Kassim Majaliwa: Namuagiza Naibu Waziri Mkuu kushughulikia suala la uhaba wa mafuta nchini

Kassim Majaliwa: Namuagiza Naibu Waziri Mkuu kushughulikia suala la uhaba wa mafuta nchini

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Naibu Waziri Mkuu, Dk Dotto Biteko kukaa na wadau wa mafuta ili washughulikie changamoto ya upatikanaji ndani ya siku saba.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Septemba 7, 2023 alipokuwa anajibu maswali ya papo kwa hapo kutoka kwa wabunge katika kipindi cha asubuhi.

Katika swali la msingi, Mbunge wa Lushoto (CCM) Rashid Shangazi alitaka kujua Serikali inaweka mkakati gani kuhakikisha upatikanaji wa mafuta unakuwa ni mzuri nchini.

Mbunge huyo amesema kumekuwa na sintofahamu kuhusu suala la mafuta kwani licha ya bei zinazopanda kila wakati lakini mafuta hayo huwa hayapatikani kila inapofika jumatano ya kwanza ya mwezi ambayo ni siku ya kutangaza bei mpya ya bidhaa hiyo.

“Nikiri tunayochangamoto ya mafuta nchini, lakini zipo jitihada mbalimbali ambazo zinachukuliwa na Serikali kuondokana na tatizo hilo kwani nishati hiyo ndiyo injini ya uchumi,” amesema Majaliwa.

Waziri Mkuu amesema tayari Rais alishamteua Naibu Waziri Mkuu ambaye ni Waziri wa Nishati pia ambaye ameanza kushughulikia jambo hilo kwa kukaa na wadau mbalimbali.

“Niendelee kumuagiza Naibu Waziri Mkuu aendelee kushughulikia hili ndani ya wiki moja tuwe na majibu na katika hilo wapanue wigo kwa waagiza mafuta ili tuwe na mafuta ya kutosha na suala la bei tutaangalia huko mbeleni,” amesema Majaliwa.

Mjadala huo umeibuka ikiwa ni siku moja tu tangu Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) kutangaza bei mpya za mafuta zitakazotumika Septemba ambazo zimepaa ikilinganishwa na Agosti.

Katika taarifa kwa umma iliyotolewa jana Jumanne Septemba 5, 2023 saa 4 usiku na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Dk James Mwainyakule imeonesha kuwa kuanzia Jumatano Septemba 6 jijini Dar es Salaam petroli itauzwa Sh3,213 na dizeli itauzwa kwa Sh3,259.

Bei hizo zinamaanisha kuwa katika Mkoa wa Dar es Salaam petroli imeongezeka kwa Sh14 kutoka Sh3,199 ya Agosti huku dizeli ikiongezeka zaidi kwa Sh324.

MWANANCHI
Maigizo jazz band
 
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 12, Kikao cha 8, leo Septemba 7, 2023.

Ratiba:
  1. Hati za kuwasilishwa Mezani​
  2. Maswali kwa Waziri Mkuu​
  3. Maswali ya kawaida​
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Namuagiza Naibu Waziri Mkuu kushughulikia suala la ukosefu wa mafuta nchini.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amekiri uwepo wa changamoto ya uhaba wa mafuta nchini wakati akijibu swali la Rashid Shangazi, Mbunge wa mlalo (CCM) aliyetaka kufahamu mipango ya Serikali katika kukabiliana na changamoto kubwa ya uhaba wa mafuta nchini.

"Kwanza nikiri kwamba tunazo changamoto za upatikanaji wa mafuta nchini kwa sababu baadhi ya vituo kwenye maeneo mbalimbali vimekuwa vikikosa mafuta na watanzania wanaohitaji huduma hii maeneo kadhaa tumeona wakiwa wanalalamika kukosekana kwa mafuta" amesema.

Waziri Majaliwa amesema zipo jitihada kadhaa zinazofanywa na Serikali kuondoa tatizo la uhaba wa upatikanaji wa mafuta na amemuagiza Naibu Waziri Mkuu kushughulikia suala hili, muhimu zaidi nishati yenyewe ipatikane nchini.

Kamsukumia kaa la moto
 
Bungeni

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Naibu Waziri Mkuu, Dk Dotto Biteko kukaa na wadau wa mafuta ili washughulikie changamoto ya upatikanaji ndani ya siku saba.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Septemba 7, 2023 alipokuwa anajibu maswali ya papo kwa hapo kutoka kwa wabunge katika kipindi cha asubuhi.

Katika swali la msingi, Mbunge wa Lushoto (CCM) Rashid Shangazi alitaka kujua Serikali inaweka mkakati gani kuhakikisha upatikanaji wa mafuta unakuwa ni mzuri nchini.

