Kasulu, Kigoma: Wajawazito wapanda kwa zamu kitandani kujifungua, wengine walazwa chini

Kasulu, Kigoma: Wajawazito wapanda kwa zamu kitandani kujifungua, wengine walazwa chini

Wajawazito katika Kata ya Kalela Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wanapeana zamu kupanda kitandani kujifungua na wengine kulazwa chini kutokana na Zahanati ya Kalela kuwa na chumba kimoja cha wodi ya wazazi chenye kitanda kimoja.

Chanzo: Nipashe

View attachment 1916490

View attachment 1916492
Komaeni si hamtaki tozo nyie? Na Hali hii ni kawaida sana Kanda ya Ziwa ambako watu wamerundikana hadi sio vizuri.

Japo hiyo ni zahanati imejitahidi kutoa huduma za kuzalisha wanawake.
 
Ilisikika Sauti ya mwanaume mmoja pale Dodoma akijinasibu eti 'serikali imeanza kufanya malipo ya ndege mpya Tano, ikiwemo ya mizigo na nyingine za abiria"

Mkuu, Sky Eclat , hayo ndiyo matumizi ya Kodi ya jasho lako!
Ndege wananunua ni bata mizinga wasioweza hata kutaga licha ya kupaa.
 
Ukiona Rais wetu anavyozunguka na Airbus, unaweza kudhani Tanzania haina matatizo madogo kama hayo.
Ni matatizo madogo eti? Acha ujinga wewe lipa tozo serikali ikomeshe huo umaskini.

Nilidhani yule ambae alikuwa hapandi Airbus alimaliza hayo matatizo 😁😁😁.

Ni hivi kujenga majengo ya awali ya zahanati ni mil.350,000 na kuweka Vifaa na dawa na wataalamu sio chini ya mil.700,000 kwa Zahanati.

Ndio maana Mwendazake alijenga majengo lakini hadi anakufa hospital na vituo vya afya havijaanza kufanya Kazi,yanahitajika mabilioni Ili huduma zianze kutolewa ipasavyo.
 
Ndege wananunua ni bata mizinga wasioweza hata kutaga licha ya kupaa.
Basi Hamna namna, acha watoto wasomee chini ya miti, akina Mama wajifungue kwa zamu kitanda kimoja zahanat nzima, Tozo ziendelee, na midege inunuliwe ya kutosha!

Ndege hoyeee!!
Ilisikika Sauti ya kiongozi mmoja aliyependa ndege kuliko chochote!
 
Nchi yetu hali ngumu sana ya uchumi ila watu wanavyotafuna hela kama hawana akili vizuri
Kuna mikoa na mikoa. Kuna sehemu za mikoa ya Kigoma, Tabora, Rukwa na Katavi. Kama umezaliwa na kukulia huku DAR, Moro, Kili na Arusha huwezi kuamini kwamba Ni Tanzania.
Nilifika sehemu kule Rukwa nyumba haina hata kibatari. Lkn stoo kumejaa mahindi na kila sampuli ya maharage.
 
Basi Hamna namna, acha watoto wasomee chini ya miti, akina Mama wajifungue kwa zamu kitanda kimoja zahanat nzima, Tozo ziendelee, na midege inunuliwe ya kutosha!

Ndege hoyeee!!
Ilisikika Sauti ya kiongozi mmoja aliyependa ndege kuliko chochote!
Pesa ya kujenga mataa na uwanja wa ndege wa Chato zingeweza kujenga vituo vingi tu vya afya.
The fifth phase gov was good at MISALLOCATION OF NATIONAL RESOURCES.
 
Kuna mikoa na mikoa. Kuna sehemu za mikoa ya Kigoma, Tabora, Rukwa na Katavi. Kama umezaliwa na kukulia huku DAR, Moro, Kili na Arusha huwezi kuamini kwamba Ni Tanzania.
Nilifika sehemu kule Rukwa nyumba haina hata kibatari. Lkn stoo kumejaa mahindi na kila sampuli ya maharage.
Viongozi wetu wanaturudisha nyuma sana kwenye maendeleo pesa hazitumiki ipasavyo.
 
Viongozi wetu wanaturudisha nyuma sana kwenye maendeleo pesa hazitumiki ipasavyo.

Wamegundua watanzania wanachohitaji ni maendeleo ya kuona kwa macho tu: mabarabara, madaraja, maflyover, reli, meli, madege, majengo, n.k. Pesa/gharama zinazotumika ni siri yao. Wananchi hawana shida na hilo; wanajua hela yao inatumika vyema!
 
Wamepandisha mafuta bei juu sijui Tozo lakini hakuna kitu tutaanza kuziona V 8 toleo jipya barabarani kigoma ni moja ya mikoa iliyosahaulika kabisa kwenye maendeleo...
 
Wamegundua watanzania wanachohitaji ni maendeleo ya kuona kwa macho tu: mabarabara, madaraja, maflyover, reli, meli, madege, majengo, n.k. Pesa/gharama zinazotumika ni siri yao. Wananchi hawana shida na hilo; wanajua hela yao inatumika vyema!
Ujinga wa mwafrika yule Bwana alijaza chumba manoti yetu akidhani ataishi milele kafa kayaacha kaondoka bila hata kumi.
 
Na hicho kitanda wakiibe pia ili wajifungulie chini kabisa. Unaijua vieite wewe!?
 
Back
Top Bottom