Katarama kapiga tena kwenye mshono!

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Kufuru nyingine leo katoa Iriza new model ine ukitaka tamko nne au 4 ambazo kwa bei ya sokoni billion tatu na milion mia sita sawa na YUTONG 20

Leo Morogoro road ilikuwa ni kelele za mahoni wakati chuma zikiliacha jiji la Dar kuelekea Mbeya kwa msafara wa kuvutia zikiwa full headlight, full double hazard

Last week inasemekana pia alipeleka chuma kama hizo pia.. Nia yake kubwa ni kumkanyagisha miwaya mvimba macho anayeekea kukata pumzi kwenye njia zote za masafa marefu

Dar Bukoba

Dar Tunduma

Dar Mbeya

Dar Mwanza

Dar Kahama

Nilichokiona leo ni kile kitaa tunaita funika bovu! chuma zingine zote modeli ya mvimba macho zilikuwa zinapiga salute kubwq mbele ya mbabe IRIZA

Kwa kifupi alichofanya KATARAMA ni kutafuta heshima na kuonesha ubabeπŸ’ͺ🏿πŸ’ͺ🏿πŸ’ͺ🏿
Picha kwa hisani ya joseph_mbeya πŸ™πŸΏ
 
Mvimba Macho....
Hapa sjui ni Mchina na New Force zake?
Hongera kwa Mwamba Katarama. Uzuri wa Nchi zetu za Waizi ukiingia kwenye Biashara kama hiyo Wazee wa Madili/Wapigaji wanaotaka kutakatisha pesa zao ni Mwendo wa kukujazia Mabasi/Mtaji unavimba mjini kiulaiiiini.
 
JWTZ wameenda kuchukua Yutong za kutosha nina hakika kwenye vitabu imeekwa bei ya scania.
Una wakili?πŸ™ŒπŸΏπŸ™ŒπŸΏπŸƒπŸΏπŸƒπŸΏπŸƒπŸΏ
Hongera zake.
Ila zama hizi mabasi hayakimbii. Enzi zile unatoka Dar asubuhi unafika Mbeya mchana saa nane unakutana na ugali mezani licha ya barabara kuwa mbovu. Zile Scania zilikuwa balaa
Sasa hivi tochi nyingi halafu kumbuka hizi ni luxury coach
 
Gari za mchina zinawahi sana kuchoka, namba unakuta DZ lakini bodi imetepeta na engine inaenda kama kondoo, tulitoka Mwanza na katarama na mwenzangu kapanda yutong sisi tulifika Dar saa nne asubuhi, wazee wa Yutong wakafika saa kumi jioni, halafu nauli ni ileile we kuwahi tu booking!
 
Una wakili?πŸ™ŒπŸΏπŸ™ŒπŸΏπŸƒπŸΏπŸƒπŸΏπŸƒπŸΏ
Siku hizi hakuna kesi za mahakamani ni mwendo wa kutupwa msituni tu.

Swali ni kuwa, je nimezindikwa vya kutosha kuamini siwezi kamatwa kihuni, jibu ni ndio. Nina zindiko la Mwalufyale, wakija wanakuta kisiki kitandaniπŸ˜‚
 
JWTZ wameenda kuchukua Yutong za kutosha nina hakika kwenye vitabu imeekwa bei ya scania.
Una wakili?πŸ™ŒπŸΏπŸ™ŒπŸΏπŸƒπŸΏπŸƒπŸΏπŸƒπŸΏ
tulitoka Mwanza na katarama na mwenzangu kapanda yutong sisi tulifika Dar saa nne asubuhi, wazee wa Yutong wakafika saa kumi jioni, halafu nauli ni ileile we kuwahi tu booking!πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…