Kataa kabisa urafiki au mahusiano ya kawaida na Askari Polisi

ila ninyi polisi mmezidi
Usifundishe watu kuwa na chuki kama ulonayo.
Hata kwa mwenyezi Mungu utahesabiwa kwa kauli zako.
ni hayo tu we kubali ama kataa ila jua haya maandishi yatakutafuna.
Huwezi ishi kwa amani na furaha kwa chuki kama hizi upandazo.
Naamini we ni mtoto hakuna mtu mzima mwenye akili au mitizamo ya namna hii
 
Reactions: Tui
ila ninyi polisi mmezidi
Hakuna kitu kibaya kama kupanda chuki kwa watu.
Usiwe kama mwanamke aliyeachana na Mume wake akapanda chuki kwa watoto wake hasa wa kike na kuanza kuwaambia bint zake kuwa wanaume si watu ni MBWA na kuwasihi wasiolewe na kuwaambia endapo mtu akiolewa hana radhi nae
Ishi
ishi sahihi
kuwa chanya
epuka chuki za mwanamke aliyepewa talaka
 
Reactions: Tui
Uko sahihi lakini utekelezaji wa majukumu yao umegubikwa na matukio mengi ya uonevu na mauji, cha msingi polisi mweke mbali katika cycle yako ya maisha, kutana nae pale inapojitajika kufanya hivyo, baada ya hapo jikatae, hawafai

Sasa ndugu askari polisi, naomba usihemkwe sana, uzi huu utadumu milele na mpaka hapa ni wazi uzi huu umekushika pabaya Afande uchira, uzi huu hauna lengo la kueneza chuki dhidi yenu, lengo kuu nikuwaokoa wananchi kutoka katika hatari ya kuwa wahanga wa mikono yenu iliyajaa umauti, unafiki, uonevu na ulimbukeni, watu wanapoamua kujiweka mbali na aina fulani ya watu katika jamii, haipaswi kutafasiriwa kama chuki, bali ni maamuzi ya kupeana uhuru katika harakati za kimaisha, nyie hamfai kuwa rafiki zetu sisi raia, tutaongea na nyie ikiwa inahitajika kufanya hivyo. Mko wengi nyie polisi na pia mnahadi nyumba zenu hivyo KUWENI na umoja wenu na urafiki wenu, sisi raia hatutaki urafiki na nyie, timizeni majukumu yenu pasipo kutuomba pesa za bia.
 
Lkn wako Polisi wema pia.Samaki mmoja akioza chukua aliyeoza mtupe baki na walio safi.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
We jamaa unawajua sana polisi! Halafu ukishawapa hela wanaanza kujifanya washikaji.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Members who reacted to message #1

All (60) Thanks (52) Kicheko (5) Nzuri (2) Mshangao (1)​

 
Tuishinao kwa akili.Sema hawa ndugu zetu wanatanguliza shida zao binafsi sana.Niliishapata tatizo pale polisi kituo cha Mlimani (UDSM)...miaka ya nyuma sana...wakati suala letu linaendelea na nikawa nareport kila wiki- mara naanza kuona simu kutoka kwa askari upelelezi...mara nina-shida, mara nisaidie ndugu yangu, mara hivi...na wakati huo anasahau aliishaniweka ndani.....Na alijua kabisa ulikuwa ni mchongo tu...na uonevu wa waziwazi...
Huyu afande ngoja leo nimtafute..maana kipindi kile alisema anajiandaa kustaaf lkn mambo bado hayajaeleweka..
 
Yaani umpige ocd? Labda ocd wa mchongo.
Ogopa sana hao jamaa kukuua na kusingiziwa kuwa wewe ni jambazi hawaoni shida
 

Urafiki na polisi ni kama mkongojo wa muwa. Ukiwa na njaa huo mkongojo lazima uutafune tu.
Hata nchi zilizoendelea kama Marekani, raia hawataki mazoea kabisa na mapolisi.

Hao jamaa wameshajitenga na jamii na huwa wanajiona wao ni wa maana zaidi kuliko raia wa kawaida. Ni ufinyu wa kufikiri tu. Wakishastaafu ndo huwa wanaanza kujisogeza karibu na jamii.
 
Siku ukija kupatwa na tatizo ndipo utaona umuhimu hata wa kufahamiana na polisi

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app

Kwahiyo huduma za kiusalama zinatolewa kwa kufahamiana? Nilidhani ni uzalendo na wajibu.

Unataka kuwaambia nini wageni wanaotoka nchi nyingine na kufika Tanzania ambapo hawamfahamu mtu hata mmoja? Kwamba hawatapata msaada wa polisi wakikutwa na tatizo just because hawafahamiani na polisi?

Kauli zenu ndo zinajenga uozo kwenye hizi taasisi
 
#POLISI SIO RAFIKI, POLISI SIO NDUGU, MKATAE POLISI
Nakubaliana na wewe kabisa! Tunacheka nao tu lakini siyo wenzetu! Tangu classmate wangu anivuruge ushahidi wa kesi ya mauaji ya dadangu sina hamu nao kabisa! Ila naona kama Tecklove anajipitishapitisha karibu na mimi sijui nimgonge?
 
Hakuna kitu kama hiki, OCD ni big fishes halafu ni watu ambao wanalinda sana status zao hawezi kuingia kwenye mzozo wowote na raia na hata ikitokea hivyo basi watatumwa vijana wake wakushughulikie. Ocd hashikani mashati hata iwe baa vijana wake watakunyoosha na hutarusha hata maneno achilia mbal utosi kama unavosema. Pia OCS Hana power yoyote kwenye uwepo wa OCD. Ni mtawala wa shughuli zote za kituo ila OCD akisema ktu flan hapana OCS hatii neno mana ni boss wake
 
Mwana amepigwa mkono na OCD nae hakukubali ikabidi amvamie Vurugu likatokea pana polisi wengine pale ikabidi waamue ugomvi na wale polisi walioamua ugomvi hawakumpiga mwana. Kwa mazingira kama yale OCD hakutegemea kama mwana angemvamia na kumuigia mwilini.
Znz ni tofaut na bara mkuu OCD sio big fish ni wa kawaida tu.
Jambo jengine Znz kuna uamii sana walio weng san wana backup za wakubwa uko kwenye jesh la polisi.
Kuna OCD mmoja alishawah kunambia ukitaka uwapate waznz ukimkamata tu malizana nae apo apo ukimweka ndan t baada ya nusuu utakuta cm inanigia kutok kwa mkubw wako uko juu umuschie kijana.
Mtu ana mjomba wake ni CP unadhan atakua muoga kwa polisi kama me na ww?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…