Kataa Ndoa School of Thought, ni upi mtazamo wenu juu ya Masuala haya?

Kataa Ndoa School of Thought, ni upi mtazamo wenu juu ya Masuala haya?

Mtoto yeyeto aliyelelewa na single parent kisaikolojia hawezi kuwa sawa na aliyelelewa na co parent hata kwenye mahusiano wanashindwa kubalance.
Usiingie ndoa na asiyelelewa na both parents labda kama wewe ni Yesu.
Wengi wanatabia ngumu.
 
Huwezi zaa watoto wote timamu lazima wehu wawepo, lakini Stable family humbeba huyo mwehu sababu ya upendo na umoja wa kifamilia.

Lakini, wengi hapa naona wanachanganya, Family & Marriage kama ulivyo mfumo wowote, its not PERFECT, lakini it's the best we got.
Ila ukweli ni kwamba single parenting inaweza kutoa watu wazuri tu kwenye jamii

Kwa maana hiyo well behaved individuals sio lazima wawe matokeo ya familia ya wazazi wawili na bad behaved individuals pia sio lazima wawe matokeo ya single parenting
 
Nimegundua kataa ndoa wengi wamelelewa na single parent kwahiyo walisha haribiwa kisaikorojia toka wakiwa watoto ndio maana wanaona wako sahihi bila kujua uzuri wa kulelewa na wazazi wote wawili
Mkuu nimelelewa kwenye familia bora kabisa ya baba na mama tena familia iliyojaa utulivu na upendo , toka nakua mpaka najitambua sijawahi kushuhudia wazazi wangu wakizozana hata siku moja, in short nimetoka kwenye familia ambayo naweza kuiita the best.
Wakubwa zangu walionitangulia kuzaliwa wameoa na wengine wameolewa na wana familia zao safi kabisa ila mimi msimamo wangu ni huo NDOA NI UTAPELI na sitaoa. Na home wanalitambua kabisa hili
Nina watoto wawili mpaka sasa na wako safi kabisa
 
Mtoto yeyeto aliyelelewa na single parent kisaikolojia hawezi kuwa sawa na aliyelelewa na co parent hata kwenye mahusiano wanashindwa kubalance.
Usiingie ndoa na asiyelelewa na both parents labda kama wewe ni Yesu.
Wengi wanatabia ngumu.
Vipi watu wenye tabia ngumu kwenye ndoa na walilelewa na wazazi wote wawili?

Vipi watu ambao wamelelewa na wazazi wote wawili ila wanamatatizo ya kisaikolojia?
 
Ndoa ni nini?, ndoa ni mkataba wa kingono uliopewa nguvu na serikali na taasisi za kidini unaompa manufaa mwanamke na kumkandamiza mwanaume.
Hii ndio maana halisi ya ndoa na serikali dini na asasi(mashirika ya kimataifa) yamekuja kumdhoofisha mwanaume hapo na kumnyanyua zaidi mwanamke ilihali mpambanaji na anayehakikisha mambo yote yapo sawa katika familia ni mwanaume. LATAA NDOA NAIUNGA MKONO
KATAA NDOA NI UJAMBAZI
 
Ila ukweli ni kwamba single parenting inaweza kutoa watu wazuri tu kwenye jamii

Kwa maana hiyo well behaved individuals sio lazima wawe matokeo ya familia ya wazazi wawili na bad behaved individuals pia sio lazima wawe matokeo ya single parenting
Single Parent sio Chaguo bali ni Matokeo hasi ya mifumo ya Ndoa na Mahusiano kufail.

Wapo wanyama, wakishazaa watoto wanaachia wenzao mfano Kuku, Mbuni n.k sababu nature ndio imewadictate hivyo, lakini Kiumbe Mwanadamu, halelewi hivyo.
 
Vipi watu wenye tabia ngumu kwenye ndoa na walilelewa na wazazi wote wawili?

Vipi watu ambao wamelelewa na wazazi wote wawili ila wanamatatizo ya kisaikolojia?
Ndoa sio Perfect system but it's the best among others and suitable to mankind.
 
ajenda hii kataa ndoa iko nyuma ya makundi ya wanaume wafuatao.

wavulana chini ya miaka 20.
wavulana miaka 30 kuendelea ambao hawana ramani yoyote.
walioumizwa na mapenzi kupitiliza wamejikatia tamaa.
ambao wana matatizo ya kutopata uzao,wanatumia kete hiyo kuficha madhaifu yao.
mkorinto tuoneshe mke wa Yesu au Mtume Paulo aliyewaandikia nyie wakorinto waraka.
 
