KATAVI: Shule ya Tulieni ina Wanafunzi 2,509, madawati 169, Walimu 14

KATAVI: Shule ya Tulieni ina Wanafunzi 2,509, madawati 169, Walimu 14

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Tulieni iliyopo Manispaa ya Mpanda, Mkoa wa Katavi amesema shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa madawati ambapo mpaka sasa shule hiyo ina madawati 169 ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi 2,500 ambao wengi wao hawana sehemu za kukaa.

Ameyasema hayo alipokuwa aliwasilisha changamoto hizo mbele ya Mwenyekiti wa CCM wa Tawi la Tulieni walipotembelea, Aprili 24, 2026, ili kujua mwenendo wa shule hiyo pamoja na kuzipeleka maeneo husika.

Katika changamoto nyingine ya ukubwa wa eneo wa shule hiyo Mwenyekiti wa CCM katika tawi hilo amesema wameichukua na wataiwasilisha Ili kupata majibu ya kwanini eneo hilo limekuwa ni dogo tofauti na uhalisia wa taarifa za kwenye karatasi.

Chanzo: KINYOGOTO JR
 
Katavi ni miongoni mwa mikoa michache iliyoruhusiwa kuvuna miti ili kusafirisha magogo.
Ikiwa mkoa una miti ya kutosha kiasi hicho ni vipi shule za mkoa huo zikose madawati?
 
Back
Top Bottom