Hii vita siku mkiimaliza mtuambie. Kuna jamaa yangu ka umri kalienda kidogo, maneno yakawa mengi sana. Mwaka jana akapata kazi TRA, hivi ninavyoandika nafuatilia mbuzi kwa ajili ya ka sherehe ka engagement yake na soon ni ndoa.
Msichokijua wengi ni kwamba maisha yamebadirika sana, kama ulibahatika kuzaliwa kwenye chochote kuna wenzio wanajitafuta ili wapate chochote ndio waoe lengo ni kutoitesa familia.
Kijana mwenye akili timamu hawezi kuoa eti mke huja na riziki zake huo ni ukuda sana. Acha nifuatilie mbuzi kijana afanye yake, mnawasema watu hadi wanakosa raha. Kwenye vifua vya vijana wengi kuna maumivu ya kusemwa juu ya haya mambo na chanzo ni uchumi mbovu wa vijana wengi