Kassim Majaliwa: Serikali imetoaTsh. bilioni 15 kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kununua mahindi toka kwa wakulima

Kassim Majaliwa: Serikali imetoaTsh. bilioni 15 kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kununua mahindi toka kwa wakulima

Hakuna neema hapo mkuu nakupa mfano mdogo tu hapa

Mkoa wa ruvuma umezalisha ziada ya tani lak3 msimu huu lakn NFRA watanunua tani elfu 30....
Pesa za ziada za tozo zielekezwe huko, hatuwezi kuacha tani zote hizo zibaki mikononi mwa wakulima, msimu ujao watalima vipi, na kwa kipindi hiki wataishi vipi?! NFRA iongezewe fungu haraka sana!!
 
Wakulima waruhusiwe na wapewe utaratibu utakaowawezesha kuuza mazao soko la nje ya nchi ili wapate zaidi.
Kama walivyotangaza kwamba wananua,vile vile watangaze kuwa wakulima wanaruhusiwa kuuza nje ya nchi ili mwananchi/mkulima awe na wigo mpana wa kujitafutia kipato.
Nadhani kwa kipindi ambacho mazao yamezalishwa kwa wingi basi NFRA wapewe fungu la kutosha la kununua ziada yote, halafu wao sasa ndio wafanye utaratibu wa kuuza ziada nje ya nchi, tukiruhusu uuzaji holela wa kitu basic kama mahindi, tutakuja kuuana njaa humu, maana ugali ndio kimbilio la wengi kwa kupata mlo nafuu na wa kushiba hasa.

Mi vibarua huwa nawasongeaga ugali na dagaa tu, halafu wanadanganyia na tembele au mchicha pori, wanashiba vizuri then nawapigisha kazi kama matrekta, kazi inaenda, so tuwe makini na mahindi jamani....
 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeshatoa sh. bilioni 15 kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ili kununua mahindi kutoka kwa wakulima.

“Uzalishaji wa mahindi ni mkubwa lakini na sisi pia tumeimarisha hifadhi yetu ya Taifa ya chakula. NFRA tumeipa fedha za kwenda kununua mahindi kwa bei ya kumwezesha mkulima ili ajikimu hadi msimu ujao. Uwezo si mkubwa sana, lakini tumeipa shilingi bilioni 15,” amesema.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Septemba 2, 2021) Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kwela, Mheshimiwa Deus Clement Sangu kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeshatoa sh. bilioni 15 kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ili kununua mahindi kutoka kwa wakulima.

“Uzalishaji wa mahindi ni mkubwa lakini na sisi pia tumeimarisha hifadhi yetu ya Taifa ya chakula. NFRA tumeipa fedha za kwenda kununua mahindi kwa bei ya kumwezesha mkulima ili ajikimu hadi msimu ujao. Uwezo si mkubwa sana, lakini tumeipa shilingi bilioni 15,” amesema.

Ametoa kauli hiyo jana (Alhamisi, Septemba 2, 2021) Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kwela, Mheshimiwa Deus Clement Sangu kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu amesema siku nne zilizopita alikuwa ziarani mkoani Katavi na aliona hali halisi ya mlundikano wa mahindi na akakutana na watu wa NFRA ili aone kasi yao ya ununuzi ikoje.

“Nilibaini kuwa uwezo wao ni mdogo na nikapokea malalamiko ya wananchi kwamba kituo cha kupokelea mahindi kiko mbali, kwa hiyo tumeamua kuanzia sasa kila Halmashauri itapaswa iwe na kituo japo kimoja cha kupokelea mahindi ili kuharakisha ununuzi wa zao hilo.”

