GE2025 Kassim Majaliwa atangaza ghafla kutogombea tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mimi nashauri ajipange kwa mwaka 2030 kutokana na miiko ya ssm waliyojiwekea japo sio kwamba nitampigia kura, hilo nalisema kwa ajili ya uhai wa chama chao
Mwaka 2020 atakuwa na miaka 70s unafikiri umri huo atafanya nini akili ikiwa imechoka
 
Salaam!

Tunasikia tu habari kuwa ameghairi kugombea Ubunge ambapo Yeye mwenyewe kwa kauli yake alisikika akidai atagombea.

Sasa ni muhimu atoke hadharani na kusema hayo.

Nawasilisha 🙏
 
Katumia akili nategemea na wazee wenzake Kama akina
Lukuvi
Kabudi
Mulamula
Na wao kukaa pembeni
 
  • Thanks
Reactions: naa
Awali Aliwahi kutangaza kugombea sema itakuwa ameamua Kwa shingo upande maana miaka 15 tuu Bungeni ila 10.kama PM alipewa ngekewa.

Sasa anarudi back bencher kutoa ushauri.

Biteko kama ni raia basi u PM ni wake.
Biteko ni mtu sana sema sasa changamoto ilo lingine ndo tatizo
 
Sijui team yetu itakuaje sasa, ile timu ilikua inaleta ushindani wa kweli. Yanga na Simba walikua wanapata tabu sana kuchukua point za wale wana Lindi 😢 😭 😿 😢
 
Ukiangalia mafao ya Waziri Mkuu Mstaafu, hana sababu ya kung'ang'ania ubunge.

Amandla...
 
Yaani hili tu ndo limekufanya unitukane "mpumbavu?"

Huu ni mjadala tu na mimi nimeandika ninachofikiri tena nimesema specific kuwa "these are my speculations" halafu wewe unanitukana, why..??

Sikia bwana Lucha. Hilo tusi likurudie wewe mwenyewe kichwani mwako na familia na watoto wako...!
Mpumbavu siyo tusi ni sifa, kwahiyo nimekusifia
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ametangaza rasmi kustaafu kugombea tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa, mkoani Lindi, baada ya kuliongoza kwa takribani miaka 15 mfululizo tangu mwaka 2010.

Soma, Pia: Waziri Mkuu, Majaliwa atangaza kugombea tena Ubunge wa Ruangwa akiaga Bunge

Vyanzo vyetu vya habari kutoka kwa wandani wa Waziri Mkuu Majaliwa vimeieleza Jambo TV kuwa, akiwa jimboni kwake Ruangwa kwa siku kadhaa za mashauriano na wananchi na wazee wa eneo hilo, Majaliwa amefikia uamuzi huo baada ya tafakari ya kina na ushauri wa wadau mbalimbali na amewashukuru Wanaruangwa kwa kipindi chote cha miaka 15 ya kumpa ubunge na kuwawakilisha vyema.

Hatua hiyo imekuja siku chache tu baada ya Majaliwa kutangaza Bungeni, Juni 26, 2025, kuwa anapanga kugombea tena ubunge wa jimbo hilo, akisisitiza kuwa anaendelea kuhitaji ridhaa ya wananchi. Hata hivyo, kauli hiyo sasa imebadilika rasmi.

"Ninatambua wakati mwingi nimekuwa nje ya jimbo nikilitumikia taifa lakini wana Ruangwa wameendelea kuniunga mkono. Nitumie nafasi hii kusema asanteni sana na ninamuomba Mwenyezimungu azidi kuimarisha mshikamano uliopo kati yetu sote. Ninaomba kuwajulisha kuwa ninakuja kuchukua fomu ya kuomba ridhaa yenu tena.", alinukuliwa bungeni.

Uamuzi wa Majaliwa umepokelewa kwa hisia tofauti, huku baadhi ya wachambuzi wa siasa wakiutaja kuwa ni uamuzi wa busara na wa kiungwana, hasa baada ya kumaliza kipindi chake cha miaka 10 cha Uwaziri Mkuu tangu alipoteuliwa mwaka 2015.

Hatua hii pia inakuja wakati chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikiwa katika harakati za ndani za uteuzi wa wagombea wa nafasi za udiwani na ubunge kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Zoezi hilo limeanza Juni 28 na linatarajiwa kukamilika Julai 2, 2025.

Chanzo: Jambo TV
Mh Majaliwa Pumzika pumzika mambo makubwa yako mbeleni uwe na amani jamuhuri ipo kukulinda mpaka mwisho. Amen umevipiga vita vya imani na mwendo umeumaliza mnara utajengwa pale sabasaba well done agent.
 
Sijui team yetu itakuaje sasa, ile timu ilikua inaleta ushindani wa kweli. Yanga na Simba walikua wanapata tabu sana kuchukua point za wale wana Lindi 😢 😭 😿 😢
Majaliwa ni Rais ajae mama yako Mkoloni Kaburu toka Zanzibar watamwengua mbio za Urais
 
Wacha akapumzike kwani pesa alizokusanya zinatosha kula hadi vitukuu vya vitukuu vyake
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ametangaza rasmi kustaafu kugombea tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa, mkoani Lindi, baada ya kuliongoza kwa takribani miaka 15 mfululizo tangu mwaka 2010.

Soma, Pia: Waziri Mkuu, Majaliwa atangaza kugombea tena Ubunge wa Ruangwa akiaga Bunge

Vyanzo vyetu vya habari kutoka kwa wandani wa Waziri Mkuu Majaliwa vimeieleza Jambo TV kuwa, akiwa jimboni kwake Ruangwa kwa siku kadhaa za mashauriano na wananchi na wazee wa eneo hilo, Majaliwa amefikia uamuzi huo baada ya tafakari ya kina na ushauri wa wadau mbalimbali na amewashukuru Wanaruangwa kwa kipindi chote cha miaka 15 ya kumpa ubunge na kuwawakilisha vyema.

Hatua hiyo imekuja siku chache tu baada ya Majaliwa kutangaza Bungeni, Juni 26, 2025, kuwa anapanga kugombea tena ubunge wa jimbo hilo, akisisitiza kuwa anaendelea kuhitaji ridhaa ya wananchi. Hata hivyo, kauli hiyo sasa imebadilika rasmi.

"Ninatambua wakati mwingi nimekuwa nje ya jimbo nikilitumikia taifa lakini wana Ruangwa wameendelea kuniunga mkono. Nitumie nafasi hii kusema asanteni sana na ninamuomba Mwenyezimungu azidi kuimarisha mshikamano uliopo kati yetu sote. Ninaomba kuwajulisha kuwa ninakuja kuchukua fomu ya kuomba ridhaa yenu tena.", alinukuliwa bungeni.

Uamuzi wa Majaliwa umepokelewa kwa hisia tofauti, huku baadhi ya wachambuzi wa siasa wakiutaja kuwa ni uamuzi wa busara na wa kiungwana, hasa baada ya kumaliza kipindi chake cha miaka 10 cha Uwaziri Mkuu tangu alipoteuliwa mwaka 2015.

Hatua hii pia inakuja wakati chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikiwa katika harakati za ndani za uteuzi wa wagombea wa nafasi za udiwani na ubunge kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Zoezi hilo limeanza Juni 28 na linatarajiwa kukamilika Julai 2, 2025.

Chanzo: Jambo TV
Kassim Majaliwa Kassim ni miongoni mwa Presidential materials.
 
Akachukue fomu ya urais wachuane na bi porojo 😹😹
 
Back
Top Bottom