Kata moja ya Tambani Mbagala Mbande wafadhili wamejenga misikiti 36 na bado wanajenga mingine, ila hawajajenga kiwanda hata kimoja

Kata moja ya Tambani Mbagala Mbande wafadhili wamejenga misikiti 36 na bado wanajenga mingine, ila hawajajenga kiwanda hata kimoja

Wana chuki tu kama india wamevunja mskiti wamejenga jengo la kuabudia wahindu
Sasa unauliza hoja kuabudu ama hoja kuabudu waislam?
Kila kitu kiwe kwa kiasi, kama walikuwa wanataka kuwasaidia, basi wajitolee ata kuwajengea nyumba za maana
 
sie tuitwae na kuigeuza maghala ya kuhifadhia mazao ya mashambani, nani ataenda kuswali huko? Kuna siku inakuja hiyo misikiti itabaki magofu hakutakuwa na wa kusali watu wamebadilika hawataki tena imani za kimagumashi haziwapi chakula
Kuna misikiti Mingi barabara ya kuanzia Chalinze Hadi Morogoro imeota Hadi majani na vichaka wanaishi nyoka na panya Haina waumini watu walikula pesa za wafadhili wakaijenga wakaingia mitini Haina waumini hata mmoja
 
Viwanda Atajenga Babako,bado Misikiti Haitoshi Inatakiwa Iwe Mingi Zaidi Ili Hata Kama Tuko Kazini Tusitembee Umbal Mrefu
 
Wakiendekeza ibada uzalishaji unakuwa sifuri; ni nani aliishi kwa kula ibada?
mimi Naishi Kwa Kula Ibada Simply Ibada Kwa Mujibu Wa Uislamu Ni Kitu Chochote Kinachompendeza Mungu Hata Kazi Halal Ni Ibada.Kama Unaongelea Kuswal Bas Kuswal Msikitin Hakumalizi Hata Dakika 10 Tunatoka.Kama Kuswal Ni Umaskin Bas Waislamu Weng Wangekuwa Maskini Lakini Ni Vice Versa Hata Kwenye List Ya Matajir Tanzania Waislamu Ndo Wanaongoza Kariakoo,mnazi,oysterbay Kumejaa Matajiri Wengi Waislamu Na Wanaswal
 
habari wadau.

Utafiti wangu binafsi katika Kata moja inayoitwa TAMBANI iliyopo Mbagala Mbande kuna misikiti 36 ambayo imejengwa na wafadhili taasisi za kiislamu za wa Arabu na bado inaendelea kujengwa mingine.

kinachonishangaza kwa nini Wafadhili hao hawajajenga shule hata moja waislamu wasome vizuri wazalishe Ma engineer, Madaktari na wataalamu wa fani mbali mbali,

kinachonishangaza pia kwa nini wafadhili hao hawajajenga kiwanda hata kimoja ili waislamu ama raia wa TAMBANI wapate ajira waache kushinda vijiweni bila kazi waondokane na umaskini

KWA NINI MSAADA UWE KUONGEZA NYUMBA ZA IBADA TU ?

najiuliza wafadhili hao kwa nini wasijenge hata chuo cha ufundi ama cha teknolojia hata kimoja ili watu wa TAMBANI wapate mafunzo ya kitaalamu wajikomboe kiuchumi ?

kujenga misikiti sio jambo baya , ni jambo zuri kufadhili kuwajengea wananchi sehemu za kuabudia. ila nimeshangaa sana why msaada uwe kujenga misikiti tu na kuchimba visima vya kutawazia.

Tunapaswa tuwaambie wafadhili adui wetu mkubwa ni Ujinga, Maradhi na Umaskini. Vitu vya kupambana ma hawa maadui watatu ndio wanapaswa kutujengea kwa wingi.

Kutujengea Shule, zahanati na viwanda ndio ufadhili wa kweli.

Kiwanda kimoja kinafuta umaskini wa watu wengi.. kuliko kujenga nyumba za ibada kila mtaa huku waumini wanazo sehemu za kusali tayari
Nyie 🌈 mumejenga viwanda vingapi?
 
