Kati ya DED na DAS nani bosi wa mwingine?

Kati ya DED na DAS nani bosi wa mwingine?

DAS anawajibika kwa RAS, hali kadhalika DED. Hivyo hakuna line ya uwajibikaji wa moja kwa moja wa DED kwa DAS. Hata hivyo kiitifaki DAS yupo juu zaidi ya DED.

Niongeze kwamba DAS anauwezo wa kumuita DED ofisini kwake na akamuagiza cha kufanya. Lakini DED hawezi kufanya hivyo kwa DAS.
 
Nimepata mkanganyiko kujua nani bosi wa mwenzake kati ya DAS na. DED naomba kuelemishwa mwenye kujua.
Huu nao ni ushahidi kuwa wateule wa rais katika TZ ni ngumu hata kufanya kazi. Kwani wote ni wateule wa mkulu na ni rahisi hata kufitiniana.

Angalia hata DC na DED, ndio maana utasikia wilaya fulani DC na DED hawaelewani na hapo mkuu asipoingilia kwa kusitisha uteuzi wa mmoja au wote basi hata maendeleo mnasubiri miaka hata 10.
 
DED = District Executive Director, DAS = District Administrative Secretary & DC = District Commissioner. Wote hao ni kuteuliwa na kutumbuliwa wakati wowote. Nani mkubwa hapo
Mi naona hapo DED ni mpanga mikakati ya maendeleo wakati DAS ni mambo utawala aka Uongozi na DC ni mwanasiasa wa wilaya, huyu wa mwisho hana lolote ila chake ni siasa tu.
 
DAS anawajibika kwa RAS, hali kadhalika DED. Hivyo hakuna line ya uwajibikaji wa moja kwa moja wa DED kwa DAS. Hata hivyo kiitifaki DAS yupo juu zaidi ya DED.

Niongeze kwamba DAS anauwezo wa kumuita DED ofisini kwake na akamuagiza cha kufanya. Lakini DED hawezi kufanya hivyo kwa DAS.
Upo sahihi kabisa, ila vyeo vyao vinafanana yaani hakuna mkubwa zaidi ya mwenzake hata maslahi na stahili zao zinafanana
 
Huu nao ni ushahidi kuwa wateule wa rais katika TZ ni ngumu hata kufanya kazi. Kwani wote ni wateule wa mkulu na ni rahisi hata kufitiniana. Angalia hata DC na DED, ndio maana utasikia wilaya fulani DC na DED hawaelewani na hapo mkuu asipoingilia kwa kusitisha uteuzi wa mmoja au wote basi hata maendeleo mnasubiri miaka hata 10.
DC anateuliwa na Rais wa Jamhuri lakini DED anateuliwa na Waziri wa TAMISEMI. DC anakazi zake na DED anakazi zake, hawaingiliani.
 
DAS anawajibika kwa RAS, hali kadhalika DED. Hivyo hakuna line ya uwajibikaji wa moja kwa moja wa DED kwa DAS. Hata hivyo kiitifaki DAS yupo juu zaidi ya DED.

Niongeze kwamba DAS anauwezo wa kumuita DED ofisini kwake na akamuagiza cha kufanya. Lakini DED hawezi kufanya hivyo kwa DAS.
Hili ndo jibu sahihi
 
Nimepata mkanganyiko kujua nani bosi wa mwenzake kati ya DAS na. DED naomba kuelemishwa mwenye kujua.
Una haki ya kuchanganyikiwa mkuu,hata mimi huwa nachanyikiwa,lakini naona kama wako at par,ingawa wakati mwingine naona kwa vile DAS ndiye kiongozi wa watumishi wote Wilayani,basi DED yuko chini ya DAS.Inachanganya kwa kweli.

Mimi huwa nadhani kuna haja ya kufuta mfumo wa kuwa na Halimashauri, ili kuondoa huo mkanganyiko ambao kiukweli unaleta misuguano na mikanganyiko isiyo ya lazima na hivyo kukwamisha utendaji kwa ujumla.Hivi kwa nini tusiwe na DC na DAS tu na chini ya DAS kukawa na idara mbali mbali ambazo zitashuhulikia issues za Willaya?Huu mfumo wa kuwa na Halimashauri ambao ulikuwepo tangia enzi za ukoloni,ukafutwa mwaka 1972 na kurudishwa tena mwaka 1982,unaongeza tu bureaucracy,matumizi ya fedha yasiyo ya lazima,ugumu wa udhibibiti na hivyo kuongeza uwezekano wa upigaji.Kwa ujumla mfumo huu uko inefficient.

Binafsi sioni faida za msingi za Halimashauri,infact naona kama they are just a liability to the government.
Halimashauri zetu zimeshindwa kabisa ku-meet expectations za Watanzania,zifutwe.
 
DAS anawajibika kwa RAS, hali kadhalika DED. Hivyo hakuna line ya uwajibikaji wa moja kwa moja wa DED kwa DAS. Hata hivyo kiitifaki DAS yupo juu zaidi ya DED.

Niongeze kwamba DAS anauwezo wa kumuita DED ofisini kwake na akamuagiza cha kufanya. Lakini DED hawezi kufanya hivyo kwa DAS.
Upo sawa. DAS anauwezo wa kumuagiza DED/MKURUGENZI, Lkn huyu DED ndiye mwenye mafungu na watumishi wooote uwajuao waliopo karibu nawe Ie walimu, wauguzi, ELIMU nk. DED ni kazi ngumu. Hao wooote, RAS, DAS DC & RC na ma Wizara yote ukiacha ya ulinzi na mambo ya ndani kwa uchache huagiza kwa DED ili atekeleze. DED sio mchezo. Huyu DED siku akiwa Mbunge au Katibu Mkuu nk huwa kiongozi mzuri sana kwa kuwa kaishi na watu/watumishi sana, kalaumiwa na kupongezwa sana tu, so anajua uhalisia wa mambo MENGI.
 
Back
Top Bottom