KERO Kata ya Kijombe (Njombe) bado uhaba wa Maji ni tatizo kubwa, Mamlaka ya WANGIWASA fanyieni kazi hii

KERO Kata ya Kijombe (Njombe) bado uhaba wa Maji ni tatizo kubwa, Mamlaka ya WANGIWASA fanyieni kazi hii

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mwanongwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2023
Posts
611
Reaction score
567
Licha ya sisi Wananchi kulalamika kila mara lakini ni kama Mamlaka zinazohusika zimeziba masikio, kwa kuwa haitusikii, wanatatuaje kilio chetu.

Kwenye kata yetu ya Kijombe, Wilaya ya Wanging'ombe hapa Njombe uhaba wa maji ni kilio kikubwa kwa baadhi ya Wananchi hali inayosababisha kutumia maji ya kwenye madimbwi.

Mamlaka ya Maji Wanging'ombe (WANGIWASA) wameweka mgao usiyokuwa na maana, kwenye kila Kijiji maji ya Bomba yanatoka mara mbili kwa mwezi.

Hii ni hatari sana kwa Watoto wa Sekondari ya Kijombe ambao wanalazimika kwenda kutafuta maji kwenye maeneo hatarishi.

Hapa wakipatwa na majanga mbalimbali lawama itakuwa kwa nani? Maana Kwa shida hizi wanazozipitia ni balaa, Mamlaka za Maji zitusaidie hali hii siyo nzuri na inaweza kuchangia kuibuka kwa magonjwa ya tumbo.

DSC_0829.JPG

DSC_0826 222.JPG

Pia soma ~ Wakazi wa Kijombe, Wilaya ya Wanging'ombe (Njombe), kwenye huduma ya maji tunaisikia kwenye bomba
 
Back
Top Bottom