Kati ya DED na DAS nani bosi wa mwingine?

Swali la msingi hapa ni.. Je kuna haja ya kuwa na DED pamoja na DAS kwa wakati mmoja? au nyadhifa mojawapo ingefutwa tu.
 
maDAS na ma DED wa sasa hivi ni makada wa ccm
tusitegemee maendeleo,vyeo wamepewa kama ajira za ndani za ccm kwa wanachama wake...la la land
 
DED = District Executive Director, DAS = District Administrative Secretary & DC = District Commissioner. Wote hao ni kuteuliwa na kutumbuliwa wakati wowote. Nani mkubwa hapo
Kiutendaji DAS ndio mwenye mamlaka zaidi DED anatekeleza maagizo ya DAS
 
Virefu vyao tafadhali.
 
Wadungu naomba nami nichangie mada hii ambayo wengi wanaona kama uhusiano wa DED na DAS ki-protokali unachanganya. Mchango wangu utazingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi.
1. Mkuu wa Wilaya (DC)
Mkuu wa Wilaya anateuliwa na Raisi kwa mujibu wa kifungu cha 13 (2) cha sheria ya Tawala za Mikoa (The Regional Adminstration Act, 1997). Majukumu yake ni pamoja na kuwa mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya. Kwa mantiki hiyo anakuwa muwakilishi wa Raisi katika kusimamia ulinzi, usalama na shughuli za maendeleo kwa ujumla. Akishateuliwa mkuu wa Wilaya anaapishwa na kusimamiwa kiutendaji na mkuu wa Mkoa (kifungu 13 kifungu kidogo cha 3).

2. Katibu Tawala wa Wilaya (DAS)
Kifungu cha 16 (2) cha sheria ya Tawala za Mikoa kinamtambua DAS kama principal adviser (yaani mshauri mkuu) wa DC. Kifungu hiki pia kinasema DAS anateuliwa kwamujibu wa sheria ya Utumishi wa Umma. Bahati mbaya sina hiyo sheria hapa na nimetafuta mtandaoni sijaweza kuipakua. Ila natoa hoja yangu hapa kwa kuzingatia uteuzi wa Ma-DAS uliofanywa tarehe 5.8.2018 na Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma. Katika tangazo lake kifungu cha 1.2 Waziri alisema, "Leo nimewaita kuzungumza nanyi kuhusu Uteuzi na Uhamisho wa baadhi ya Makatibu Tawala wa Wilaya. Kwa mamlaka niliyokasimiwa kwa mujibu wa Sheria nimefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Wilaya ili kujaza nafasi wazi kumi nane (18) zilizopo katika wilaya za Kinondoni, Mpwapwa, Dodoma, Iringa, Bukoba, Kigoma, Siha, Mtwara, Newala, Misungwi, Njombe, Kondoa, Manyoni, Kilindi, Chunya, Pangani, Bagamoyo na Handeni".
Hivyo, kwamujibu wa tangazo la Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma ambalo nimenukuu hapa, uteuzi wa DAS upo chini yake kisheria.

3. Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya (DED)
Kwa mujibu wa kifungu cha 22 (2) cha Sheria ya Utumishi wa Serikali za Mitaa ( The Local Government Service Act, 1982), DED anateuliwa na Raisi. Majukumu kiutendaji DED anakuwa Chief Executive wa Halmashauri na anaripoti kwa Katibu Tawala wa Mkoa (RAS).

Hitimisho
Kwangu mimi sioni mkanganyiko wowote wa kisheria kati ya DED na DAS, maana DED anateuliwa na Raisi na DAS anateuliwa na Waziri wa Utumishi wa Umma. Sema DAS anaweza kuonekana katika mazingira flani kuwa boss wa DED pale ambapo anatekeleza kazi anazotumwa na DC. Pia, nimewahi kuona mahala DAS anaudhuria vikao vya Council Management (CMT) ambavyo DED ndio mwenyekiti. DC ni mkuu kiitifiki kwa DED ingawa wote wanateuliwa na Rais, utofauti wao unatokana na majukumu. DC anapolinda amani, usalama na maendeleo ni pamoja na kazi anazofanya DED na wakuu wengine wa vyombo vya Ulinzi na Usalama kwenye ngazi ya Wilaya.
Huu ni uelewa wangu kwa kadri nilivyoelewa sheria husika, kama kuna mahala nimekosea niko tayari kukosoloewa maana mimi si mwanasheria kitaaluma. Asanteni
 
Imeshatokea mara kadhaa Rais akateua Ma-DAS. Cheki rekodi.
 
Hakuna mkubwa kwa mwenzake kwa mwenzake kwa kuwa wana majukumu tofauti, DED ni kiongozi wa Halmashauri yaani Local Governmen (Serikali za mitaa) na RAS yuko Central government (Serikali kuu)
 
naongezea tu kwamba huyo Das ni political figure na yule mwingine kabla ya awamu hii alikuwa mtaalamu mbobezi wa mambo flan ya halmashaur mfano utawala nk
 
Kimaslai na marupurupu na kimafungu nani yupo juu ya mwingine kumbuka masurufu na mafungu ndio nguvu ya Kiti na Cheo.Hivyo mi naona DED ndio kila kitu hao wengine ni vyeo vya kisiasa zaidi.
 
Hakuna tatizo hapo. DAS NI MWAKILISHI WA SEREIKALI KUU KATIKA NGAZI YA WILAYA AKIMSAIDIA DC AKISHUGHULIKA NA MASWALA YA UTAWALA,WAKATI DED NI MAMLAKA YA SERIKALI ZA MITAA INAYOPASWA KUWA HURU. KATIKA DHANA HALISI YA UNG'ATUZI, DED ALITSKIWA KUWA INDEPENDENT LAKINI NI TOFAUTI.
 
Kimaslai na marupurupu na kimafungu nani yupo juu ya mwingine kumbuka masurufu na mafungu ndio nguvu ya Kiti na Cheo.Hivyo mi naona DED ndio kila kitu hao wengine ni vyeo vya kisiasa zaidi.

Kimaslahi DED ana mshiko kuliko wenzie, nimewahi kuona mara kadhaa nikiwa mkoa ....DC au DAS wanaomba omba msaada sana kwa DED kila wanapokwama halafu na mara nyingi DED anakuwa na sifa ya kupiga shule kadhaa wakati wenzie mmmmh!
 
DC na DAS ndo hawakupasa alafu baadhi ya vitengo vilivyo kwa DC km Usalama vikajitegemea kwenye kila halmashauri
 
Kwa awamu hii mtachanganyikiwa sana! Moja wote wanasiasa hii ndiyo mbaya kuliko. N.a. wote wameteuliwa na rais, hivyo ukuu au udogo utategemeana na ukaribu wako na jiwe basi.
 
Ila DAS hana fedha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…