Katavi: Mabasi ya Wanafunzi yabainika kufungwa mipira kwenye mfumo wa breki

Katavi: Mabasi ya Wanafunzi yabainika kufungwa mipira kwenye mfumo wa breki

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoa wa Katavi kimebaini dosari katika mabasi yanayotumiwa kusafirisha Wanafunzi katika Shule za watu binafsi ikiwemo baadhi ya mabasi kukutwa yamefungwa mipira kwenye mfumo wa breki ambayo ni hatari kwa usalama.

Dosari hizo zimebainika wakati Kikosi hicho kikifanya ukaguzi wa mabasi hayo kabla muhula mpya wa masomo kuanza ambapo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Katavi, Leopord Fungu amewataka madereva kutojaza Wanafunzi kinyume na idadi inayotakiwa huku akisisitiza kuzingatia nguzo tano za udereva wa kujihami.

Nao, baadhi ya madereva wa mabasi hayo wamefurahishwa na kitendo cha ukaguzi huo sambamba na kukumbusha taratibu mbalimbali za uendeshaji wa vyombo vya moto.
 
Ingekuwa wanakagua wilaya zote, kama huku mbinga shule ya mbunge ina magari mabovu, likikusanya watoto asubuhi kupeleka shule likirudi linaenda gereji, mchana pia likirudisha watoto linaenda gerreji, gari mda wote inashinda gereji kutengenezwa.

Shule nzuri sana,shida gari linatembea huku linatetema,

Mbunda,,,,fanya ubadili school bus mbovu.
 
Kupitwa na uzi sitaki japo sina cha kusema asante kwa kunisoma ni mm mr pipa
 
Shida ya hizi school bus wananunua mabus yaliochakaa either bus au noah zile wanazipiga rangi zao za yellow kazi wanaanza hawazingatii usalama angalieni shule kama indian school ya temeke ilivo na mabus tena mapya mazuri sio sisi tunajali faida tu uwekezaji hamna
 
Alafu kuna mpuuzi mmoja anasema kataa polisi,kama syo uchizi ni nini?
 
Toeni kodi kwenye school bus hizo acheni mambo ya kutaka tutumie vitu chakavu hata hizo mlizokagua mnaona zipo sawa ni mbovu tuu itafika muda watoto wetu watapanda Quantum au hizo Coaster mnazopanda staff shule sio adhabu...
 
Back
Top Bottom