“Tunawahakikishia wakulima wetu kwamba tunanunua mahindi kupitia NFRA na Bodi ya Mazao Mchanganyiko na pia tumefungua milango kwa yeyote anayetaka kuuza mahindi nje. Mtu akitaka kuuza mahindi Zambia, Congo, Msumbiji au Malawi yuko huru kufanya hivyo ili mradi atoe taarifa ili nasi tujue tumeuza kiasi gani,” amesema wakati akimjibu Mhe. Sangu ambaye alitaka kujua Serikali imejipanga vipi kuziwezesha taasisi za Serikali kama NFRA ili ziweze kununua mahindi ya wakulima.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema Serikali haiwezi kuunganisha taasisi za NIDA na RITA kutokana na tofauti za majukumu yake. Alikuwa akijibu swali la Mhe. Abubakari Damian Asenga, mbunge wa Kilombero ambaye alishauri taasisi hizo ziunganishwe ili kurahisisha upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa ambavyo alisema kwa sasa vinacheleweshwa sana.
“NIDA inatoa kitambulisho cha Taifa ambacho kinamtambulisha Mtanzania na hakitolewi kwa mtu ambaye si raia wakati RITA inatoa cheti cha kuzaliwa kikionesha kuwa umezaliwa wapi, tarehe yako ya kuzaliwa na pia wanatoa cheti cha kifo.”

Amesema RITA inaweza kutoa cheti cha kuzaliwa kwa mtu yeyote aliyezaliwa Tanzania kwa sababu pale hospitalini akishazaliwa mtoto, taarifa zitaonesha hivyo na inaweza kutoa cheti kwa huyo mtoto huyo hata kama siyo Mtanzania.

“Mtu anaweza kuzaliwa Tanzania na kupewa cheti cha kuzaliwa kwa kuwa amezaliwa ndani ya nchi yetu, lakini mtu huyo anaweza asiwe Mtanzania kwa mujibu wa sheria zetu.”

Amesema taasisi hizo zinaweza kupeana taarifa pale inapobidi lakini vyote vina majukumu tofauti. “Urasimu unaosemwa hapa nimeusikia wakati nilipofanya ziara kwenye mikoa ya pembezoni. Na huko nimekuwa nikisisitiza umakini katika kuchunguza taarifa za waombaji.”

“Kuchelewa kwetu kwenye mikoa ya pembezoni ambako pia kunaitwa urasimu, kunafanywa kwa nia nzuri ili kujiridhisha kama kweli anayeomba kitambulisho ni raia wa Tanzania,” amesisitiza.

“Nataka niwahakikishie Watanzania kwamba mtu yeyote Mtanzania ambaye Baba na Mama ni Watanzania, ni lazima atapata kitambulisho cha Taifa, kikubwa wawe na subira. Nasi kwa upande wetu tumejitahidi kuongeza vifaa na watumishi ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa vitambulisho hivyo hasa kwa wale ambao wamehakikiwa na wanastahili.”
 
Waziri Mkuu ni Kiranja wa Mawaziri na manaibu wote wakiwemo watendaji wengine wa Serikali ktk idara mbalimbali tunamuomba awe mkali ili tusonge mbele kama Taifa, kuna baadhi ya watendaji hawawezi kufanya kazi hadi wasukumwe au wasimamiwe, kamwe asiwaonee muhali, hatuwezi fikia malengo kama tutaendelea kubembelezana na kuleana.

Changamoto zinazonwakabili wananchi wa Taifa hili ni nyingi mno, zipo ambazo zinaweza kutatuliwa ktk levo ya kijiji, wilaya, moka au Taifa.

Endapo kiongozi ktk kila ngazi atatekeleza wajibu wake kikamilifu hakika tutasonga, hata hivyo usimamizi wa karibu ni muhimu sana.
 
Naona PM ameteleza kidogo, fedha leo zimekuwa za serikali na wakati huwa tunaambiwa ni za Rais? shame government
 
Majaliwa ameshindwa kujiuzulu tu, ni wazi haungi juhudi za bibie.
 
Umefika wakati sasa Tanzania ipige marufuku kuuza mahindi nje ya nchi. Mahindi ni lazima yakobolewe humu humu nchini na kuweza kupata unga ili kuongeza thamani (achiia mbali bidhaa nyingine nk. Hawa wanaonunua mahindi yetu wanatuchezea sivyo waongeze bei mara tatu.
 
