Pamoja na ukweli kwamba madereva "vichaa" wapo makampuni yote. Soko la bus Tanzania lilikuwa limetawaliwa na Scania kwa series zake mbalimbali.
Ghafla Machina kavamia soko na kumuondoa Scania (Swedish). Pamoja na mchina kuchukua nafasi wamiliki wengi wamekuwa wakibadili baadhi ya spear na kuweka za Scania pale engine, gearbox na differential zinapokuwa zimechoka na kuwa na power just like Scania.
Meanwhile mchina nae amekuwa akiboresha. Sasa Scania ametaka kurudi kwenye soko kwa kuzalisha series zinazoendana na mazingira na Bei muafaka zaidi, na Katarama ni mojawapo ya makampuni yamepata series hizo. Sasa vita ni kubwa sana kati Dragon/Yuotong/Higher etc vs Scania. Mashindano yapo kwenye three main areas.
1. Uimara wa board kwa maana ya ustahimilivu wa mazingira magumu, endurance wakati wa ajali, road stability.
2. Bei ya kununulia na gharama ya uendeshaji(Price, maintenance and operational costs). Scania guaranteed 6years bila overhaul ya engine plus buyuback guarantee.
3. Mwendokasi(torque )hasa kwenye sehemu za mwinuko unampatia guarantee mteja kutembea constant speed at all terrains, na pasipo ongezeko la matumizi makubwa ya mafuta.
Yapo mengine ambayo ni technical lakini watumiaji wengi wanaangali hayo zaidi.
Sasa hii vita unaweza kuiona wakatia Sauli amenunua Scania, Katarama nae amekuwa amekutana nayo.
Nimalizie kwa kusema madereva ni victims kwani "ukiwa na Binti mrembo mara nyingi hupenda kuonyesha urembo wake" Sasa katika kuonyesha urembo ndio wakati mwingine kukosa umakini, kuoverspeed mahali pasipohitajika. Ila vita ipo kwa warembo na hata wanaokuja hapa wengi wamefadhiliwa kusema vibaya kampuni ile.
Mabus yanayokimbia, na yanayofanya vurugu mbaya njiani ni mengi sana ila hayasemwi na hao wanaosema ila ikiwa brand ya bus ni tofauti wanapaza sauti. Hiki ndio kiini Cha yote