Kila kitu kiwe kwa kiasi, kama walikuwa wanataka kuwasaidia, basi wajitolee ata kuwajengea nyumba za maana
Wewe umejuaje kama hio walofanya sio kwa kiasi
Au kuna kiasi maalum cha kujenga misikiti ama kusaidia kilichoekwa na sirikali?
Pia mtu anatoa msaada ama anasaidia kwa anachoona kinafaa unatakaje ajenge nyumba wakati yeye kaona ajenge kanisa ama barabara au msikiti
USAID si wanajenga hapa mpaka vyoo tena wanaeka na masharti ya kijinga jinga
 
Hakuna sehemu waaarabu wanaibiwa na waswahili matapeli waislamu kama kwenye ujenzi wa misikiti

Mwarabu tajiri yeyote ukisema unaomba Hela ya ujenzi wa msikiti au madrasa anakuona wewe ndie mwislamu Bora mno anatoa Pesa chapchap

Waswahili wanswapiga kwenye kuanzia gharama za ununuzi wa kiwanja Hadi ujenzi.Msikiti utajengwa ila hizo gharama zake utakaa Chini.Na Kwa kuwa waarabu Wana Pesa nyingi wanachojali madrasa au msikiti umejengwa basi
Naunga mkono hoja.

Kuna mwamba fulani lake zone alijikuta anakuwa tajiri wa kutupwa ghafla tu kwa mchongo huo. Full kuoa na kugawa noti kitaa kama ana kiwanda cha kuzifyatua, Hadi pale mwamba mwendazake alipomminya ndo akastopisha ugawaji hela na kuingia kwenye siasa akawa diwani (sijui jiwe alimminyaje, maana tangu pale hagawi hata mia!)
Jamaa alikuwa akijenga msikiti kwa maximum ya milioni 30 halafu kwa mwarabu kavuta milioni 150! Ma kajenga misikiti mingi mno ukanda huo. Sijui kama huo mchongo ulishakata ama bado anaendelea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakiendekeza ibada uzalishaji unakuwa sifuri; ni nani aliishi kwa kula ibada?
Sijui kwa dini nyengine ila kwa waislam hata kufanya kazi pia ni ibada
Nandio maana hata kwenye qur an tunasisitizwa baada ya kumaliza sala tutawanyike kufanya shughuli nyengine ikiwemo ibada ya kufanya kazi
Kwa lugha nyepesi uzalishaji pia ni ibada kwenye uislam hapa napo unasemaje
 
Hiyo ni jamii ya kiislamu. Hitaji lao ni ahera (kama ipo anyway). Elimu dunia is not a priority to them. Pwani yote priority ni madrasa n misikiti. Tuwaache wapiganie ahera ambayo hawana uhakika usiokuwa na mashaka kama ipo! (mnisamehe najua mtanirukia.
Ahera ina uhakika.....
Wale wa kuishi duniani milele furahieni ya dunia.
Wanaoitaka ahera waachwe....
 
Sijui kwa dini nyengine ila kwa waislam hata kufanya kazi pia ni ibada
Nandio maana hata kwenye qur an tunasisitizwa baada ya kumaliza sala tutawanyike kufanya shughuli nyengine ikiwemo ibada ya kufanya kazi
Kwa lugha nyepesi uzalishaji pia ni ibada kwenye uislam hapa napo unasemaje
Hao jamaa wanaojengewa hizo nyumba za ibada wana viwanda vingapi?
 
Wewe umejuaje kama hio walofanya sio kwa kiasi
Au kuna kiasi maalum cha kujenga misikiti ama kusaidia kilichoekwa na sirikali?
Pia mtu anatoa msaada ama anasaidia kwa anachoona kinafaa unatakaje ajenge nyumba wakati yeye kaona ajenge kanisa ama barabara au msikiti
USAID si wanajenga hapa mpaka vyoo tena wanaeka na masharti ya kijinga jinga
Wajenge viwanda watu wapate ajira, na sio kuwajengea majengo ili kuwamezesha mawazo ya kusadikika
 
habari wadau.

Utafiti wangu binafsi katika Kata moja inayoitwa TAMBANI iliyopo Mbagala Mbande kuna misikiti 36 ambayo imejengwa na wafadhili taasisi za kiislamu za wa Arabu na bado inaendelea kujengwa mingine.

kinachonishangaza kwa nini Wafadhili hao hawajajenga shule hata moja waislamu wasome vizuri wazalishe Ma engineer, Madaktari na wataalamu wa fani mbali mbali,

kinachonishangaza pia kwa nini wafadhili hao hawajajenga kiwanda hata kimoja ili waislamu ama raia wa TAMBANI wapate ajira waache kushinda vijiweni bila kazi waondokane na umaskini

KWA NINI MSAADA UWE KUONGEZA NYUMBA ZA IBADA TU ?

najiuliza wafadhili hao kwa nini wasijenge hata chuo cha ufundi ama cha teknolojia hata kimoja ili watu wa TAMBANI wapate mafunzo ya kitaalamu wajikomboe kiuchumi ?

kujenga misikiti sio jambo baya , ni jambo zuri kufadhili kuwajengea wananchi sehemu za kuabudia. ila nimeshangaa sana why msaada uwe kujenga misikiti tu na kuchimba visima vya kutawazia.

