Kassim Majaliwa: Navishukuru vyama rafiki CHADEMA, CUF na ACT Wazalendo kwa kunipigia kura ya " Ndiyo" niwe Waziri mkuu!

Kassim Majaliwa: Navishukuru vyama rafiki CHADEMA, CUF na ACT Wazalendo kwa kunipigia kura ya " Ndiyo" niwe Waziri mkuu!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Waziri Mkuu mh Kassim Majaliwa amewashukuru wabunge wa vyama rafiki Chadema, Cuf na ACT wazalendo kwa kumpigia kura za "ndio" kwenye ushindi wake wa 100% wa kumthibitisha kushika wadhifa huo.

Mh Majaliwa amesema maendeleo hayana chama hivyo atashirikiana na wabunge wote bila kujali itikadi katika kuwaletea maendeleo ya haraka wananchi.

Maendeleo hayana vyama!
 
Vyama rafiki au yule mbunge ndio rafiki yenu?

Angetakiwa kusema anamshukuru mbunge rafiki kwa kumpigia kura.
Hahah mnamkataa Mbunge wenu tena? Yule ni Mbunge wa CHADEMA na yupo pale kaa ridhaa ya wananchi! Wabunge wengine akiongozwa na Mwenyekiti wenu Mbowe wameshindwa kutetea majimbo yao. Msimkatae mwenzenu kisa yuko peke yake. Ndo demokrasia hiyo vumilieni tu.
 
Maendeleo hayana vyama (wapinzani walichelewesha maendeleo).

Lakini CCM ndiyo yenye kuleta maendeleo (nileteeni flani ili niwaletee maendeleo, mkichagua upinzani sahauni maendeleo).

Kalaghabao.
 
Hahah mnamkataa Mbunge wenu tena? Yule ni Mbunge wa CHADEMA na yupo pale kaa ridhaa ya wananchi! Wabunge wengine akiongozwa na Mwenyekiti wenu Mbowe wameshindwa kutetea majimbo yao. Msimkatae mwenzenu kisa yuko peke yake. Ndo demokrasia hiyo vumilieni tu.
Umenikumbusha ya nape Nauye ya kuwashukuru wapiga kura wake, nilishangaa sana
 
Eti vyama rafiki wakati kwenye kugombea ubunge walikupitisha bila kupingwa!!

Huku ni kujikosha tu kutokana na dhuluma mlizofanyia wapinzani.
Mtu anapita bila kupingwa lakini bado anashukuru wapiga kura wake, only in Tanzania
 
Back
Top Bottom