Hayo Yote Uliyoandika Kwenye Ndoa Za Sasa Hayupo Walifanikiwa Wazee Wetu Tu.

Swali Kwanini Hayo Uliyoandika Yamekuwa Nadharia Kwenye Ndoa Za Sasa?

Yes, kuna changamoto ya taasisi ya ndoa na hata kwa wazee wetu zilikuwepo, lakini ni exaggeration kusema kuwa yote hayafanyi kazi sasa.

Madhara ya usawa wa kijinsia, uliberali n.k kama ambavyo yameathiri mifumo mingi ya asili ya mwanadamu, ndoa is not immune. Ingawa bado situation could be (and would be) far worse bila ndoa, kuliko ndoa zikilindwa.
 
mkorinto tuoneshe mke wa Yesu au Mtume Paulo aliyewaandikia nyie wakorinto waraka.
Yesu hakuja kuoa wala kula kula masaa yote kama watu wengine.

paulo nayeye alikuwa muwazi kwamba kwa case ya kuingiliana basi kila mmoja wenu ajihalalishie mmoja atakayempenda,na watakaoamua kuishi walivyo kama SADAKA kwa Mungu basi ni heri zaidi.

sasa wewe unabaki single ili ufokoe watoto wa watu bila kikwazo,hutafanana na yeyote hapo juu.
 
Mkuu nimelelewa kwenye familia bora kabisa ya baba na mama tena familia iliyojaa utulivu na upendo , toka nakua mpaka najitambua sijawahi kushuhudia wazazi wangu wakizozana hata siku moja, in short nimetoka kwenye familia ambayo naweza kuiita the best.
Wakubwa zangu walionitangulia kuzaliwa wameoa na wengine wameolewa na wana familia zao safi kabisa ila mimi msimamo wangu ni huo NDOA NI UTAPELI na sitaoa. Na home wanalitambua kabisa hili
Nina watoto wawili mpaka sasa na wako safi kabisa
Hahahaha wewe una matatizo yako kwenye haso zako
 
Kwahiyo shida kwa vijana ni pesa
Kwa vijana wanaojitambua, shida ni uchumi. Vijana wengi sasa ivi wanajua kuwa maisha ya ndoa bila uchumi ni kuteseka na kuteseka sio maisha. Tafuta uchumi kwanza kama kijana wa kiume ukiona mwanga anzisha familia. Maisha sio yale wazee ya lwenda shamba mama na baba na watoto wakikua wanasaidia, sasa ivi kila kitu ni cash. Aloo vijana wanaogopa kuaibika
 
Kwahiyo shida kwa vijana ni pesa
Unajua mkuu vijana wanataka maisha na uchumi imara suo bora uchumi. Hebu ona huyu jamaa alichokifanya ndio utajua alikua na ndoto zake na sasa zimetimia anaanzisha familia.

Jamaa alipomaliza chuo alipata kazi ya kufundisha private akawa analipwa poa tu, kwa kijana asie na ndoto kubwa angeoa. Jamaa hakuoa, jamii ndio ikaanza ooh mbona huoi na una kazi. Mwana akafanya kazi akitafuta kazi ya mdoto yake, baada ya miaka minne akapata kazi bank. Jamaa akaenda jamii maneno oa oa, mwana alifanya kazi miezi 6 akaacha, kazi ilikua ngumu na pesa kidogo tofauti na matarajio.

Akarudi kitaa kama loser kabisa hana kila kitu, akaaza kufukuzia kazi popote huku akii kimbiza ndoto yake. Mara boom ikaitika TRA, mwana anasema hana anachodai zaidi sasa ni happy family.

Ona mkuu, ni rahisi kufanya aliyoyafanya kama huna familia. Hakuna mtu muoga kuacha kazi kama mwenye familia. Jamaa alikua na ujasiri kwa sababu alikua alone. Sasa kuna wale husema ooh ukioa milango inafunguka waapii, mbona jamaa kapata alichotaka bila mke?
 
Back
Top Bottom