GE2025 Kassim Majaliwa atangaza ghafla kutogombea tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa

GE2025 Kassim Majaliwa atangaza ghafla kutogombea tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Unazungumzia watu wasiojitambua na kujua wanataka nini
Wewe ndiyo hujitambui kwani mpina huzungumzia ufisadi wote hujawahi kumwelewa? au weee ni mnufaika wa Wizi wa pesa za umma? Gwajima kaukataa Utekaji mauaji manyanyaso kwa wapinzani kwani wewe ni mnufaika wa matendo haramu ya kishetani?
 
Naona kaona haina haja ya kutoka kuwa PM kwenda kuwa mbunge tu ilihali Bashite kashaandaliwa shavu, ni kushusha CV
 
Pumzika kwa Heshima baada ya Miaka 10 ya kujitolea vipawa vyako vya uongozi.
 
Ni ujinga ulkua Wazir mkuu,misafara ulkua nayo unapita ving'ora kila sehem alaf unastaafu unaanza Tena kupanga folen umpishe Wazir mkuu apite ww na ww unaelekea bungen
Pengine alikua na speculation kwamba akipita atakua tena W/Mkuu.
 
Kama kweli ametqngaza kustaafu basi nampa HONGERA nyigi sana.
ataendelea kubaki na heshima yake kwa kuitumikia nchi yetu kwa uaminifu na uadilifu.
 
Hakipo kikatiba lakini pia katiba inamruhusu Rais kuanzisha nafasi yoyote ya kiuongozi kwa jinsi atakavyoona inafaa
It means Kasim hakuweza kumudu nafas ya u PM, hadi akapewa deputy, ilitakiwa ajiuzuru punde tyuuh.
Ilikua ni matusi na dharau kwake, Lol
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ametangaza rasmi kustaafu kugombea tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa, mkoani Lindi, baada ya kuliongoza kwa takribani miaka 15 mfululizo tangu mwaka 2010.

Soma, Pia: Waziri Mkuu, Majaliwa atangaza kugombea tena Ubunge wa Ruangwa akiaga Bunge

Vyanzo vyetu vya habari kutoka kwa wandani wa Waziri Mkuu Majaliwa vimeieleza Jambo TV kuwa, akiwa jimboni kwake Ruangwa kwa siku kadhaa za mashauriano na wananchi na wazee wa eneo hilo, Majaliwa amefikia uamuzi huo baada ya tafakari ya kina na ushauri wa wadau mbalimbali na amewashukuru Wanaruangwa kwa kipindi chote cha miaka 15 ya kumpa ubunge na kuwawakilisha vyema.

Hatua hiyo imekuja siku chache tu baada ya Majaliwa kutangaza Bungeni, Juni 26, 2025, kuwa anapanga kugombea tena ubunge wa jimbo hilo, akisisitiza kuwa anaendelea kuhitaji ridhaa ya wananchi. Hata hivyo, kauli hiyo sasa imebadilika rasmi.

"Ninatambua wakati mwingi nimekuwa nje ya jimbo nikilitumikia taifa lakini wana Ruangwa wameendelea kuniunga mkono. Nitumie nafasi hii kusema asanteni sana na ninamuomba Mwenyezimungu azidi kuimarisha mshikamano uliopo kati yetu sote. Ninaomba kuwajulisha kuwa ninakuja kuchukua fomu ya kuomba ridhaa yenu tena.", alinukuliwa bungeni.

Uamuzi wa Majaliwa umepokelewa kwa hisia tofauti, huku baadhi ya wachambuzi wa siasa wakiutaja kuwa ni uamuzi wa busara na wa kiungwana, hasa baada ya kumaliza kipindi chake cha miaka 10 cha Uwaziri Mkuu tangu alipoteuliwa mwaka 2015.

Hatua hii pia inakuja wakati chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikiwa katika harakati za ndani za uteuzi wa wagombea wa nafasi za udiwani na ubunge kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Zoezi hilo limeanza Juni 28 na linatarajiwa kukamilika Julai 2, 2025.

Chanzo: Jambo TV
Aka tubu asamehewe dhambi zaks kwa yaliyo fanywa na serikali kipindi cha utawala wake kama msimamizi mkuu wa serikali.
Watu kupotea, watu kuuawa hivyo, kesi za Kubambikiza, nk.
 
Back
Top Bottom