Sisi wengine huyo paskali tulishampuuza maana kipindi cha wale covid 19 walipofukuzwa alijitokeza na kutuletea notes za administrative law humu jf akijifanya kueleza kuwa walifukuzwa bila kufata taratibu za misingi ya haki huku akitumia maneno ya KILATIN kama NEMO JUDEX IN CAUSA SUA NA AUDI ALTERAM PARTEM, mim nilimuuliza maswali yafuatayo,
1. Je anaamin hao(covid 19) wamefukuzwa
2. Kama jibu ni ndio hata bila kufata taratibu je watabaki kuwa wanachama au mpaka mahakama iwarudishie uanachama wao kama itaona kunahoja hio?
3. Hukumu yoyote inapotolewa hata kama imekiuka misingi ya kisheria je huwa haifanyi kazi au inafanya kaz mpaka itakapoamuliwa vinginevyo kwenye refaa au mapitio?
Haya maswali hajawahi kuyajibu. Mwisho nikamshauri kuwa kama anaona wameonewa akajiunge na jopo la mawakili wanaowatetea hao covid 19 napo hajawahi kufanya hivyo sasa huyo naye ni wa kuamini au ni kumpuuza tu, kinachonishangaza ni kwamba humu jf kuna watu huwa wanafikiria huyo jamaa ni smart kumbe ni mbumbumbu tu haya leo hii mwanasheria anamuunga mkono Assad ambaye hajui chochote kuhusu mikataba hio kama sio aibu ni nini?