KERO Kata ya Kibata wilaya ya Kilwa ina miundombinu ya barabara mibaya na kupelekea maisha kuwa magumu

KERO Kata ya Kibata wilaya ya Kilwa ina miundombinu ya barabara mibaya na kupelekea maisha kuwa magumu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Charles Xavery

New Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
1
Reaction score
0
UGUMU WA MAWASILIANO YA BARABARA NA MADARAJA NDANI KATA YA KIBATA WILAYA YA KILWA NI WA KUTISHA.

Kibata ni miongoni mwa kata 23 ndani ya Wilaya ya Kilwa. Kata hii Ina vijiji vinne. Kata hii Ina jumla ya shule nane(msingi 7 na Sekondari 1). Vilevile ni kata yenye dispensary 4 sawa na vijiji vyake.

Tatizo kubwa la kata hii ni MIUNDOMBINU ya BARABARA NA MADARAJA ambayo inayafanya maisha ya Watumishi na wanajamii kuwa ngumu sana.

Kinachowauma Watumishi na wanajamii ni kuona maisha ya wilaya jirani(Rufiji) na kata zake wakiwa na maisha Mazuri ya kimiundombinu wakati Tanzania ni nchi moja.

Wengi wa Watumishi wanashindwa hata kukaa kwa muda mrefu kutokana na hali hiyo ya kutisha ukilinganisha nyakati za Sayansi na Teknolojia tulizo nazo Sasa.

Tatizo la ubovu huu wa MIUNDOMBINU limesababisha mitihani ya Taifa 2024 darasa la nne,Saba, kidato Cha pili na kidato Cha nne kusambazwa kwa Pikipiki.

Hivyo wananchi na Watumishi wanaotoa huduma katika kata hii wanaomba wapewe upendeleo wa pekee ili kuondoa tatizo hili ili nao waweze kufanana na Watu wengine waishio nchi hii.
 
Back
Top Bottom