Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Kumekuwa na mjadala unaoibuka na kufa kila mara. Nao si mwingine bali wa kuruhusu uraia pacha katika Tanzania. Serikali imekuwa ikipiga danadana wakati huo ikipigia chapuo uwekezaji wa watanzania waishio ughaibuni nchini. Kuna dalili kuwa serikali ina uchu na pesa ya watu hawa lakini haiwataki wao. Nchi za Nigeria na Kenya zenye uraia pacha zimekuwa zikivuna fedha nyingi za kigeni toka kwa raia wake walioko ughaibuni. Tanzania, tokana na sera mbovu ya uraia, inazidiwa na hata kiinchi kidogo kama Togo chenye watu takriban milioni kumi na kinachozidiwa na mkoa wa Lindi kwa ukubwa. Bonyeza hapa kujua ni nchi gani inavuna pesa toka diaspora na kwa kiasi gani.
Kwa kuzingatia hayo hapo juu, kati ya CCM, serikali, na Watanzania, nani mwenye mtima nyongo na anayependa vya dezo toka kwa diaspora wakati anawachukia?
Kwa kuzingatia hayo hapo juu, kati ya CCM, serikali, na Watanzania, nani mwenye mtima nyongo na anayependa vya dezo toka kwa diaspora wakati anawachukia?