Kasumba ya gari ni Toyota naona sasa Tanzania imeanza kuisha

Hapo ndio wanasema jikune mkono unapofikia.
Ukijidai MO au Bakhresa maumivu yake ni makubwa ha ha ha
 
Toyota Stout (Dume) kaitafute moshi!b kule migombani zipo za kutosha!! Na Rombo kule walikuwa wakizitumia kuingiza bia za magendo kutoka kenya miaka hiyo,ila baada ya biashara hiiyo kufa waliyapaki juu ya mawe,Kullaya &family walikuwa nayo si chini ya saba!! Kila mtoto wa kiume alimilikishwa lake akaletee guiness!akija mtoto wa dada nae anapewa lake!!
 
Stout ni dume la mapickup yote. Niliwahi kufanya kazi za kimafunzo (trainee) pale Toyota City-Nagoya, jamaa wanajua kusulubu gari kabla hawajaamua kuliingiza sokoni. Suspension, Geabox, differentials, ball joints, na engine zinazusulubiwa kweli kweli ndipo waseme sasa twuzipele sokoni. wenyewe wnakuambia kuwa Stout ndiyo iliyokuwa kipimo chao, kwani ile ilisuluiwa sana, na hivyo kuiweka kama benchamark hata baada ya kuistaafisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…