Katavi: Afungwa miaka 30 kwa kufanya mapenzi na mtoto wake

Katavi: Afungwa miaka 30 kwa kufanya mapenzi na mtoto wake

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
bakaa.jpg
MAHAKAMA ya Wilaya Mpanda, imemuhukumu Agustino Michese (59) kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa kufanya mapenzi na mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 16.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya Mpanda Rebeka Mwalusako amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo tarehe tofauti za mwezi wa tano hadi Disemba 30,2022 katika kijiji cha Isinde.

Amesema mtuhumiwa ametenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 158 kifungu kidogo cha (1) (a) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyo fanyiwa marejeo mwaka 2019.

Hatahivyo mtuhumiwa wakati akisomewa maelekezo ya awali alikili kutenda kosa hilo huku akijitetea alikuwa amelewa hivyo alijua anaefanyanae tendo hilo ni mke wake.

Upande wa mashitaka umeleta mashahidi watano akiwemo mtoto mwenyewe ambapo mtoto huyo ambae jina lake limehifadhiwa wakati akitoa ushahidi wake alisema baba yake amemfanyia kitendo hicho mara tatu huku akimtaka kutopiga kelele endapo atapiga atamfanyia kitu kibaya.

Ndipo alichukua maamuzi ya kumuelezea shangazi yake kutokana na kile anachofanyiwa na baba yake huku akidai hakuweza kumwambia mama yake kwababu ana matatizo ya akili hivyo alihofia alimwambia hatolifanyia kazi suala hilo.

Shahidi mwingine ambae ni daktari aliemfanyia vipimo mtoto huyo ameiambia mahakama kuwa uchunguzi wa kitabibu umebaini ni kweli mtoto huyo aliingiliwa.

Amesema mbali nakubainika kuingiliwa pia mtoto huyo ilibainika kuwa ameambukizwa magonjwa ya dhinaa ambapo baba yake baada ya kufanyiwa vipimo aligundulika kuwa na magonjwa hayo.

MWANANCHI
 
Lakini sheria ya kanunu ya adhabu Sura namba 16, marekebisho mapya ni 2022 siyo 2019.
 
Sioni wale wanaosema “wanawake ni makatili sana”, “sijawahi kuona viumbe wa ajabu kama wanawake”, au wale wanaosema ukiona huyo mwanaume kafanya hivyo ujue mwanamke wake kamkosea hakuna mwanaume asie na akili.

Huwa natamani niwawashe vibao.
Mje na huku mumchukue baba yenu, mwakilishi wenu huyu sasa ndo symbol ya wanaume wanaosema mwanaume hawezi kutosheka na mwanamke mmoja.

Na msije na utetezi eti sio wanaume wote,
Hata mnavotukanaga wanawake mnasema ni viumbe wasio na akili. Basi huyu ndo amewakilisha wanaume wote, kichwa cha chini kikiwa kimewaka anaweza paramia hata farasi
 
Ukiweka jinsia katika hii case utaonekana wewe ndio umeyumba zaidi ya hata hakimu aliyetoa hiyo adhabu pekee pasipo kuunganisha ushahidi wa afya ya akili ya mtuhumiwa na hukumu ya matibabu ya afya ya akili.

Kama ni ukweli madai ya Binti kwamba mama mzazi ni mgonjwa wa akili ni rahisi kuhisi pia baba mzazi ni mgonjwa.

Shangazi amesaidia kuwahisha “majeruhi” kwenye mamlaka tu ila tayari kilema kimeshampata mlengwa. Pole sana kwa mtoto.

Tuendelee kushindania jinsia huku tukipotezea mambo ya msingi na wajibu wetu wa “kijinsia”, tutakipata tunachokitafuta.
 
Back
Top Bottom