Kataa ndoa tunakemea ufungaji wa ndoa, kipindi hiki kikali cha talaka na mgawanyo wa mali

unyonge wa kiuchumi, uoga wa ugumu wa maisha ya ndoa, unawafanya vijana kujificha aibu zao kwenye vichaka vya wazi kama hivi kwa fedheha sana.

eti kataa ndoa,
kumbe maskini ya Mungu kijana ni choka mbaya kiuchumi, haelewi mbele wala nyuma, umri unasonga na digrii yake ya First Class imeshindwa kabisa kumkwamua kwenye mkwamo ambao unamuhangaisha kisaikolojia daily, na hatimae anakuja kujifariji kwenye kundi la watu wa aina yake ambao hawamsaidii chocho zaidi ya kumstress zaid ili apate msononeko utakaommaliza polepole akiwa mpweke pekeyake. dah,

ama kwa hakika maisha ni kombolele, butua...
 
Mkiishi kwa amani na furaha, polisi na mahakama hazitawatambua katu!
 
Bwashee unajua kua hata matajiri wanateseka kwenye ndoa zao?
Unajua kua kuna watu wamefilisiwa kwa matokeo ya talaka?

Ndoa sio mbaya ila sheria za ndoa ndio mbaya hasa kwenye masuala ya talaka na mgawanyo wa mali.
 
Naam ndoa ni kwatu sahihi, na ndoa zenye maana zilikuwa zile za watu wa 1940- 1980.

Huku kwingine ni kujaribu kuikausha bahari, kwa tisheti ya ccm.
Una maneno magumu zaidi ya jiwe.
Ndoa Bado zipo za maana kabisa. Ila ukiokota yoyote mradi anapumua na Tako kubwa ni lazima ulie na karatasi za taraka.
 
Bwashee unajua kua hata matajiri wanateseka kwenye ndoa zao?
Unajua kua kuna watu wamefilisiwa kwa matokeo ya talaka?

Ndoa sio mbaya ila sheria za ndoa ndio mbaya hasa kwenye masuala ya talaka na mgawanyo wa mali.
ni umaskini mbaya sana gentleman,
kwamba huna kiwanja, huna nyumba, huna shamba, huna pesa, huna mke, umri umesonga, una digrii lakini huajiriki na unateseka kwa upweke na hatimae mvi na upara vinakupata ukiwa kwa wazazi, dah.

vijamaa vya 2000 vinatusua maisha kiulainiiiiii

kataa ndoa ni uzembe na mateso makali ya kisaikolojia
 
Umekariri upande huo tu naona,
Kuna watu wenye uwezo wao walikua ndani ya hizo ndoa,baada ya kutendwa wakaona ndoa ni utapeli na ni mateso yakujitakia,
Fikiria nje ya box kijana,elewa mada na comment zangu kwa akili huru.
 
Una maneno magumu zaidi ya jiwe.
Ndoa Bado zipo za maana kabisa. Ila ukiokota yoyote mradi anapumua na Tako kubwa ni lazima ulie na karatasi za taraka.
hahaha sio magumu ni vile nime jionea maajabu huku, sema una jaribu kukwepa tu.

ko una maanisha ndoa ni kama mchezo wa kamari, ucheze na amani yako, muda wako, uhuru wako ukale ndonga nzito 😅😂.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…