Unataka yatokee kama ya korosho ? Maana naamini tunazalisha mahindi mengi kuliko tunavyotumia
Hili unalisema lingewezekana kama serikali ingekua inatoa ruzuku kwenye pembejeo za kilimo
 
Unataka yatokee kama ya korosho ? Maana naamini tunazalisha mahindi mengi kuliko tunavyotumia
Hili unalisema lingewezekana kama serikali ingekua inatoa ruzuku kwenye pembejeo za kilimo
Mkuu unataka sisi tuwe watumwa milele. Kuna shida gani tukianza na packaging. Kwanza ukifanya hivyo utauza unga mwingi zaidi na ku-create employment etc. Mwanzo wa safari ni hatua moja.

BTW kuhusu korosho kama umeona USA watanunua korosho zote kutoka Tanzania ambazo ziko processed, kwa hiyo basi huo mfano wako hauna mashiko. We need to start from somewhere, and as you know starting is very difficult (always). Tanzania uwezo huo tunao tuache kulialia kama vitoto vilivyokosa lawalawa.
 
Naona PM ameteleza kidogo, fedha leo zimekuwa za serikali na wakati huwa tunaambiwa ni za Rais? shame government
Wajinga kama ww hawawezi kosekana hata serekali ifanyeje!!?
lazima utafute sehemu upake m.avi ndio raha yako!
 
Mkuu unataka sisi tuwe watumwa milele. Kuna shida gani tukianza na packaging. Kwanza ukifanya hivyo utauza unga mwingi zaidi na ku-create employment etc. Mwanzo wa safari ni hatua moja.

BTW kuhusu korosho kama umeona USA watanunua korosho zote kutoka Tanzania ambazo ziko processed, kwa hiyo basi huo mfano wako hauna mashiko. We need to start from somewhere, and as you know starting is very difficult (always). Tanzania uwezo huo tunao tuache kulialia kama vitoto vilivyokosa lawalawa.
Mkulima wa Namtumbo anayelima Kilimo cha kukopeshwa mbolea alipe gunia za mahindi ndo unamuongelea afanye packing ya unga ?
 
Kwa kuwa TMA imetangaza Hali ya ukame siku zijazo, Serikali izuie huuzwaji wa nafaka nje ya Nchi ili kukabiliana na mfumuko wa bei ambao unaweza kusababisha njaa kwa baadhi ya maeneo.
 
Wapi imesema hivyo?
Mie ndo nimekuelewa hivyo labda unifafanulie,
Kwenye swala la kilimo , mkulima wa chini ameachwa mkiwa , ataabike kulima kukopa mbolea , 2akati mwingine apate hasara kutokana na uhaba wa mvua na risks kibao, Muda pekee mkulima anakuwa kwenye spotlight za serikali ni pale anapofanikiwa kuvuna salama.
Ndipo hapo zinapojitokeza mamlaka kadhaa kuja na sheria zake .
Kama kweli tunatakq kuuza proceed maize , swala linatakiwa lianze na kum support mkulima anapopambana kueweka mazao shambani.
 
Kupitia kwa WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeshatoa sh. bilioni 15 kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ili kununua mahindi kutoka kwa wakulima.

“Uzalishaji wa mahindi ni mkubwa lakini na sisi pia tumeimarisha hifadhi yetu ya Taifa ya chakula. NFRA tumeipa fedha za kwenda kununua mahindi kwa bei ya kumwezesha mkulima ili ajikimu hadi msimu ujao. Uwezo si mkubwa sana, lakini tumeipa shilingi bilioni 15,” amesema.
Hili swala serikali iachane nalo na kama lina ulazima wanunue kwa ajili ya hifadhi ya chakula tuu sio eti kuwa soko la wakulima.

Nimeona wakulima wanapiga a vikumbo malalamiko kibao kana kwamba Serikali ndio ikiwaambia walime mahindi itanunua au serikali ndio imeshusha bei za mahindi.
 
Ile neema ya Mbolea kupanda bei bado tunaikumbuka.Serikali iache kufanya mzaha na wakulima.
Serikali iliwaahidi wakulima kununua mahindi yao? Au iliwaambia walime mahindi?

Sioni logic hapo Kazi ya NRFA ni kununua chakula cha kukabiliana na janga la njaa na sio kufanya biashara.
 
Back
Top Bottom