Tunapaswa tuwaambie wafadhili adui wetu mkubwa ni Ujinga, Maradhi na Umaskini. Vitu vya kupambana ma hawa maadui watatu ndio wanapaswa kutujengea kwa wingi.

Kutujengea Shule, zahanati na viwanda ndio ufadhili wa kweli.

Kiwanda kimoja kinafuta umaskini wa watu wengi.. kuliko kujenga nyumba za ibada kila mtaa huku waumini wanazo sehemu za kusali tayari
Baadhi ya wanafunzi waliotakiwa kujiunga na kidato cha kwanza katika maeneo mbalimbali ya Kanda ya Ziwa wamegoma kuripoti shuleni kwa kigezo kuwa wenzao waliomaliza kidato cha nne, sita na chuo kikuu wapo mitaani bila ajira.

Wanafunzi hao wamesema hali hiyo imewakatisha tamaa ya kuendelea na masomo ya sekondari badala yake kuamua kutafuta shughuli nyingine za kiuchumi ikiwemo mafunzo ya ufundi.

Kwa mujibu wa gazeti la Nipashe, mmoja wa wazazi wa watoto ambao hawajaripoti shuleni, mkazi wa Kata ya Turwa wilayani Tarime mkoani Mara, Elizabeth Charles amesema binti yake alikataa kuandikishwa na kutaka apelekwe chuo cha ufundi cherehani kutokana na wahitimu wengi kuwa mitaani bila kazi maalum.

Source: Jamii forum
 
Wajenge viwanda watu wapate ajira, na sio kuwajengea majengo ili kuwamezesha mawazo ya kusadikika
Mawazo ya kusadikika kwako ila kwao mawazo halisi
Mawazo ya kusadikika yanajengwa na wanasiasa
Kwani jukumu la kuwajengea viwanda raia husika nila wafadhili ama la sirikali? 🤔
 
Dini ni kifubaza fikra
Siku Moja nikiwa na mshikaji mmoja huko mbande nikawa namsindikiza mshikaji anatafuta nyumba ya kupanga no dalali chaka to chaka....

Tukafika nyumba Moja tukakuta wazee wa makamo mume na mke tukasalimia tukaeleza shida yule bibi akasema nyumba tumepata AKAULIZA DINI TUKAJIBU WAISLAMU AKATUAMBIA TUNGEKUA WAKRISTO ASINGE TUPANGISHA MAANA TUTAPIGA KWAYA KWENYE NYUMBA YAKE😄😄😅😅🤣🤣😂😂😂

Uswahili, Umaskini na uislamu ni Tatizo hapa ulimwenguni

Hayo mambo nilikuaga nayaona kwenye maigizo ya kaole sanaa group 😅😅😅🤣🤣😂

Job true true cc. Mjanja M1
 
Hao jamaa wanaojengewa hizo nyumba za ibada wana viwanda vingapi?
Viwanda kazi ya sirikali sio ya hao wajenga miskiti
Kwani idadi ya miskiti hio ni billion ngapi na inajenga viwanda vingapi kwapamoja?
Mwisho utakula wafadhili zaidi ya watano wamejenga hizo nyumba za ibada
 
Pesa ni zako [emoji38][emoji38][emoji38]? Jenga wewe mweny elimu ...Elimu ya mkoloni mpaka leo watu ni maprofessor hawajui hata kubuni viwanda wamebaki siasa tu.

Kuchangisha watu kujeng shule ambazo faida wanakula wao..kununua magari ya bei mbaya huku watoa sadaka wanatoa pesa kupata huduma ...

Serikali haina dini itajenga hii sio nchi ya kiislamu.
Elimu nj ya mkoloni ,dini ni ya mkoloni ,una hagua kipi,ukiumwa unaenda msikitoni au hospitalini
 
Back
Top Bottom