BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
UMESIKIA ishu ya baadhi ya wanaume wa Kijiji cha Mapili Kata ya Ilela, Halmashauri ya Mlele mkoani Katavi?
Kama hujasikia ipo hivi, kumbe wanatamani sana kuwawezesha wake zao kiuchumi, lakini wanashindwa kuwawezesha kiuchumi wakihofia wanawake hao kubadilika na kutowasikiliza wakiwa na kipato.
Hayo yamebainika katika mdahalo maalum ulioandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Marie Stopes Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali uliofanyika jana Julai 12, 2022 katika Kijiji cha Mapili Kata ya Ilela, kwa lengo kutoa elimu ya afya ya uzazi na masuala ya ukatili wa kijinsia.
Akichangia mada kwenye kongamano hilo, Yohanne Samuel alidai wake zao wakipata fedha hujiona wapo juu ya waume zao na ushahidi mzuri ni pale wanapovunja vikundi vyao maarufu kama Vikoba.
“Wakipata fedha za Vikoba huwa wanakuwa wakali kwa kujiona wana fedha nyingi, ndiyo sababu tunaogopa kuwasaidia kiuchumi, watatunyanyasa sana,” alisema Abdul Japhar.
"Sisi wanaume sio wanyanyasaji, isipokuwa wake zetu ndio hutunyanyasa, kwa sababu utakuta mtu unampa mtaji halafu baadaye anakuja kukugeuka," alisema Juma Kapangano kwenye kongamano hilo.
Kwa upande wao walengwa ambao ni wanawake wa kijiji hicho wamedai kuachiwa majukumu ya kifamilia na waume zao, hali inayofanya wao kutaka kujishughulisha na biashara ndogondogo, ili kulea watoto wao.
"Mwanaume anaweza kutoka, akirudi anadai chakula tena anaweza kukupiga wakati hajaacha hata pesa ya chakula, wala mboga, hivyo ili kuhakikisha familia inakula inakubidi wewe mwanamke uhangaike," alisema Rosemary Alex
"Wanawake tunanyanyasika sana hata magonjwa haya ya VVU kwa asilimia 99 Kijiji chetu wanaweza kuwa wamechangia wanaume, kwa sababu mwanamke anaweza kushawishika kutafuta pesa kwa njia zisizo rasmi kama kuchepuka,” amesema Gaudensia Issa.
Naye mshauri wa masuala ya kijinsia, vijana na makundi maalum kutoka shirika la Marie Stopes, Magdalena Thomas amesema wamebaini kwamba wananchi wa kijiji hicho hawana uelewa na masuala ya ukatili wa kijinsia.
"Kuna elimu duni kwenye masuala ya ukatili wa kijinsia pamoja na afya ya uzazi, hivyo tunaendelea kufanyia kazi pamoja na kuhamasisha wadau wengine waweze kufika na kutoa elimu hiyo," alisema.
Source: Habari Leo