Kati ya dagaa na mlenda, Mboga gani unapendelea kula na ugali?

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Ili ugali upande na unoge unahitaji visindikizaji yaani mboga, kwa upande wangu mie napenda sana ugali na dagaa ukiwepo na mlenda naweza kula ugali kwa raha sana.

Kama kuna mlenda napenda dagaa wakavu au wapikwe rosti changanya nyanya chungu na bamia yaani wee acha tu.

Wakuu, wewe ugali unapenda kula na mboga gani?

Ugali mlenda.jpg

​
 
Mimi ugali huwa naushusha sana hasa kukiwa na picha ya samaki mbele yangu.

Vilivile ninaweza kula ugali mkubwa kwa ugali mdogo, yaani ugali mkubwa nitauchukulia kama ugali, na ugali mdogo unakuwa kama mboga tamu mno. Ni mindset tu!
 
Ili ugali upande na unoge unahitaji visindikizaji yaani mboga, kwa upande wangu mie napenda sana ugali na dagaa ukiwepo na mlenda naweza kula ugali kwa raha sana.

Kama kuna mlenda napenda dagaa wakavu au wapikwe rosti changanya nyanya chungu na bamia yaani wee acha tu.

Wakuu, wewe ugali unapenda kula na mboga gani?

Hata mimi hivyo hivyo...
 
Hivi ni nani aliyetubunia kula hiki chakula (ugali) kisicho na ubora na kukifanya kuwa ni chakula chetu kikuu cha kujivunia?

Chakula kinachotakiwa kuliwa kama dawa na ukivuka masharti kinakudhuru, kwanini tuanzishe mada yake kukisifia?

Tusivyojua madhara makubwa yatokanayo na ugali, wengi hudhani kuwa ugali ni chakula bora kinacholeta nguvu na siha mwilini kuzidi aina zingine zote za vyakula vya nafaka!

Kwani hizo mboga hauwezi kuzila kwa kutumia chakula kingine na si ugali?

Dagaa rost kwa viazi vitamu na mlenda kwa mihogo, hauwezi kula hivyo?

Unavyoutaja ugali kwa kuusifia namna hiyo miye hadi naishiwa power.
 
Hivi ni nani aliyetubunia kula hiki chakula (ugali) kisicho na ubora na kukifanya kuwa ni chakula chetu kikuu cha kujivunia?

Chakula kinachotakiwa kuliwa kama dawa na ukivuka masharti kinakudhuru, kwanini tuanzishe mada yake kukusifia?

Tusivyojua madhara makubwa yatokanayo na ugali, wengi hudhani kuwa ugali ni chakula bora kinacholeta nguvu na siha mwilini kuzidi aina zingine zote za vyakula vya nafaka!

Kwani hizo mboga hauwezi kuzila kwa kutumia chakula kingine na si ugali?

Dagaa rost kwa viazi vitamu na mlenda kwa mihogo, hauwezi kula hivyo?

Unavyoutaja ugali kwa kuusifia namna hiyo miye hadi naishiwa power.
Ugali ni mtamu japo ni chakula cha ajabu.
 
Sijawahi kula mlenda, I don't like it kutoka uvungu wa moyo, sipendi pia kisamvu.
Mkuu hizi mboga za kienyeji saazingie waweza usizipende kutokana na mapishi.

Mlenda una mapishi mengi na una ladha nyingi pia kutegemeana na mapishi.

Na kisamvu nacho hivyo hivyo kina ladha nyingi sana.

Kama ulivyo wewe, nami hunitokea baadhi ya mapishi ya mboga za kienyeji, mdomo wangu hushindwa kuhimili ladha zake.
 
Back
Top Bottom