Moisemusajiografii
JF-Expert Member
- Nov 3, 2013
- 55,705
- 104,843
CCM ni bloody ng'ombezz!Mipango ya kijingajinga sana.
Nimekubali kabisa kuwa kama wewe ni masikini basi utabakia na umasikini wako wkaati kundi la watu wachache wakifaidi rasilimali za taifaHakuna anayejali mwananchi ndugu yangu.
Huyu sasa amepoteza hata ile akili ya kawaida. Ina maana mpaka sahizi hajui wanaoharibu amani ya nchi?Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ametoa wito mzito kwa viongozi wa dini nchini, wakiwemo Masheikh, Maaskofu, Wachungaji na Mapadri, kushirikiana na Serikali katika kulinda amani na utulivu wa taifa ili kuzuia machafuko yanayoweza kuwapingia wananchi haki zao.
“Yakitokea machafuko kwenye nchi yetu tutaenda wapi? Nchi yetu hii tuna historia nzuri ya amani, ndio maana imekuwa kimbilio kwa nchi za jirani zilizopata matatizo na machafuko. Tusichafue taifa tukawa wakimbizi kwenye taifa lingine mkapoteza haki zenu zote. Niwaombe sana Maaskofu wote, Masheikh, Wachungaji na Mapadri watusaidie katika eneo hili la kutunza amani.”
Waziri Katambi amehakikisha kuwa Serikali iko makini na imejipanga kikamilifu kuhakikisha amani na mshikamano vilivyorithiwa kutoka kwa waasisi wa taifa vinaendelea kulindwa kwa nguvu zote