Hata mimi hivyo hivyo...Ili ugali upande na unoge unahitaji visindikizaji yaani mboga, kwa upande wangu mie napenda sana ugali na dagaa ukiwepo na mlenda naweza kula ugali kwa raha sana.
Kama kuna mlenda napenda dagaa wakavu au wapikwe rosti changanya nyanya chungu na bamia yaani wee acha tu.
Wakuu, wewe ugali unapenda kula na mboga gani?
Nimeipenda hii🤣🤣Dagaa, bila kusahau kapilipili muwasho fulani hv
Anyway, unapata chakula kwa tabu afu bado unaweka pilipili 😂
Hii combo ni balaa upate na samaki wa kuchoma hapo na ka pilipiliUgali wa muhogo na kisamvu
Dagaa chukuchuku halafu unaweka na ndimu 🏃Ugali na dagaa chukuchuku mambo yanakuwa saaafi.
Bibi yangu alikuwa akipendelea ugali wa muhogo uliochanganywa na unga wa mahindi kwa nyama ya kuku iliyopikwa kama supu bila nyanya mwaka 2000 iyoo miss sana my grand mamaHii combo ni balaa upate na samaki wa kuchoma hapo na ka pilipili
Hivi ni nani aliyetubunia kula hiki chakula (ugali) kisicho na ubora na kukifanya kuwa ni chakula chetu kikuu cha kujivunia?Ili ugali upande na unoge unahitaji visindikizaji yaani mboga, kwa upande wangu mie napenda sana ugali na dagaa ukiwepo na mlenda naweza kula ugali kwa raha sana.
Kama kuna mlenda napenda dagaa wakavu au wapikwe rosti changanya nyanya chungu na bamia yaani wee acha tu.
Wakuu, wewe ugali unapenda kula na mboga gani?
Ugali ni mtamu japo ni chakula cha ajabu.Hivi ni nani aliyetubunia kula hiki chakula (ugali) kisicho na ubora na kukifanya kuwa ni chakula chetu kikuu cha kujivunia?
Chakula kinachotakiwa kuliwa kama dawa na ukivuka masharti kinakudhuru, kwanini tuanzishe mada yake kukusifia?
Tusivyojua madhara makubwa yatokanayo na ugali, wengi hudhani kuwa ugali ni chakula bora kinacholeta nguvu na siha mwilini kuzidi aina zingine zote za vyakula vya nafaka!
Kwani hizo mboga hauwezi kuzila kwa kutumia chakula kingine na si ugali?
Dagaa rost kwa viazi vitamu na mlenda kwa mihogo, hauwezi kula hivyo?
Unavyoutaja ugali kwa kuusifia namna hiyo miye hadi naishiwa power.
Unateseka ukiwa wapi?Unavyoutaja ugali kwa kuusifia namna hiyo miye hadi naishiwa power.
Mkuu hizi mboga za kienyeji saazingie waweza usizipende kutokana na mapishi.Sijawahi kula mlenda, I don't like it kutoka uvungu wa moyo, sipendi pia kisamvu.