wa kiungwana, hasa baada ya kumaliza kipindi chake cha miaka 10 cha Uwaziri Mkuu tangu alipoteuliwa mwaka 2015.

Hatua hii pia inakuja wakati chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikiwa katika harakati za ndani za uteuzi wa wagombea wa nafasi za udiwani na ubunge kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Zoezi hilo limeanza Juni 28 na linatarajiwa kukamilika Julai 2, 2025.

Chanzo: Jambo TV
Lukuvi, Marry Nagu and the like wajifunze kupitia Mh. Majaliwa, madaraka ni kuwatumikia wananchi, si kutumikia kooo na familia!
 
Huyu kagundua mapema kuwa mwaka huu hakutakuwa na uchaguzi kama reforms hazitafanyika. Lkn pia anafahamu kuwa endapo reforms zitafanyika chadema inachukuwa nchi.

Mungu ibariki chadema!
🤣🤣🤣🤣 Dah baingi izo
 
Huyu washauri wake wako sahihi sana, ile kupewa naibu wake, wakati cheo hiko hakipo kabisa ktk katiba, ilikua ni dharau na matusi kwake. Ilitakiwa ajiuzuru punde tyuuh.

Kila la kheri kwake, ktk maisha ya ustaafu wake.m
Hakipo kikatiba lakini pia katiba inamruhusu Rais kuanzisha nafasi yoyote ya kiuongozi kwa jinsi atakavyoona inafaa
 
Back
Top Bottom