Waziri Mkuu Khasim Majaliwa, baadhi ya wanaomjua, bila mamlaka ya kufokafoka kama aliyopewa na Magufuli, uongozi ni changamoto kwake. Sasa kwa awamu hii, ni mifumo ndio inatakiwa kuwa na nguvu, ndio maana Rais Samia anasuka mifumo ya haki jinai. Sasa mifumo ya haki jinai itapunguza nguvu ya wale wa "Kamata" "Weka ndani" "Peleka mahakamani".
Khasimu Majaliwa ni muumini wa mifumo iliyopo (status quo) kwa kuwa ilimbeba. Mifumo kandamizi ambayo ilimpa fursa ya kusema "Kamata huyu" "Fukuza huyu" "Peleka Mahakamani". Kimsingi, ni mifumo ambayo haifuati taratibu (due process) na ndiyo ilimfanya aonekane mchapa kazi. Nje ya mifumo hiyo, hamna kitu.
Mifumo ya ukusanyaji wa mapato, hakuiboresha kwa wakati wowote ule ili mapato yasivuje. Alichobakiza ni kuvizia taarifa za halmashauri, anaenda huko, anafoka, anakamata, basi, anaishia hapo, hakuna mchakato alioanzisha wa kuifumua na kuiboresha mifumo hiyo.
Alikuwa anastawi kisiasa mifumo ikiwa hivyo, kwa kuwa ilimpa nafasi ya kuonekana pale mifumo inapoonyesha udhaifu. Aliutunza udhaifu wa mifumo ili adumu (thrive) kisiasa.
Kwa ujumla, hakuna mabadiliko makubwa yoyote aliyosimamia wakati wa uongozi wake.
Udhaifu wake sasa unaonekana kwa sababu SSH anataka mifumo ifanye kazi, Majaliwa anakuwa anapwaya kwa aina hiyo ya uongozi.
Na ndivyo anavyoonakana kuwa hivyo sasa.
Rais Samia akizisuka Halmashauri na Idara za Serikali vizuri zaidi, ndivyo Kassim anavyozidi kupoteza relevance.