Katambi ampa onyo kali Afande Sele. Hatufanyi mzaha

Katambi ampa onyo kali Afande Sele. Hatufanyi mzaha

Kama angekuwa Jidenna ningemchezesha Bambi,,

Jinsi navyomchezea kama mpira wa Sambi,,

Kichwa hakifai dread lazima ziote tambi,,

Bora angetengeneza couple na yule Mange Kimambi,,
Ati, waziri mzima anaringia kishkwambi,
Atapigwa na dudu hadi tutatoa rambirambi,
Katika mazishi yake lazima nipigwe Kambi,
Hata kama watapika ugali pamoja na kumbikumbi.
 
Hapo zamani za kal kulikuwa na waziri wa mambo ya ndani, kutoka kule mkoa wa mlima mrefu. Huyu jamaa alikuwa kiboko kweli kweli,mbwembwe nyingi na maagixo kede kede.

Alikuwa maarufu zaidi kwa kutoa amri za siku saba, unifuate ofisini, vinginevyoooo.

Jamaa alikuwa moto kweli kwelihakuna asichoweza fanya, idara na taasisi zote aliingilia, hadi akapewa cheo kisichokuwepo.

sijui nataka kuandika nini, aagh!
Lyatonga Mrema?
 
Nimefuatilia kiasi siasa za Mh. Katambi, namuona ni mwanasiasa anayependa sana kutumia ubabe kwenye mambo yake. Nadhani walio karibu nae wamsaidie kumshauri abadili mfumo wa siasa zake kwani ye ni kijana na ana safari ndefu kwenye siasa. Unapokuwa kiongozi unakuwa umepewa dhamana ya kuwa mbele dhidi ya wenzio wengi ambao wapo nyuma yako. Hupaswi kuwaona wote walio nyuma yako si watu wenye akili kuliko wewe bali ni dhamana tu ambayo hamuwezi kupewa wote. Tutumie nafasi zetu kwa unyenyekevu na hofu ya Mungu ili kuacha alama njema nyuma yetu.
 
Mambo kadhaa yamechangia yeye kuwa hivyo
Kubwa, Anajishtukia, anajijua hana uwezo na amekamata cheo kizali. Kwa hiyo anaona anadhalaulika
 
Dudud baya akapondwe mapumbu kidogo na kipigwa miti huwa ana jisahau sana
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Katambi amempa onyo kali sana kwa Msanii Afande Sele baada ya kujirekodi video akitoa kauli pia akimwambia asifanye mzaha.

Soma Pia: Afande Sele: Si sahihi Waziri Katambi kumuita Dudu baya kwenye Meza walipokaa wenye tuhuma za Ushoga

Huyu Jamaa alipokuwa sauti na CDM alikuwa very smart ila aliponunuliwa kwa Vipande thalatha vya pesa wakaondoa brain akabaki kichwani na uji.

Afande ametoa maoni/mawazo kisha anapewa onyo wakati mawazo/maoni hayuapigwi rungu ni either uchukue au uyaache na si kumtisha aliyetoa maoni wakati ibara ya 18 inalinda uhuru wa kutoa maoni...Hawa vichaa wanashindwa kufuata katiba kabisa.
 
Back
Top Bottom