Kasulu, Kigoma: Maduka yafungwa kumshinikiza Rais Samia awaondoe wafanyakazi wa TRA Wilayani

Kasulu, Kigoma: Maduka yafungwa kumshinikiza Rais Samia awaondoe wafanyakazi wa TRA Wilayani

Corticopontine

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2019
Posts
666
Reaction score
1,277
Wafanyabiashara Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma leo May 29, 2021, wameanza mgomo wakiwatuhumu baadhi ya Maafisa wa TRA kwa kuwabambikia kodi Wafanyabiashara wasiotoa rushwa kwao.

Kwenye mgomo huu Wafanyabishara hao wamesisitiza kwamba wanayo orodha ya majina ya Maofisa wote wabambikizaji na kuitaka Serikali kuingilia kati.

Tayari Mbunge wa Kasulu Mjini Prof. Joyce Ndalichako pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye wamefika Kasulu kufanya mkutano na Wafanyabiashara hao ili kuweka mambo sawa.
 
Hapana TRA wako sawa kabisa. Kodi haitaki lele mama. Tulipekodi kwa maendeleo ya Nchi yetu.
 
Mmeanza migomo? Au kwa sababu ni Samia? mlikuwa mnafungiwa account na hamgomi, acheni ubaguzi.
 
Shida kubwa ya Nchi za Afrika ni kiingiza siasa kwenye mambo ya utendaji
 
Wafanyabiashara Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma leo May 29, 2021, wameanza mgomo wakiwatuhumu baadhi ya Maafisa wa TRA kwa kuwabambikia kodi Wafanyabiashara wasiotoa rushwa kwao.

Kwenye mgomo huu Wafanyabishara hao wamesisitiza kwamba wanayo orodha ya majina ya Maofisa wote wabambikizaji na kuitaka Serikali kuingilia kati.

Tayari Mbunge wa Kasulu Mjini Prof. Joyce Ndalichako pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye wamefika Kasulu kufanya mkutano na Wafanyabiashara hao ili kuweka mambo sawa.
Hivi unawezaje toa rushwa ili ulipe kodi?? Mbona hii imekaa kimtego au wanasababu na MTU?? Mm ningekwenda Takukuru kwa Salum Hamduni ili washikwe hao wanaotaka rushwa.Sasa na kesho trafik mmoja akiomba rushes madereva tusiendeshe magari? Na inawezekanaje wore waliombwa rushwa kwani wanalipa kodi sawa au wanatofautiana kutegemeana na biashara ulivyoenda.Mtazamo wangu zipo taasisi husika wangetumia busara kutibu shida kuliko hiki maana hapa isije kuwa wanataka MTU afukuzwe ili mambo yaende vizuri.Us Haiti want sends Takukuru ili apatikane Hugo mla rushwa wanaomsema.
 
Ukistaajabu ya mifumo ya Serikali utayaona ya Kasulu!

Katika hali isiyotarajiwa mji wa Kasulu leo ulishuhudia wafanyabiashara wa maduka ya bidhaa mbalimbali wakifunga biashara zao kwa kile walichodai wafanyakazi wa mamlaka ya mapato Wilaya ya Kasulu wamezidi kuomba rushwa na kuwakadiria kodi zisizo rafiki na mitaji yao.

My take: Kwa kauli ya Samia ya kutaka kuwanyenyekea wafanyabiashara inaenda kuleta mgongano mkubwa na wa kihistoria katika nyanja hiyo.
 
Back
Top Bottom