Kasuku kanionesha tabia halisi ya huyu Jamaa. Kumbe mnafiki sana

Kasuku kanionesha tabia halisi ya huyu Jamaa. Kumbe mnafiki sana

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Kuna kipindi nlitaka kufuga Kasuku Mimi nawapenda. But demu wangu wa kipindi hicho alinikataza kabisa. Akisema hawa ndege wana imani imani flani pia.

Tulikuwa tukibishana sana. Na anadai wangesababisha hata mimi na yeye tusioane. Hivyo hakutaka kabisa kusikia hizo habari. Kwa kipindi hicho sikutaka kumpoteza kwa sababu ya Kasuku.

Anyway .... Sikufuga na bado yeye sikumuoa. So nadhani haikuwa kigezo.

Ila leo nimegundua kuna watu wanafiq sana. Na wanaharibu hata imani za dini. Jamaa yangu huyu yeye yupo na mkewe na mtoto mdogo wa mwaka mmoja.

Nimekuja mtembelea. Nimekaa sebuleni kwake sasa nikamwita ili aje niondoke. Maana naona hiki kibaridi sijui kaenda kupasha moto msuli. Kamwita mkewe wameenda chumbani kisha kimya. Mimi huku walijisahau wakawa wamewasha TV hivi vipindi vyao tamthiliya za Kiswahili.

Binafsi ukitaka nikimbiza haraka nyumbani kwako niwekee hayo makitu. Basi nikaona muda umeenda. Nikajaribu piga simu inaita ipo hapa hapa mezani.

Basi nikaita baba xxxxxx. Nikaita tena.

Kasuku si akajibu " nakuja acha usengeh wewe" nikashtuka. Sina mazoea hayo na huyu jamaa. Kabisa. So nikaita tena. Akajibu tena "nakuja acha usengeh wewe" akaanza rudia rudia hayo maneno. Nikaamua kunyamaza.

Nimejifunza jamaa siyo swala tano wala nini. Mhuni tu na anatumia dini vibaya. Mi nlikuwa namheshimu sana lakini kitendo cha kumwambia Kasuku wake anitukane kimenifikirisha sana. Why lakini? Mimi nilimkosea nini? Je ningekaa tu sebuleni kumsubiri mtu anamla mkewe? Si heshima. Na ni yeye kaniomba nimpitishe kwake leo hakuwa na gari. Kaniambia nisubiri tutoke wote. Then naambulia matusi? Siyo haki. Nimeumia sana. Sijapenda kwa kweli
 
Mwanaume unamind vitu vidogo namna hiyo.

Inaonekana umekulia maisha ambayo hujajutana na changamoto za msingi mpaka vitu vidogo vikusumbue
Usipo mind vitu vidogo utashtuka umefanywa vikubwa. Mtu anaweza kukugusa tako. Ukaona si issue siku nyingine ata advance. In Every little action, there is reaction.
 
Sijaelew ina maana kwamba jamaa anafuga Kasuku au ?
Daaaah... Na hapo nimetumia kiswahili chepesi sana kama namwandikia mtu wa darasa la pili F. Mwambie mtu akueleweshe basi ndugu yangu Manyanza.
 
ukitafsiri sana kwa sisi tuliofanya bandarini hili wala sio tusi ila ni taadhari unapewa kuwa uache huenda kwa mazingira walionao unatakiwa uelewe nini kinafanyika na kisha ujiongeze kumwita mwanaume mwenzio tena kwa jina la baba fulani sio mwito sahihi kwa mwanaume ulitakiwa umwite jina lake.

Baba fulani wanaita wanawake mwanaume huwezi mwita mwanaume mwenzio baba fulani si kawaida yetu.
tena akiwa na mkewe chumbani!
 
ukitafsiri sana kwa sisi tuliofanya bandarini hili wala sio tusi ila ni taadhari unapewa kuwa uache huenda kwa mazingira walionao unatakiwa uelewe nini kinafanyika na kisha...
Ooooh.... Huwa naambiwa Makuli wana lugha zisizo za kistaarabu. Sawa Chawa nimekuelewa.
 
ukitafsiri sana kwa sisi tuliofanya bandarini hili wala sio tusi ila ni taadhari unapewa kuwa uache huenda kwa mazingira walionao unatakiwa uelewe...
Sisi wengine tumelelewa na wazazi wote wawili na maeneo ambayo huwezi sikia matusi. Ndo maana hata siyajui matusi.
 
Sisi wengine tumelelewa na wazazi wote wawili na maeneo ambayo huwezi sikia matusi. Ndo maana hata siyajui matusi.
una bahati kwanza kulelewa na wazazi wote wawili ila unatakiwa ujifunze kuwavumilia wengine pia kwakuwa binafsi naamini kila mtu unayekutana naye anachakwako na ni fursa kwako hivyo tunahitaji kuvumiliana na kupendana.
na tafsiri ya umependo ni kuvumilia kwa mapungufu ya wengine na kuwapenda tusiofanana nao.
 
Back
Top Bottom