Katazo la kulala wanaume wawili Lodge

Wild sniper

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2015
Posts
4,399
Reaction score
8,629
Ni Jumatatu tulivu tenaaa

Hivi hili katazo ambalo tunakutana nalo kwenye nyumba za kulala wageni iwe lodge, guest au hotel ya kuwa hawaruhusiwi kulala wanaume wawili limekaaje wandugu? Au limezingatia nini hasa hadi kuwekwa maana ka wengine naona sio sawa kabisa wengine tuna safari tunafikia sehemu na bajeti inabana kweli tuchukue room 2 kulala masaa kadhaa tu tuendelee na safari zetu.

Sijajua ni katazo la kiserikali yani kuna hiyo sheria au ni maamuzi tu ya wenye hizo biashara hebu wanaojua watujuze, na kama ishu ni ushoga hahah mbona wanawake wanalala au wao hawahofiwi kuwa wasagaji?
 
Je wadada nao wana katazwa kulala wa wili wawili ?/kama katazo hili lina wa exclude wadada basi huu ni unyanyasaji wa kijinsia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…