Katavi: Mwanafunzi wa Darasa la Tatu ajinyonga kwa kukosa nguo mpya siku ya Sikukuu

Katavi: Mwanafunzi wa Darasa la Tatu ajinyonga kwa kukosa nguo mpya siku ya Sikukuu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mwanafunzi wa Darasa la Tatu katika Kijiji cha Uruwila, Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi amejinyonga kwa kutumia sweta lake alipokuwa amelala chumbani kwake.

Akitoa taarifa ya tukio hilo Januari 03. 2025, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Kasta Ngonyani, amesema tukio hilo limetokea mnamo January 2, 2025 Majira ya Saa tisa alasiri.

Ameeleza kuwa Matrida Kalibi aligundua kujinyonga kwa mtoto wake Christina Kalilo (8) mwanafunzi wa Darasa la tatu.

Ngonyani ameongeza kuwa mwanafunzi huyo amejinyonga kwa kutumia sweta lake kwenye chumba alichokuwa amelala.

Taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi imeeleza kuwa chanzo cha kujinyonga kwa Mwanafunzi huyo ni kutonunuliwa nguo za Sikuuu ya Chrismas na mwaka mpya.

PIA SOMA

- Dodoma: Mtoto ajinyonga kwa kukosa nguo za Sikukuu
 
Kuna muda umaskini ni kitendawili kigumu sana huwezi kumueleza sababu gani hautamnunulia nguo mpya mtoto wa umri huo na akakuelewa, ye ataamini haumpendi na maumivu yanazidi ile siku anaona watoto wenzake wote wamevaa nguo mpya
 
Narudia kuwaambia, msichukulie mambo haya kirahisi sana, Leo Kwa yule, kesho kwako.


Ulishawah jiuliza mtoto kama huyo wa Miaka 8 ajifunzia wapi kujinyonga??.

Ndugu zangu, HAKIKISHENI WATOTO WENU NYUMBAN WANAANGALIA MICHEZO YA TV INAYOENDANA NAO KIUJUMBE KIMAADILI NA KIUMRI.


Katoto kanaona Movie , Dada Mmoja, kakatazwa asiolewe na Muislam, Dada ni Mkristo, Dada anaamua kujinyonga.

Kumbuken scenes kama hizi Huwa zingatia uzuni na ndan ya familia, wapo ambao hulopoka... Bora alivyoninyongaa, wazazi wake makatili.

Vitoto vinasikiliza, vinaona jinsi ya kujinyonga, kanaishi siku kakifanya kosà, mzazi akakachapa, kanakumbuka Ile movie, kanamuona Baba ni katili.

Kwanini asijinyongr naye?? Atajinyonga akiwa Hujui kitendo anachofanya ,yeye atajinyonga akichukilia ni mchezo tu kwamba Baba na mama watamkuta, wataanza Kuliaa, watambembeleza, kumbe ndo kanakua kamekufaa
 
Back
Top Bottom