Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Maigizo jazz bandWaziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Naibu Waziri Mkuu, Dk Dotto Biteko kukaa na wadau wa mafuta ili washughulikie changamoto ya upatikanaji ndani ya siku saba.
Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Septemba 7, 2023 alipokuwa anajibu maswali ya papo kwa hapo kutoka kwa wabunge katika kipindi cha asubuhi.
Katika swali la msingi, Mbunge wa Lushoto (CCM) Rashid Shangazi alitaka kujua Serikali inaweka mkakati gani kuhakikisha upatikanaji wa mafuta unakuwa ni mzuri nchini.
Mbunge huyo amesema kumekuwa na sintofahamu kuhusu suala la mafuta kwani licha ya bei zinazopanda kila wakati lakini mafuta hayo huwa hayapatikani kila inapofika jumatano ya kwanza ya mwezi ambayo ni siku ya kutangaza bei mpya ya bidhaa hiyo.
“Nikiri tunayochangamoto ya mafuta nchini, lakini zipo jitihada mbalimbali ambazo zinachukuliwa na Serikali kuondokana na tatizo hilo kwani nishati hiyo ndiyo injini ya uchumi,” amesema Majaliwa.
Waziri Mkuu amesema tayari Rais alishamteua Naibu Waziri Mkuu ambaye ni Waziri wa Nishati pia ambaye ameanza kushughulikia jambo hilo kwa kukaa na wadau mbalimbali.
“Niendelee kumuagiza Naibu Waziri Mkuu aendelee kushughulikia hili ndani ya wiki moja tuwe na majibu na katika hilo wapanue wigo kwa waagiza mafuta ili tuwe na mafuta ya kutosha na suala la bei tutaangalia huko mbeleni,” amesema Majaliwa.
Mjadala huo umeibuka ikiwa ni siku moja tu tangu Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) kutangaza bei mpya za mafuta zitakazotumika Septemba ambazo zimepaa ikilinganishwa na Agosti.
Katika taarifa kwa umma iliyotolewa jana Jumanne Septemba 5, 2023 saa 4 usiku na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Dk James Mwainyakule imeonesha kuwa kuanzia Jumatano Septemba 6 jijini Dar es Salaam petroli itauzwa Sh3,213 na dizeli itauzwa kwa Sh3,259.
Bei hizo zinamaanisha kuwa katika Mkoa wa Dar es Salaam petroli imeongezeka kwa Sh14 kutoka Sh3,199 ya Agosti huku dizeli ikiongezeka zaidi kwa Sh324.
MWANANCHI
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 12, Kikao cha 8, leo Septemba 7, 2023.
Ratiba:
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Namuagiza Naibu Waziri Mkuu kushughulikia suala la ukosefu wa mafuta nchini.
Hati za kuwasilishwa Mezani Maswali kwa Waziri Mkuu Maswali ya kawaida
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amekiri uwepo wa changamoto ya uhaba wa mafuta nchini wakati akijibu swali la Rashid Shangazi, Mbunge wa mlalo (CCM) aliyetaka kufahamu mipango ya Serikali katika kukabiliana na changamoto kubwa ya uhaba wa mafuta nchini.
"Kwanza nikiri kwamba tunazo changamoto za upatikanaji wa mafuta nchini kwa sababu baadhi ya vituo kwenye maeneo mbalimbali vimekuwa vikikosa mafuta na watanzania wanaohitaji huduma hii maeneo kadhaa tumeona wakiwa wanalalamika kukosekana kwa mafuta" amesema.
Waziri Majaliwa amesema zipo jitihada kadhaa zinazofanywa na Serikali kuondoa tatizo la uhaba wa upatikanaji wa mafuta na amemuagiza Naibu Waziri Mkuu kushughulikia suala hili, muhimu zaidi nishati yenyewe ipatikane nchini.
Wafanyabiashara wanaficha... soon baada ya tangazo la EWURA kupandisha bei za mafuta pump zote nchini zili-burst kwa kuzidiwa na wingi wa mafuta. Tatizo sio uhaba perse; kuna kitu kingine - nchi imekuwa ya cartels hii.
Mtu wa mwisho kuagizwa ni mimi nikakamue mpapai nipate mafuta ya bodaboda yangu.Hiyo ndio itifaki inavyotaka , Rais anamuagiza PM, PM anamuagiza DPM, DPM anamuagiza Waziri, Waziri anamuagiza Karibu Mkuu na Katibu mkuu anawaagiza watendaji wakuu wa idara na taasisi zilizopo chini ya wizara na hao pia wanawaagiza watumishi wengine. Hapo hakuna mzigo mzito kwa mtu wala nini
Hizi ni porojo. Walikuwa wapi wasishughulikie muda wote?Kwani yeye Kasimu asingeiweka kazi hiyo.
Labda rais wa masaburi yakoHuyu Ndio Anafaa Kuwa Rais.fullstop
Almheshiwa kapatamsaidizi muruwa kilichobaki apigekazitu kusakamaendeleo
Mgalatia mwenzenu huyo,maana january kutwa mlikuwa mnamtusi ,aya sasa tatizo la umeme alimalize yeye akisaidiwa na tecdaah biteko kazi anayooo...kaingia tu na kuwekwa mtu kati 😅 😅 😅
i guess PM kawapambanisha wao wao ili ajue kama Vpm amekuja kumsaidia au ni chawa na s💯 akiweza stabilize price ya mafuta majaliwa atajua ana mtu ila akishindwa majiliwa atajua tu ofisini kwake amekuja mamluki 😂😂😂 ni karata nzuri sana tusubiri Dr Biteko ana nini cha kuwapa watanzania 😂Ok, kwa hiyo sasa hivi PM anaweza kuagizwa na Rais, nae akamuagiza naibu wake, kumbe haikuwa kazi kubwa kama nilivyodhani mwanzo kujiuliza ni yapi yatakuwa majukumu ya naibu waziri mkuu.
Majaliwa siku hizi anaweza kuamua kwenda kupumzika nyumbani hata miezi miwili, inawezekana kuna tatizo la kiafya..