Kataa kabisa urafiki au mahusiano ya kawaida na Askari Polisi

Kataa kabisa urafiki au mahusiano ya kawaida na Askari Polisi

Polisi wa vyeo vya chini wengi wanazengua ila wakubwa wao hawana shida kivile.

Kuanzia nyota tatu kupanda juu ni nadra sana kukuta wenye tabia ambazo sio za kiproffessional.
Kwasababu ni wachache pia na hawakutani na raia moja kwa moja
 
Tumetoka kwenye KATAA NDOA sasa ni KATAA POLISI.

Ila polisi sijui wana nini. Yani hata akiwa ndugu yako akajua una issue/jam flani inayoweza kukuletea kwikwi badala ya kuongea na wewe uache yeye atakulengeshea manjagu wenzake wakutoe mpunga halafu yeye huko chemba anaenda kupewa gawio.
yaani ni wa hovyo hovyo tu... KATAA POLICE
 
Mtendaji wa kijiji na polisi tofauti yao ni Bunduki na mayunifomu basi!! Woote masinichi, njaa kali, shule ndogo, ubabe wa kujiami, wapumbafu, wajinga afu mbaya zaidi wanajikomba CCM utadhani kuna kitu wanawekewa hukoooo mnapopajua
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ni juzi tu kuna mwana ni derev bajaj alikamatwa na ocd kufik kituon ktk majibizano yule ocd alimpiga kibao mwana mpak alipat maruerue ila uzur mwana hakua mnyonge dlimrukia ocd na kupiga utosi na kuanguka nae chini kuna polisi wengin wanaingilia kati kuamua ugomv ocd amepanic anatak mwana apelekwe mahakaman mkuu wa kituo akaingilia kati na kumlaumu ocd kwa kujichukulia sheria mkononi.
Kuanzia mda ule heshima ilipatikan kwa kila mmoja kumuheshim mwenzake.
moral ni kwamba hupaswi kuwa mnyonge na kuogopa polisi ata kama ana chego gani.


Hatari sana hii, kama mkuu wa kituo asingekuwepo na kuna SMG karibu, dogo angeuwawa, IQ za police ni ndogo sana, usitafute heshima kwao, kaa mbali nao kabisa, na ukiingia kwenye 18 zao kuwa mpole uondoke ukiwa hai. Tuishi,

Cha muhimu:

  • Kaa mbali na police, hata kama ni ndugu.
  • Tupige sala kila siku asubuhi Mungu aongoze njia zetu.
  • Ukiingia kwenye 18 zao kuwa mpole, negotiate.
 
Ila sisi tukikabwa tunawakimbilia polisi wakati mwingine ukimpigia tu mkuu wa kituo simu kua nasikia huku kwangu siyo SHWARI defender hii napo nisiwe nao karibu bado sijashawishika mtaani kwetu bila polisi hatulali
kuwa nao tu karibu siku moja utashawishika utamuelewa tu mtoa mada
 
Ninachojua mimi polisi ni sehemu ya jamii. Ni kweli Kuna polisi ni wasumbufu kupita kiasi. Kiuhalisia hao wanaenda kinyume na kanuni za utumishi wa umma. Lakini pia kuna polisi ni wastaalabu na wana utu hata zaidi ya baadhi ya raia wenzetu.

Nakumbuka mwaka juzi mwzi wa 7 Kuna askari polisi walikuja kwangu kwa lengo la kupekuwa. Kwa maelezo kwamba nauza dawa za kulevya aina ya bangi. Mimi kwa kujiamini 100% kwamba sifanyi biashara hiyo niliwaruhusu askari hao wapekuwe. Walimwita kiongozi wa mtaa wakapekua ndani ya nyumba hawakupata kitu chochote.

Kijana mmoja ambae walikuja nae ambae badaae niligundua kuwa alikuwa ndiye mtoa taarifa kwa hao askari aliwambia hao askari kwamba afande hatujapekua kwenye ile stendi ya tenki la maji lililopo nyuma ya nyumba. Askari hao tuliongozana nao mpaka nyuma ya nyumba na chini ya stendi hiyo walitoa mfuko ambao waliufungua na ndani yake kulikuqa na bangi.

Sikuamini macho yangu kuona bangi ipo nyumbani kwangu tena ndani ya gate!! Kiongozi wao aliamuru form za upekuzi zikajazwa na mashahidi wawili ambao ni kiongozi wa mtaa na jilani yangu wakaaandikwa maelezo. Kisha afande huyo akasema ""ndugu endelea na shughuli zako kesho asubuhi uje kituoni" na akanipa namba yake ya cm

Kesho yake nilienda kituoni afande huyo akanihoji kwa kina na kuniuliza Nina ugomvi na nani nami nikamwambia. Kisha akaniambia kwa mazingira waliyoikuta hiyo bangi na jinsi ilivyowekwa ni wazi kwamba imewekwa na mbaya wangu. Hivyo niendelee na shughuli zangu wakinihitaji wataniita. Lakini sikuwahi kuitwa na askari hao. Lakini mbaya wangu nilimjua na malipo niliyomlipa kwa ubaya huo ni Mungu anajua

Lakini nikiwa wilaya ya Bunda mkoa wa Mara nilikutana na askari mmoja nadhani ni mtu wa arusha kwa cheo ni inspector. Askari huyo sintamsahau maishani. Ni mnyanyasaji wa kiwango cha kutisha nadhani halipwi mshahara kwa njaa aliyonayo. Hivyo ndiyo maana nasema polisi ni jamii na ndani ya jamii yao kuna polisi wema na wabaya
Well said mzee japo wengi ndo wabaya
 
Kuna demu mmoja mjeda (police) kanizimikia balaa, unataka kuniambiaje weye.!! alinikamata kosa la barabarani kutoka hapo yaani nataka kuoa kabisa kabisa maana si kwa mambo yale aisee !!
Unataka kuoa polisi?

Ushauri wangu usijaribu kuweka hata wazo la kuoa mwanajeshi, polisi wala trafiki mwanamke.
 
Habari Wanajukwaa!
Kwanza nikushukuru sana Mkuu kwa kuleta chapisho lenye hoja ndani yake; ni wazi kuwa kwa hatua iliyofikia Polisi sio tena ndugu wa wanajamii na hii kwa kiasi kikubwa imetokana na utendaji kazi wao mbovu sana pamoja na mienendo yao.
Polisi nawachukia sana ingawa nina kidemu changu kimoja ni FFU sijui nifanyeje tu Mkuu labda Mshana Jr unisaidie mawazo 😀
 
Back
Top Bottom