Katavi: Afisa Ardhi ahukumiwa kwenda jela Miaka 2 kwa tuhuma za Rushwa

Katavi: Afisa Ardhi ahukumiwa kwenda jela Miaka 2 kwa tuhuma za Rushwa

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Afisa Ardhi Msaidizi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Japhet Noberth MweziMpya, amehukumiwa kwenda jela miaka 2 au kulipa faini ya TSH.200,000 kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya TSH. 70,000

Katika Hukumu hiyo ya shauri la jinai Na. CC. 90/2022 iliyotolewa Agosti 30, 2022 na Hakimu Mkazi, Gasper Luoga, Mshtakiwa amekiri makosa yake na kulipa faini ili kuepuka kifungo
 
Fine laki mbili???!!! Duh
Kweli maisha sio fair wengine wananunua mabasi halafu kuulizwa wanaogopwa.

Mtaani kwangu kuna bwana mdogo anafanya kazi kama muhasibu mdaidizi wa manispaa flani, kajenga Nyumba ya kama miln 300 ndani ya miezi mi'4.

Hata kama ni mkopo benki walimkopa kwa dhamana ipi? kwao alipotoka Morogoro wanaishi Nyumba ya familia yenye matumbo matatu yaani Nyumba ya Babu yake ambae ana wake watatu.

Halafu watu wanamsifu jamaa anakili sana lakini mtaani hapohapo kuna dogo muokota chupa za plastiki aliiba pampu ya maji kwa jirani alipigwa nusu ya kuuwawa na mpaka sasa kapoteza meno yote ya mbele na mtaani anachukiwa kama njaa akipita tu watu wanachukua tahadhari ya vitu.

[emoji20][emoji20][emoji20] Kweli maisha sio fair kabisa
 
Kweli maisha sio fair wengine wananunua mabasi halafu kuulizwa wanaogopwa

Mtaani kwangu kuna bwana mdogo anafanya kazi kama muhasibu mdaidizi wa manispaa flani, kajrnga Nyumba ya kama miln 300 ndani ya miezi mi'4

Hata kama ni mkopo benki walimkopa kwa dhamana ipi???
Taja manispaa hyo

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Amelipa faini baada ya kukiri kosa, kwa mujibu wa utumishi wa umma hana kazi tena uyo, maana ashatiwa hatiani licha ya kulipa faini kukwepa adhabu ya kwenda magereza kutumikia kifungo.
 
Huyo amekula bila kuangalia urefu wa kamba yake hajioni kuwa ni afsaa mdogo tu.
 
amehukumiwa kwenda jela miaka 2 au kulipa faini ya TSH.200,000 kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya TSH. 70,000[emoji848][emoji2827]
 
Wanakwapua mabilioni wanatanua kwenye ma V8 Iila huyu Afisa wa elfu 70 anaenda Jera, !!!!! Dah Tanzania yangu!!!!!!
 
amehukumiwa kwenda jela miaka 2 au kulipa faini ya TSH.200,000 kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya TSH. 70,000[emoji848][emoji2827]
Hapo ameingiliwa 130,000/= [emoji16]
 
Back
Top Bottom