Dr am 4 real PhD
JF-Expert Member
- Jun 30, 2016
- 20,877
- 43,633
Tukio la kujinyonga la kijana wa CHADEMA kutokana na tofauti za KISIASA na mama yake mzazi ambae Ni CCM
Chuki za KISIASA na UHASAMA baina ya mama na mtoto umepelekea kifo
Najaribu kujiuliza huyu mama yake mzazi atatoa machozi msibani?
Najaribu kujiuliza CCM TAIFA au CCM Mpanda watampelekea kifuta jasho Cha kumpoteza mtoto Alie mzaa yeye mwenyewe?
Mama mzazi hato mwona Tena mwanae kisa itikadi za kisiasa hili Jambo linaumiza Sana itikadi za kisiasa...
Pengine mama aliamini kua mtoto Alie mzaa mwenyew hawezi kua na itikadi tofauti na zake pengine hapo ndio kweny mzizi wa hiki tukio
Somo la political torelance litolewe kwa raia wote na tuvumiliane tupendane.
Mungu Ibariki Tanzania
======
Kijana anayefahamika kwa jina la Twaybu Omary, 22, mkazi wa Mtaa wa Nsemulwa Kata ya Nsemulwa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, amekutwa bafuni akiwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia waya mweusi, huku chanzo kikidaiwa ni baada ya mama yake kukataa kuwa mfuasi wa CHADEMA.
Kitanzi
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi Abdi Isango amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema siku moja kabla ya kifo cha kijana huyo kulitokea tofauti ya majibizano ya kisiasa, ambapo marehemu alikuwa ni mfuasi wa CHADEMA na alikuwa akimshawishi mama yake kuhamia chama hicho ndipo mama yake ambaye ni mfuasi wa CCM akakasirika na kumpiga kofi mwanaye.
Akimzungumzia mtoto wake huyo aliyejiua, Mama mzazi wa marehemu Mariam Shamsha, amesema mtoto wake alikuwa anapenda kusoma lakini alishindwa kumtimizia ndoto zake kutokana na kipato chake kuwa kidogo.
"Mwanangu aliniambia nijiunge na CHADEMA, mimi nikakataa nikasema siwezi kujiunga, nikamuambia mimi nina uzalendo na nchi yangu", amesimulia Mama wa marehemu.
( Via Eatv.tv)
======
TAARIFA YA JESHI LA POLISI
KUJINYONGA
Mnamo tarehe 30/09/2020 majira ya saa 14:30 huku katika mtaa wa Kwalakwacha kata ya Nsemulwa na Tarafa ya Kashaulili Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi. Mtu mmoja anayejulikana kwa jina la TWAYBU S/O OMARY, mika 24, mkulima, muislamu na mkazi wa Nsemulwa. Alikutwa bafuni akiwa amejinyonga kwa kutumia waya wenye rangi nyeusi huku mwili wake ukiwa una ning'inia kwenye kenchi.
Baada ya taarifa ya tukio hilo kufika kituo cha Polisi timu ya makachero pamoja na daktari walifika eneo la tukio na kukagua eneo hilo kisha daktari alifanya uchunguzi wa kitabibu wa mwili huo. Ambapo baada ya taratibu zote kukamilika mwili ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.
RAI:- Jeshi la Polisi Mkoani Katavi linatoa wito kwa wamiliki na watumiaji wa vyombo vya moto kufuata sheria za usalama barabarani itakayosaidia kujiepusha na matukio ya ajali zinazoweza kuepukika yasitokee ndani ya jamii yanayopelekea kugharimu maisha ya watu na taifa kwa ujumla.
IMETOLEWA NA:-
ACP. Benjamin E. Kuzaga,
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Katavi.