Mbunge huyo amesema kumekuwa na sintofahamu kuhusu suala la mafuta kwani licha ya bei zinazopanda kila wakati lakini mafuta hayo huwa hayapatikani kila inapofika jumatano ya kwanza ya mwezi ambayo ni siku ya kutangaza bei mpya ya bidhaa hiyo.

“Nikiri tunayochangamoto ya mafuta nchini, lakini zipo jitihada mbalimbali ambazo zinachukuliwa na Serikali kuondokana na tatizo hilo kwani nishati hiyo ndiyo injini ya uchumi,” amesema Majaliwa.

Waziri Mkuu amesema tayari Rais alishamteua Naibu Waziri Mkuu ambaye ni Waziri wa Nishati pia ambaye ameanza kushughulikia jambo hilo kwa kukaa na wadau mbalimbali.

“Niendelee kumuagiza Naibu Waziri Mkuu aendelee kushughulikia hili ndani ya wiki moja tuwe na majibu na katika hilo wapanue wigo kwa waagiza mafuta ili tuwe na mafuta ya kutosha na suala la bei tutaangalia huko mbeleni,” amesema Majaliwa.

Mjadala huo umeibuka ikiwa ni siku moja tu tangu Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) kutangaza bei mpya za mafuta zitakazotumika Septemba ambazo zimepaa ikilinganishwa na Agosti.

Katika taarifa kwa umma iliyotolewa jana Jumanne Septemba 5, 2023 saa 4 usiku na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Dk James Mwainyakule imeonesha kuwa kuanzia Jumatano Septemba 6 jijini Dar es Salaam petroli itauzwa Sh3,213 na dizeli itauzwa kwa Sh3,259.

Bei hizo zinamaanisha kuwa katika Mkoa wa Dar es Salaam petroli imeongezeka kwa Sh14 kutoka Sh3,199 ya Agosti huku dizeli ikiongezeka zaidi kwa Sh324.

Kwa upande wake Spika wa Bunge Dk Tulia Akson Mwansasu ametoa ushauri kwa serikali kuwa ifanye tathmini kuhusu mfumo wa uagizaji mafuta kuona kama una kasoro urekebishwe au ubadilishwe ili kukimbia changamoto zinajitokeza sasa kwenye eneo la upatikanaji wa nishati ya mafuta.
"Serikali ifanye tathmini kuona kama huu mfumo wa sasa unaleta shida ubadilishwe maana haiwezekani tatizo kuwa linajirudia mara Kwa mara kama vipi turudi katika mfumo wa zamani" Alisema Dk Tulia.
 
Ilitakiwa iwe the other way around Biteko ndo angetoa siku tano.
 
Hiyo ndio itifaki inavyotaka , Rais anamuagiza PM, PM anamuagiza DPM, DPM anamuagiza Waziri, Waziri anamuagiza Karibu Mkuu na Katibu mkuu anawaagiza watendaji wakuu wa idara na taasisi zilizopo chini ya wizara na hao pia wanawaagiza watumishi wengine. Hapo hakuna mzigo mzito kwa mtu wala nini
Mtu wa mwisho kuagizwa ni mimi nikakamue mpapai nipate mafuta ya bodaboda yangu.
Kutokana na mlolongo wako waziri mkuu kazi yake ni maagizo, hasara kwa taifa.
 
mheshiwa kapatamsaidizi muruwa kilichobaki apigekazitu kusakamaendeleo
 
Mimi nashauri Serikali ikae tu na Mbunge wa Gairo mh Ahmed Shabiby ana uzoefu mkubwa kwenye Hiyo sekta ya Petrol, Diesel na Kerosine

Majibishano ya Bungeni ni dhahiri hali ni tete

Mungu wa mbinguni awape Wepesi 😀
 
Anayefanya biashara ni waziri,mbunge Unategemea nini!huko kanda ya ziwa anayefanya biashara ya pamba ni mbunge halafu anataka bei ya pamba iwe shilingi kumi ili yeye akauza shilingi 2000 unaona nchi yako ilipo eheeee
 
Ok, kwa hiyo sasa hivi PM anaweza kuagizwa na Rais, nae akamuagiza naibu wake, kumbe haikuwa kazi kubwa kama nilivyodhani mwanzo kujiuliza ni yapi yatakuwa majukumu ya naibu waziri mkuu.

Majaliwa siku hizi anaweza kuamua kwenda kupumzika nyumbani hata miezi miwili, inawezekana kuna tatizo la kiafya..
 
i guess PM kawapambanisha wao wao ili ajue kama Vpm amekuja kumsaidia au ni chawa na s💯 akiweza stabilize price ya mafuta majaliwa atajua ana mtu ila akishindwa majiliwa atajua tu ofisini kwake amekuja mamluki 😂😂😂 ni karata nzuri sana tusubiri Dr Biteko ana nini cha kuwapa watanzania 😂
 
Back
Top Bottom