GE2025 Kassim Majaliwa atangaza ghafla kutogombea tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa

GE2025 Kassim Majaliwa atangaza ghafla kutogombea tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mbwa hii imekurupuka ikanijibu. Nimesema endapo reforms zikifanyika. Maana yake mifumo ya uchaguzi itakuwa mizuri na chadema itashiriki uchaguzi. Kama huna akili uwe unasoma tu comments za watu.
Kwahiyo wanaosoma comments za watu ndo hawana akili mkuu
 
Ifike hatua hata kutubu kuwe na mipaka, haiwezekani wewe ni kutesa na kuua watu miaka na miaka, utubu tuu ghafla tena baada ya kuona huna cha kupoteza halafu usamehewe zambi zotee?

Mimi kwa kweli kuna watu Ukiniambia chaugua,
1. Wote mfutiwe dhambi au
2. Kila yule ahukumiwe kwa dhambi zake..

Mimi nitaenda na 2.
🤝🤝 Nihesabie na mimi huko kwenye namba 2. Jamii haiwezi kubadilika bila accountability. Ni vyema kila mtu apatiwe namba 2.
 
Yaani hili tu ndo limekufanya unitukane "mpumbavu?"

Huu ni mjadala tu na mimi nimeandika ninachofikiri tena nimesema specific kuwa "these are my speculations" halafu wewe unanitukana, why..??

Sikia bwana Lucha. Hilo tusi likurudie wewe mwenyewe kichwani mwako na familia na watoto wako...!
Nmesikitika sana why akutukane
 
Ifike hatua hata kutubu kuwe na mipaka, haiwezekani wewe ni kutesa na kuua watu miaka na miaka, utubu tuu ghafla tena baada ya kuona huna cha kupoteza halafu usamehewe zambi zotee?

Mimi kwa kweli kuna watu Ukiniambia chaugua,
1. Wote mfutiwe dhambi au
2. Kila yule ahukumiwe kwa dhambi zake..

Mimi nitaenda na 2.
Eti Meko asaivi anastarehe kisa alimuwahi Paroko wake akaungama......
Daaaaaa.
 
Uyo ameona anaweza kugombea ubunge na akapata lakini anaweza asiteuliwe Tena kuwa waziri mkuu,,kaona ni Bora aondoke kwa heshima ya uwaziri mkuu na sio kuja kudhalilishwa Tena kama mbunge WA kawaida wakati ulishafika nafasi ya juu kabisa kiuongozi
 
Huyu washauri wake wako sahihi sana, ile kupewa naibu wake, wakati cheo hiko hakipo kabisa ktk katiba, ilikua ni dharau na matusi kwake. Ilitakiwa ajiuzuru punde tyuuh.

Kila la kheri kwake, ktk maisha ya ustaafu wake.
Bungeni alisema anakuja kuchukua form tena leo hachukui ni kama kakatazwa vile na katii amri
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ametangaza rasmi kustaafu kugombea tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa, mkoani Lindi, baada ya kuliongoza kwa takribani miaka 15 mfululizo tangu mwaka 2010.

Soma, Pia: Waziri Mkuu, Majaliwa atangaza kugombea tena Ubunge wa Ruangwa akiaga Bunge

Vyanzo vyetu vya habari kutoka kwa wandani wa Waziri Mkuu Majaliwa vimeieleza Jambo TV kuwa, akiwa jimboni kwake Ruangwa kwa siku kadhaa za mashauriano na wananchi na wazee wa eneo hilo, Majaliwa amefikia uamuzi huo baada ya tafakari ya kina na ushauri wa wadau mbalimbali na amewashukuru Wanaruangwa kwa kipindi chote cha miaka 15 ya kumpa ubunge na kuwawakilisha vyema.

Hatua hiyo imekuja siku chache tu baada ya Majaliwa kutangaza Bungeni, Juni 26, 2025, kuwa anapanga kugombea tena ubunge wa jimbo hilo, akisisitiza kuwa anaendelea kuhitaji ridhaa ya wananchi. Hata hivyo, kauli hiyo sasa imebadilika rasmi.

"Ninatambua wakati mwingi nimekuwa nje ya jimbo nikilitumikia taifa lakini wana Ruangwa wameendelea kuniunga mkono. Nitumie nafasi hii kusema asanteni sana na ninamuomba Mwenyezimungu azidi kuimarisha mshikamano uliopo kati yetu sote. Ninaomba kuwajulisha kuwa ninakuja kuchukua fomu ya kuomba ridhaa yenu tena.", alinukuliwa bungeni.

Uamuzi wa Majaliwa umepokelewa kwa hisia tofauti, huku baadhi ya wachambuzi wa siasa wakiutaja kuwa ni uamuzi wa busara na wa kiungwana, hasa baada ya kumaliza kipindi chake cha miaka 10 cha Uwaziri Mkuu tangu alipoteuliwa mwaka 2015.

Hatua hii pia inakuja wakati chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikiwa katika harakati za ndani za uteuzi wa wagombea wa nafasi za udiwani na ubunge kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Zoezi hilo limeanza Juni 28 na linatarajiwa kukamilika Julai 2, 2025.

Chanzo: Jambo TV

Mzee wa "Rais yupo Ikulu anachapa kazi" hata akikwambia atagombea tena usimuamini.

Haaminiki katika lolote.
 
Back
Top Bottom