GE2025 Kassim Majaliwa atangaza ghafla kutogombea tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa

GE2025 Kassim Majaliwa atangaza ghafla kutogombea tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mh Kassim Majaliwa Kassim ni;

πŸ“šπŸ“š Mnyenyekevu.

πŸ“šπŸ“š Patriotic.

πŸ“šπŸ“š Intelligent.

πŸ“šπŸ“š Strategic.

πŸ“šπŸ“š Calm.

πŸ“šπŸ“š Visionary.

πŸ“šπŸ“š Truthful.
Sio kuorodhesha weka vivid evidence.

Visionary Kwa lipi?

Mnyenyekevu Kwa nani na kivipi? Huyu si ndio aliteka na kuimiza washindani wake kule Ruangwa? 😁😁

Patriotic how? Kujimegea migodi ya graphite ndio patriotism? 🀣🀣

Intelligent in which angle? Huyu Mwalimu mwenye diploma na Degree ya Open University ana akili zipi za maana?

Strategic ,weka hizo strategies hapa.

Truthful? Magufuli ni mzima anachapa kazi πŸ€ͺπŸ€ͺ

Haya mambo uwe unawaambia wenye akili za funza na wajinga kama wewe.

Huyu bwana alikoswa koswa kutimukiwa mara 2 na Mwendazake na SSH walikuwa wanamvumilia tuu πŸ˜†πŸ˜†
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ametangaza rasmi kustaafu kugombea tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa, mkoani Lindi, baada ya kuliongoza kwa takribani miaka 15 mfululizo tangu mwaka 2010.

Soma, Pia: Waziri Mkuu, Majaliwa atangaza kugombea tena Ubunge wa Ruangwa akiaga Bunge

Vyanzo vyetu vya habari kutoka kwa wandani wa Waziri Mkuu Majaliwa vimeieleza Jambo TV kuwa, akiwa jimboni kwake Ruangwa kwa siku kadhaa za mashauriano na wananchi na wazee wa eneo hilo, Majaliwa amefikia uamuzi huo baada ya tafakari ya kina na ushauri wa wadau mbalimbali na amewashukuru Wanaruangwa kwa kipindi chote cha miaka 15 ya kumpa ubunge na kuwawakilisha vyema.

Hatua hiyo imekuja siku chache tu baada ya Majaliwa kutangaza Bungeni, Juni 26, 2025, kuwa anapanga kugombea tena ubunge wa jimbo hilo, akisisitiza kuwa anaendelea kuhitaji ridhaa ya wananchi. Hata hivyo, kauli hiyo sasa imebadilika rasmi.

"Ninatambua wakati mwingi nimekuwa nje ya jimbo nikilitumikia taifa lakini wana Ruangwa wameendelea kuniunga mkono. Nitumie nafasi hii kusema asanteni sana na ninamuomba Mwenyezimungu azidi kuimarisha mshikamano uliopo kati yetu sote. Ninaomba kuwajulisha kuwa ninakuja kuchukua fomu ya kuomba ridhaa yenu tena.", alinukuliwa bungeni.

Uamuzi wa Majaliwa umepokelewa kwa hisia tofauti, huku baadhi ya wachambuzi wa siasa wakiutaja kuwa ni uamuzi wa busara na wa kiungwana, hasa baada ya kumaliza kipindi chake cha miaka 10 cha Uwaziri Mkuu tangu alipoteuliwa mwaka 2015.

Hatua hii pia inakuja wakati chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikiwa katika harakati za ndani za uteuzi wa wagombea wa nafasi za udiwani na ubunge kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Zoezi hilo limeanza Juni 28 na linatarajiwa kukamilika Julai 2, 2025.

Chanzo: Jambo TV
Kwa hiyo Namungo ndio basi tena πŸ€ͺπŸ€ͺ
 
Hafai aende tu, alikua muongo muongo sana na cheo cha Uwaziri mkuu kilimpwaya sana ni kama vile hakuwepo. Kingine hivi bongo kuna ulazima wa kua na Makamu wa Rais na Waziri mkuu kweli?? Hii ni kupoteza tu pesa za walipa kodi.
 
Jambo jema kafanya
Huwezi kutoka kuwa waziri
Mkuu alafu urudi kugonga meza,
Kuomba maji,barabara

Mtu kama ndugai alitakiwa
Naye ubunge ajitoe awapishe
Wengine

Ova
 
The New President..

Nangu Nyau- ndani ya viunga vya Tehrani.
 
Usishangae kuona Makonda ndio waziri mkuu ajaye.
 
Wenye chama chao hawamtaki Mkoloni Kaburu toka Zanzibar aendelee kutawala Tanganyika wanamtaka majaliwa awe Rais
Hii video inanena mengi sana. Wapo wengi sana kama hawa, tutawajua tu kadri muda unavyokwenda
 
Awali Aliwahi kutangaza kugombea sema itakuwa ameamua Kwa shingo upande maana miaka 15 tuu Bungeni ila 10.kama PM alipewa ngekewa.

Sasa anarudi back bencher kutoa ushauri.

Biteko kama ni raia basi u PM ni wake.
Una maanisha Nini mkuu
 
Huyu kagundua mapema kuwa mwaka huu hakutakuwa na uchaguzi kama reforms hazitafanyika. Lkn pia anafahamu kuwa endapo reforms zitafanyika chadema inachukuwa nchi.

Mungu ibariki chadema!
Day dream
 
Lukuvi ameshachukua fomu tayari, na inatabiriwa kuwa ni PM ajae. Lol
🀣🀣 Hii umetembea na bet ya odd 255,
Kwa siasa za miaka hii ni rahisi kumfikiria makonda anaweza kula shavu sio huyo mzee,
Nyakati.
 
Majaliwa alikuwa anafiti sana wakati wa Jpm!

Sasa kaona hawezi kufanya kazi na watu wajinga.
 
Mbunge wetu wa Mpanda Magharibi( Selemani Kakoso) kwa hekima zako tunaamini utafuata nyayo za Waziri mkuu maana tangu 2010 upo kwenye ubunge. Waachie vijana wenye nguvu na maono mapya waendeleze pale ulipofikia.
 
Back
Top Bottom